Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Milipuko Yafichua Kufeli kwa Serikali

Habari:

Mlipuko mkubwa katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut, umewauwa kwa uchache watu 70 na kuwajeruhi zaidi ya 4,000 wengine, waziri wa afya alisema.

Video zinaonyesha moshi ukifuka kutoka katika moto, kisha wingu kwa umbo la uyoga likafuatia mlipuko huo katika bandari ya mji huo.

Maafisa wanalaumu bidhaa zenye uwezo mkubwa wa kulipuka zilizo hifadhiwa katika bohari moja kwa miaka sita.

Raisi Michel Aoun aliandika katika mtandao wa Twitter kuwa "ni jambo lisilo kubalika" kwa tani 2,750 za ammonium nitrate kuhifadhiwa ovyo. (BBC News, 5/8/2020)

Maoni:

Picha zinazoshtua za milipuko miwili jijini Beirut zilizo sambazwa katika mitandao ya kijamii zitabakia akilini mwa wale walioziona. Ukali wa kemikali hizo na athari kwa nyumba na miundomsingi iliyo karibu kihakika hazielezeki. Huku mpaka sasa, sababu halisi bado hazijathibitishwa. Hivi punde ripoti za kuhusika kwa Umbile la Kiyahudi zimejitokeza. Kila wakati ukisonga matukio haya yatazidi kudhihirika.

Bila ya kujali ni nani au nini kilichowasha cheche iliyo pelekea mlipuko huu mkubwa sana tunaona kuwa milipuko yote ya kemikali mwanzo hutoa mshtuko mkali kwa waliosimama kando na huacha athari za muda mrefu juu ya afya ya wenyeji na mazingira. Chernobyl, Bopal, China...kuna kumbukumbu za matukio yaliyopita ambayo kamwe hazitaondoka kwa wale walioathirika hata hadi leo. Ardhi za maeneo haya ambako milipuko au mivujo ilitokea imebadilika kwa vizazi vingi vijavyo. 

Sehemu ambazo viwanda vinazalisha kemikali za ukulima, silaha au matumizi mengine daima kuna uwezekano wa kutokea ajali. Mataifa yanahitaji amali za kiviwanda.

Tatizo hapa ni kuwa kiwanda kilikuwepo katika eneo karibu mno na makaazi ya watu mjini. Kama ilivyokuwa katika majanga ya kemikali yaliyo tangulia katika nchi nyengine zilizo tajwa na mbali na hizi, sehemu ya kusikitisha zaidi ya matukio haya ni kuwa maisha ya watu sio jambo la kutiliwa wasiwasi.

Viwanda vya aina hii vinapaswa kujengwa na kufanya kazi yao katika sehemu za mashambani. Usimamizi wa maeneo ya mjini kamwe haupaswi kupuuzwa. Daima kuna hatari ambapo vyaweza kulengwa na mataifa ya kivita pamoja na matukio ya ajali zisizo za kimakusudi.

Serikali zina jukumu la kusimamia na kufuatilia amali za kiviwanda. Katika serikali iliyoko sasa, viwanda vya kibinafsi vinaweza kukwepa sheria na masharti.

Wafanyikazi wanaweza kunyanyaswa na afya na usalama kulegezwa. Angazo liko katika kupata pesa tu na sio athari za amali hiyo kwa watu walio karibu. Katika baadhi ya hali, mivujo huendelea kwa miaka na athari za afya kugunduliwa na kuonekana lakini hakuna lolote linalo fanywa.

Uislamu una nidhamu kamili ya kiuchumi ambayo huhakikisha amali ya kiuchumi inazalishwa na viwanda vizito kuwemo ndani ya jukumu la kitengo cha viwanda. Haikubaliki kwa viwanda vya kemikali kuendesha shughuli zao kwa msingi wao wenyewe, usio dhibitiwa na kuwa tishio kwa maisha ya watu. Viwanda vimekusudiwa kutumikia taifa kwa njia chanya.

Kimsingi awali na katika hali hii kufeli ni kwa serikali ambayo bado haijasimamia na kamwe haitasimamia mambo ya watu kwa usahihi kwani serikali hii imejifunga kwa kukosa wasiwasi wa kweli kwa watu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Nazia Rehman

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Agosti 2020 06:04

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu