Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir/ Ardhi Iliyobarikiwa Palestina:

Hizb ut Tahrir Iliandaa Maandamano Mawili Makubwa Kupinga Uhalifu wa Mamlaka ya Palestina na Ukandamizaji Wake wa Kisiasa

Jumamosi, Juni 26, 2021, Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina iliandaa maandamano mawili makubwa huku kukiwa na hasira iliyoibuka baada ya mwanaharakati wa kisiasa, Nizar Banat kuuawa kutokana na kukosoa kwake juu ya mpango wa chanjo ya tuhuma kati ya Mamlaka ya Palestina na umbile la Kiyahudi. Maandamano ambayo yalifanyika mjini Ramallah na Hebron yalipinga uhalifu wa Mamlaka ya Palestina na ukandamizaji wake wa kisiasa. Wawakilishi wawili kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina Mhandisi Baher Salah na Daktari Ibrahim Al-Tamimi walizungumza na umati. Wawakilishi hao wawili walithibitisha kuuawa kwa mwanaharakati, Nizar Banat, kama jinai kubwa inayomuathiri kila Muislamu.

Mhandisi Baher Salah alionesha katika hotuba yake kuwa Mamlaka ya Palestina na tabia yake ya kinyama ilibuniwa ili kulinda uvamizi, alitoa wito wahisabiwe kwa uhalifu wao na kufichua uhalisia wao. Dkt. Ibrahim Al-Tamimi alithibitisha unyenyekevu wa Mamlaka ya Palestina mbele ya umbile la Kiyahudi ambalo linataka kuwanyamazisha watu juu ya uhalifu wa serikali. Wazungumji hao wawili waliwataka watu kuachana na serikali ya Mamlaka ya Palestina na watu wa Palestina wabaki imara mbele ya wakandamizaji na kwamba hivi karibuni Mwenyezi Mungu (swt) akipenda atatukirimu na Khilafah kwa njia ya Utume. .

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina

Video ya Maandamano Mjini Khalil (Hebron)

Video ya Maandamano Mjini Ramallah

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu