Ndani ya Ubepari Usalama wa Chakula ni Mazigazi
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kuna mkanganyiko miongoni Wakenya wengi ya kuwa je ilikuwa ni busara kwa uamuzi wa serikali wa kuondosha marufuku ya vyakula vinavyotokana na mazao ya kisaki (GMO). Katika taifa ambalo kila mwaka hukumbwa na uhaba wa chakula unaosababishwa na mambo kadhaa ikiwemo ukame uliosababisha mamilioni ya Wakenya kukabiliwa na baa la njaa kila mwaka, dhana iliyoko ni kwamba vyakula vya GMO ni hatari kwa afya ya mwanadamu na katika kuendesha vyema kilimo.