Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Maoni ya Habari 07/02/2024

Maoni ya habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Kwa Mabadiliko ya Kweli… Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.

Ewe Mwenyezi Mungu, irudishe ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahuma Ameen.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 26 Rajab 1445 H sawia na 07 Februari 2024 M

Umma wa Kiislamu Kamwe Hautasalimu amri kwa Wazayuni wa Kiyahudi na Wanajeshi wa Kimsalaba wa Marekani

Mujahidina wa kaskazini mwa Ukanda wa Gaza bado wako imara katika kulizuia umbile la Kiyahudi linaloungwa mkono na majeshi yote maovu ya Magharibi. Vile vile wamesimama kidete kusini mwa Gaza, huku asilimia 80 ya mahandaki bado yako mbali na macho ya uvamizi wa Kizayuni. Ulimwengu unakabiliwa na kushindwa kutoa silaha za kimkakati kwa umbile hilo, kutokana na majaribio makubwa ya silaha yanayotumiwa na umbile la Kiyahudi dhidi ya Ukanda mdogo wa Gaza. Hakuna silaha yoyote duniani inayoweza kufuta fahamu zenye nguvu za Uislamu, Jihad, Shariah, Khilafah, ushindi na kifo cha kishahidi. Wakati kundi dogo la Mujahidina limeweza kuwashinda makafiri kwa fahamu hizi, ni kipi kitatokea wakati majeshi ya Pakistan, Afghanistan, Misri, Jordan na Uturuki yatakapotaharaki dhidi ya umbile la Kiyahudi, huku wakiwa wamejizatiti na fahamu hizi? Hili halitawezekana mpaka kusimamishwe Khilafah kwa Njia ya Utume katika ulimwengu wa Kiislamu.

20 Rajab 1445 H - 01 Februari 2024 M

Hatia na Kugeuzwa Kwake ni Ulaghai wa Mfumo Uliotungwa na Mwanadamu

Hatia ya Nawaz Sharif, Zardari na watawala wengine wa zamani, na kubatilishwa kwa hatia hizo, pamoja na kesi na hatia za hivi punde zaidi, zote ni ufichaji wa mchezo wa utawala. Hayana uhusiano wowote na uwajibikaji wa kweli. Kwa kweli, kutarajia haki kutoka kwa sheria zinazobadilika kila wakati zinazotolewa na wenye nguvu ni kama kutarajia tiba kutoka kwa ugonjwa wenyewe. Uwajibikaji halisi wa uongozi huu wa kifisadi na wa kibaraka wa kiraia na kijeshi utakuwa tu katika mahakama za Khilafah, ambazo zina historia tukufu ya miaka kumi na tatu ya uadilifu, kupitia kutabikisha Shariah. Mahakama za Khilafah kwa Njia ya Utume zitachukua hesabu kamili juu ya mali iliyoporwa na jinai za wasaliti kwa uhai, mali na heshima ya Waislamu.

21 Rajab 1445 H - 02 Februari 2024 M

Watawala duni Ruwaibidha, Wanasiasa na Makamanda wa Kijeshi Hawana Azma, Uungwana na Uanaume

Mnamo tarehe 31 Januari 2024, Jenerali Syed Asim Munir, NI (M), Mkuu wa Majeshi (COAS) aliongoza Kongamano la 262 la Makamanda wa Jeshi (CCC). Kikao hicho kilisisitiza uungaji mkono usio na shaka kwa Palestina. Makamanda hawa wa kijeshi na wanasiasa hawana ndani yao uwakilishaji Ummah bora zaidi ulioletwa kwa ajili ya wanadamu. Hawana haja ya umahiri wa kukabiliana na umbile ovu la Kiyahudi, ambalo tarehe 7 Oktoba ilithibitisha, bila shaka yoyote, udhaifu wake, na kuthibitisha kwamba ni simbamarara wa karatasi tu. Enyi askari na maafisa wa Jeshi la Pakistan wenye ikhlasi! Ni lazima mutoe kiapo cha utii cha Ba’yah kwa Khalifa ambaye atakuongozeni kufikia ushindi juu ya Mayahudi na wale waliofungamana nao, ili kwamba moja ya mema mawili, ushindi au kifo cha kishahidi, lirekodiwe kwa ajili yenu.

22 Rajab 1445 H - 03 Februari 2024 M

Khilafah Itazalisha Pembejeo Zake za Viwanda Yenyewe

Mnamo tarehe 1 Februari 2024, baraza la mawaziri la serikali kuu liliidhinisha ongezeko la bei kwa dawa 146 muhimu za kuokoa maisha, Radio Pakistan iliripoti. Pakistan ina sekta kubwa ya utengezaji dawa. Hata hivyo, Pakistan inaagiza kutoka nje pembejeo nyingi za viwandani zinazotumiwa kutengeneza dawa. Chini ya mfumo wa dunia wa Marekani, sera za Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) haziruhusu Pakistan kuboresha viwanda zaidi ya kiwango fulani. Matokeo yake, Pakistan imekuwa ni uchumi unaotegemea maduhuli ya bei ghali. Inajisalimisha kwa mfumo wa kilimwengu wa Marekani ili kupata dolari. Khilafah kwa Njia ya Utume itawekeza moja kwa moja katika sekta hii muhimu sana. Itahakikisha uzalishaji wa pembejeo muhimu za viwandani katika sekta zote, pamoja na utengenezaji wa dawa. Itaanzisha mfumo mpya wa kilimwengu kwa msingi wa Uislamu.

23 Rajab 1445 H – 04 Februari 2024 M

Wizi wa Kura ni Kutoa Sura Mpya kwa Uidhinishaji wa Sera za Wakoloni

Ukoloni umeweka maelezo ya sera za baada ya uchaguzi. Yanajumuisha mpango haribifu wa kiuchumi wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, mzozo mbaya na Mujahidina Waislamu wa Afghanistan, kusalimu amri kwa Palestina na Kashmir, usawazishaji mahusiano na Dola dhalimu ya Kibaniani, sera mbovu za kijamii za uliberali mamboleo, shutma dhaifu za kimaneno za kunajisi matukufu ya Kiislamu na utumwa wa sasa wa mfumo wa kilimwengu wa Marekani. Hitaji la wakati huu ni kuuangamiza mfumo huu haribifu wa Marekani. Hilo linawezekana tu kwa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume nchini Pakistan. Enyi Waislamu wa Pakistan! Msichafue vidole vyenu kwa rangi katika chaguzi zinazohakikisha utumwa wa ukoloni. Susieni uchaguzi wa kidemokrasia na mufanye kazi na Hizb ut Tahrir ili kusimamisha tena Khilafah.

24 Rajab 1445 H - 05 Februari 2024 M

Silaha ya Kweli ya Makamanda wa Kijeshi wa Kiislamu ni Iman katika, Kumtegemea na Kumtii Mwenyezi Mungu

Maadamu makamanda wa jeshi walikuwa wamehamasishwa na Uislamu, walizishinda dola za kilimwengu licha ya idadi yao ndogo. Historia ya kijeshi ilijaa mifano kama vile Badr, Yarmouk, Qadsiyah, Ain Jalut na Hattin. Hata hivyo, mafunzo ya kijeshi ya Magharibi yaliangamiza kiungo cha Iman na Jihad. Yaliwafanya makamanda wa jeshi kuwa watumishi wa mfumo dhalimu wa kilimwengu wa Marekani, wasiweze kuupinga. Yalipunguza uzito wa mamilioni ya wanajeshi wa Kiislamu mbele ya watu waoga zaidi. Ugonjwa huu unaolemaza unaweza kuponywa tu kwa kuzingatia ruwaza ya Uislamu pekee. Kwa hivyo, Enyi Majeshi, ipeni Nusrah Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Khalifa atakuwa ndiye atakayekuongozeni katika juhudi za kupata ushindi na kifo cha kishahidi.

25 Rajab 1445 H - 06 Februari 2024 M

Demokrasia Inahakikisha Pakistan iko Chini ya Udhibiti wa Marekani

Mnamo tarehe 5 Februari 2024, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani alisema, "Tunaendelea kufuatilia mchakato wa uchaguzi wa Pakistan kwa karibu kabisa." Marekani inafuatilia uchaguzi katika kila nchi ya Kiislamu kwa makini. Marekani inategemea Demokrasia katika Ulimwengu wa Kiislamu kudumisha udhibiti wake. Wawakilishi waliochaguliwa hutunga sheria kulingana na hongo au vitisho vya wakoloni. Demokrasia ni mlango wazi wa udhibiti wa Pakistan na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na jeshi la Marekani. Demokrasia ni kutawala kwa matakwa ya wawakilishi waliochaguliwa, badala ya maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu ﷻ na Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ. Khilafah kwa Njia ya Utume itafunga milango ya udhibiti wa wakoloni. Wajumbe waliochaguliwa wa Majlis ya Ummah wanamhisabu Khalifa kwa mujibu wa Uislamu pekee.

26 Rajab 1445 H – 07 Februari 2024 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu