Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan: Ripoti ya Habari 19/09/2021

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan imeendeleza amali umma inazozifanya katika maeneo mbalimbali ya nchi kutafuta rai jumla yenye kutambua hukmu za Uislamu na masuluhisho yake yanayohusiana na nidhamu tofauti tofauti za maisha, ambazo zinazungumzia mada anuwai, ikiwemo mfumo wa utawala katika Uislamu, ukiukaji wa usalama, tatizo la ukosefu wa ajira, mizozo ya kikabila na nyenginezo.

"Mfumo wa serikali katika Uislamu ni mfumo wa umoja na sio mfumo wa majimbo, wa serikali kuu au wa kifalme." Chini ya anwani hii, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilifanya muhadhara wa kisiasa katika jiji la El Obeid mnamo Septemba 1, 2021 mbele ya Gold Siwar Musala, ambapo Ustadh Imam Muhammad alizungumza, akielezea mfumo wa serikali kama mfumo wa umoja umejengwa juu ya msingi wa aya na hadith zinazohitaji dhana ya umoja wa Khilafah au Imama na ambazo zinaharamisha mgawanyiko na hiyo ni kwa sababu ya wingi wa imarati na mamlaka.

Chini ya anwani: "Kupambana na ukosefu wa ajira na kuunda nafasi za kazi ni jukumu la dola," Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Madani walifanya muhadhara wa kisiasa katika kituo cha mabasi cha Soko Kuu mnamo Septemba 7, 2021, ambapo Ustadh Ali Siwar alizungumza, akielezea hali mbaya ambayo watu wamefikia kutokana na ukosefu wa nafasi za kazi kwa kweli, vijana, ambao ndio tegemeo la ujenzi, wanazurura mitaani bila ya kazi!

Hizb ut Tahrir ilifanya mkao wake wa kila mwezi katika jiji la El Obeid mnamo Septemba 11, 2021, ambayo ulipewa anwani: "Usalama wa Uasi nchini Sudan na Njia ya Wokovu!" ambapo Muhammad Qoni Muhammad na Hassan Farah walizungumza. Waraka wa kwanza uliwasilishwa na Bwana Mohamed Qoni, kwa anwani: "Sababu za Kutatizwa kwa Usalama nchini Sudan," akielezea kuwa sababu ya kwanza ni utekelezwaji wa kanuni ya kirasilimali nchini Sudan na upotezaji wake wa upande wa kiroho unaomfanya mwanadamu afanye kazi ili kumridhisha Mwenyezi Mungu na kuzifanya halali na haramu kuwa ndicho kipimo cha matendo yake.

Chini ya kichwa: "Hapana kwa shirikisho, hapana kwa uhuru wa maamuzi, hapana kwa haki ya kujitawala, bali Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume ili kurekebisha na mgogoro wa utawala," Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walifanya muhadhara wa umma katika eneo la Madani katika kituo cha mabasi cha Soko Kuu mnamo Septemba 14, 2021, ambapo Bwana Adam Muhammad alielezea jinsi kafiri mkoloni alivyotumia ubabe wa zana zake katika serikali ya mpito ili kuigawanya nchi nzima.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Omdurman Kaskazini pia walifanya muhadhara wa kisiasa mnamo Septemba 14, 2021 wenye kichwa: "Chama cha siasa ni nini na kinaendelezaje taifa?" Ustadh Walid Muhammad Ibrahim alizungumzia uhalisia wa vyama vya kisiasa, makundi na harakati katika ulimwengu wa Kiislamu na jinsi walivyoibuka.

"Uislamu na usekula ni mistari iliyosambamba kamwe haukutani" chini ya anwani hii, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilifanya muhadhara wa kisiasa katika eneo la Omdurman Magharibi mnamo Septemba 15, 2021 katika soko la Libya, ambapo Profesa Ishaq Muhammad Hussein alihutubia umati.

Katika suala hilo hilo la ukiukaji wa usalama, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walifanya muhadhara wa pamoja wa kisiasa katika maeneo ya Omdurman Kaskazini na Kusini, wenye kichwa: "Jambo la ukiukaji wa usalama linathibitisha udhaifu wa serikali ya kiraia na ushiriki wa upande wa kijeshi,” mnamo Septemba 15, 2021 katika soko maarufu Omdurman, ambapo Wakili Ahmed Abkar, aliyefungua hotuba yake kwa kudhihirisha machafuko ya usalama kuenea katika mji mkuu, yakiwakilishwa kwa wizi, utekaji nyara, uporaji, vitisho kwa visu na wengineyo.

Je! Ni upi uhalisia wa mizozo ya kikabila nchini Sudan na hukmu ya Uislamu kwake? Chini ya kichwa hiki, mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walifanya muhadhara wa umma katika eneo la Kosti mnamo Septemba 18, 2021 katika soko la Rabak, ambapo Ustadh Abdul Majeed Othman Ibrahim alizungumza, ambaye alifafanua uhalisia wa mizozo ya kikabila nchini Sudan na kwamba wao ni migogoro ya bandia na ya kuzuliwa ambayo nyuma yake ni ajenda za siri kwa madhumuni ya kisiasa, yakiwemo kuipasua nchi kuwa vijidola.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu