Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kulia Machozi ya Mamba

(Imetafsiriwa)

Habari:

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) mnamo Jumanne ilishutumu ujenzi na uzinduzi wa 'Ram Mandir' iliyojengwa kwenye eneo la Msikiti wa Babri Masjid wenye umri wa karne tano huko Ayodhya nchini India. (Chanzo: Dawn)

Maoni:

Hadithi ya Msikiti wa Babri inaonyesha kuinuka na kuanguka kwa Himaya ya Mughal. Msikiti huu ulijengwa na Mfalme wa kwanza wa Mughal Zaheerud Din Babur na hakuna mzozo wowote uliowahi kuzushwa hadi Waingereza walipofanikiwa kupanda chuki miongoni mwa Waislamu na Mabaniani, yaani, mwaka 1853, wakati dhehebu la Kibaniani - Nirmohi Akhara - lilipodai eneo la msikiti huo likisema kuwa eneo la ibada la Waislamu lilijengwa baada ya kubomolewa kwa hekalu la Mabaniani. Mnamo 1859, utawala wa kikoloni wa Uingereza uligawanya eneo hilo katika sehemu mbili tofauti kwa Mabaniani na Waislamu. Waislamu waliruhusiwa kuswali ndani, huku Mabaniani wakiruhusiwa kuabudu katika ua wa nje.

Mnamo mwaka wa 1885 hatua iliwasilishwa katika mahakama moja nchini ili kupata kibali cha kujenga ‘chabutra’, au jukwaa, mbele ya Msikiti wa Babri, ili kumwabudu Ram (mungu wa Kibaniani). Ombi hili lilikataliwa mara mbili na hakimu akaamuru hali halisi, akisema ilikuwa imechelewa sana kurekebisha “kosa lililofanywa zaidi ya miaka 350 iliyopita”.

Baada ya kugawanyika kwa Bara dogo mwaka 1947, Mabaniani wenye msimamo mkali waliendelea na juhudi zao na mnamo tarehe 22 na 23 Disemba 1949, Serikali ya India ilitangaza msikiti huo kuwa “mali inayozozaniwa” na kufunga lango baada ya sanamu za miungu ya Kibaniani kuwekwa na makasisi wa Kibaniani ndani ya msikiti. Baada ya hapo hakuna swala yoyote ya Waislamu iliyoswaliwa msikitini. Mabaniani, mithili ya wote wasiokuwa Waislamu na wenye chuki dhidi ya Uislamu, waliendelea kujaribu kila njia kufikia malengo yao na harakati kubwa ilianza kujenga upya Mandir badala ya msikiti, na kusababisha ghasia za 1992, na kuua karibu watu 2000.

[مَنْ كَانَ يُرِيدُ الْعِزَّةَ فَلِلَّهِ الْعِزَّةُ جَمِيعًا إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ]

“Mwenye kutaka utukufu basi utukufu wote uko kwa Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye hupanda neno zuri, na a'mali njema Yeye huitukuza.” [35:10].

Katika Uislamu kinachopafanya mahali kuwa patakatifu ni kuamini kwamba Mwenyezi Mungu (swt) ndiye mmiliki wa ulimwengu na Yeye pekee ndiye mwenye haki ya kuabudiwa. Na kumwabudu Yeye ni pamoja na kunyenyekea kikamilifu na utiifu, hata katika kulinda haki za madhimmi (Jizya inayolipa na wakaazi wasiokuwa Waislamu wa Dola ya Kiislamu). Sayyidna Omar (ra) aliwasili Palestina mapema Aprili 637 ziara ya mji, ikiwa ni pamoja na Kanisa la Mtukufu Sepulcher. Wakati wa swala ya adhuhuri, ulipofika, Baba wa Kasisi Sophronius alimkaribisha kuswali ndani ya Kanisa lakini Sayyidna Umar alikataa, na akasema kwamba kama angeswali ndani ya Kanisa baadaye Waislamu wangeweza kudhani kwamba huo ungegeuzwa kuwa msikiti na kwa njia hii Wakristo watanyimwa mojawapo ya maeneo yao takatifu zaidi. Badala yake aliswali nje ya Kanisa ambapo msikiti uitwao Masjid e Umar (msikiti wa Umar) ulijengwa baadaye.

Hata katika Bara Hindi dogo Wamughal waliheshimu hisia za raia wao wa Kibaniani, hii ndiyo sababu uasi wa 1857 kwa msingi wa matumizi ya mafuta ya ng'ombe kwenye cartridges ulipelekea mawimbi ya mshtuko kupitia Mabaniani. Hata kama wasia wa Mtawala Babur kukataza kuchinja ng'ombe waziwazi hautachukuliwa kuwa halisi, majibu ya Mabaniani kwenye cartridges yanaonyesha hawakuwahi kukumbana na aina hii ya ubaguzi chini ya utawala wa Kiislamu.

Tunaona mengi yakitokea kote duniani na Waislamu wameathirika zaidi kwani wao ndio wanaoweza kuutekeleza Uislamu kwa kushikamana na umbile lake la asili. Hakuna nyongeza au mabadiliko yanayoweza kufanywa katika amri za Mwenyezi Mungu (swt). Mchakato wa kubomolewa kwa Msikiti wa Babri na ujenzi wa Ram Mandir umeenea zaidi ya miaka 140. Hili linaonyesha kiwango cha nguvu na uwezo Waislamu walionao juu ya ulimwengu, hata baada ya kuvunjwa kwa nguvu yake kuu, Khilafah.

Tukio hili, kama matukio yote katika ulimwengu wa Kiislamu, ni ishara ya jinsi makafiri wanataka kufuta jina la Uislamu. Wasichokielewa ni kwamba wanaweza kubomoa majengo, wakaua Waislamu kwa kimya cha watawala wa Waislamu lakini hawawezi kuufuta Uislamu duniani. Taasisi kama OIC (Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu) zinaweza kumwaga machozi ya mamba kwa kupoteza msikiti huu kama ambavyo zimekuwa zikifanya juu ya mauaji ya Wapalestina, lakini zinapaswa kuwa na uhakika kwamba Mwenyezi Mungu ameahidi ushindi kwa waumini na siku ambayo Waislamu hawa watasalimu amri watakuwa wamezama katika rehema ya Mwenyezi Mungu, wasaliti na wahaini hawatakuwa na pa kujificha isipokuwa makaazi ya mwisho ya marafiki zao makafiri, yaani motoni.

[الَّذِينَ يَتَّخِذُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِنْ دُونِ الْمُؤْمِنِينَ أَيَبْتَغُونَ عِنْدَهُمُ الْعِزَّةَ فَإِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا]

“Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je! Wanataka wapate kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.” [4:139].

Umma wa Kiislamu unapaswa kuchukua nguvu kutokana na uongofu wa Mtume wa mwisho Muhammad (saw), kufuata njia yake, kukabiliana na magumu yaliyotupwa na kuendelea kujitahidi mpaka wapate ushindi. Mafanikio yanatoka kwa Mwenyezi Mungu na ni lazima tujue kwamba hakuna vita vinavyoshindikana mpaka tuendelee kupigana kwa kujisalimisha kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote, na vita hivi ni kusimamisha utawala wa Mwenyezi Mungu hapa duniani. Iwe tutaiona siku hiyo au la, hatuwezi kukana kutoweza kuepukika. Ikiwa sisi ni sehemu ya mapambano haya, basi sisi ni wanajeshi wa Mwenyezi Mungu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ikhlaq Jehan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu