Mamlaka za Kyrgyzstan Zaendelea Kuwatesa Wabebaji Dawah
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Oktoba 31, 2022 Huduma ya habari ya Kamati ya Serikali ya Usalama wa Kitaifa ya Jamhuri ya Kyrgyz kwenye ukurasa wake wa tovuti iliripoti: “Shughuli za seli ya chinichini ya Shirika la Kidini lenye itikadi kali (REO) “Hizb ut-Tahrir al-Islami” zimekandamizwa. Mnamo Oktoba 27, 2022, ndani ya muundo wa kesi ya jinai iliyoanzishwa chini ya Kifungu cha 332 sehemu ya 2 (Uzalishaji, usambazaji wa nyenzo zenye msimamo mkali) ya Kanuni ya Jinai ya Jamhuri ya Kyrgyz, wanachama 11 wachangamfu wa REO “Hizb ut-Tahrir al-Islami”.