Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mamlaka za Uzbekistan Zaendelea Kupotosha Uislamu kwa Kutumia Maimamu Wafisadi

Habari:

Mnamo Januari 7, kampuni ya utangazaji ya televisheni ya Uzbek kwenye chaneli "Uzbekistan" ilipeperusha kipindi kinachoitwa "Uislamu - kiini na maelezo," ambacho kilijitolea kupinga muhadhara wa video wa ndugu Mahmoud Abdulmumin, ambapo alielezea suala la jihad .

Msimamizi wa kipindi hicho, Ilhom Marupov, mkuu wa maswala ya dini, na msimamizi wa madrasa ya juu Mir Arab - Yuldoshhodjaev Kh., alikanusha madai ya ndugu Mahmoud Abdulmumin kwamba maana ya Kisheria ya jihad ni vita katika njia ya Mwenyezi Mungu au utoaji msaada kwa mali, maneno, na hatua yoyote inayohusiana moja kwa moja na vita.

Msimamizi huyo wa madrasah Mir Arab Yuldoshhodjaev Kh. ilisema kwamba neno jihad linapaswa kuzingatiwa kwa maana ya kimsamiati ya neno hili, ambayo ni, kufanya bidii kubwa katika kufanya kitu, kama kusoma, kusaidia wazazi, n.k, akiviita vitendo hivi jihad. Pia Yuldoshkhodjaev Kh. alisema kuwa leo jihad imefungika tu na ulinzi wa dola na haihusiani kabisa na vitendo vya kijeshi dhidi ya makafiri na kuenea kwa Uislamu kote ulimwenguni.

Maoni:

Kazi changamfu ya Mashabab wa Hizb ut Tahrir ya kurudisha maisha kamili ya Kiislamu, sio tu ardhini, lakini pia kwenye mtandao, inaibughudhi serikali ya Sh. Mirzievayev. Hivi majuzi, serikali hiyo dhalimu umeongeza mashambulizi ya kimfumo dhidi ya Uislamu na Waislamu. Katika mapambano haya, serikali hiyo ya kihalifu hutumia maimamu wafisadi kupotosha Uislamu na kuwatenganisha Waislamu na dini yao.

Maimamu wafisadi, wanawahudumia mabwana zao, bila ya hofu ya Mwenyezi Mungu, wanawaita Mashabab wa Hizb wahaini wa nchi yao, wajinga wasiojua Uislamu, waandaaji wa harakati za kidini, wenye msimamo mkali na magaidi. Lakini juhudi zao zote ni za bure, kwani uongo wanaojaribu kuupitisha kama ukweli hauvumilii kukosolewa.

Huhitaji kuwa mwanasayansi ili usome historia ya kuwasili kwa Uislamu katika Asia ya Kati. Kwa kweli, hakuna mwanahistoria hata mmoja atakayekanusha ukweli kwamba Uislamu ulikuja katika eneo la Asia ya Kati ya kisasa wakati wa Umawiyya kwa njia ya jihad. Mmoja wa makamanda wa majeshi alikuwa Kuteiba ibn Muslim. Maswahaba walipigana sio tu kuihami Madina siku ya Vita vya Moat, bali pia waliikomboa Sham, Iraq, Afrika Kaskazini, n.k., kwa kutumia njia ya jihad. Mtume Muhammad (saw) mwenyewe, kulingana na rai tofauti tofauti, alishiriki katika vita zaidi ya 20. Kuanzia wakati wa kuanzishwa kwa Dola la Kiislamu mjini Madina yenye kung'aa, na hadi kuanguka kwa Khilafah mnamo 1924 katika eneo la Uturuki ya kisasa, jihad ilikuwa na inabakia kuwa njia ya kueneza Uislamu.

Serikali ya kihalifu, inayowakilishwa na Sh. Mirziyayev na maimamu wake wafisadi, wanajionyesha kama wajuzi na watetezi wa Uislamu, wanatafsiri hukmu ya Shariah kama yenye faida kwao. Wakati huo huo, serikali hii ya Taghut haitekelezi hukmu yoyote ya Shariah maishani. Tunaona jinsi watetezi hawa wa "Uislamu wa kweli" wanavyokataza dini kuingilia maisha, na katiba ya nchi hiyo inasema kwamba Jamhuri ya Uzbekistan ni serikali ya kisekula na dini imetenganishwa na maisha, lakini Mwenyezi Mungu anasema katika Qu'ran:

[إِنِ الْحُكْمُ إِلاَّ لِلّهِ]

“Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu.” [12:40].

[وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَآ أَنزَلَ اللّهُ وَلاَ تَتَّبِعْ أَهْوَاءهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللّهُ إِلَيْكَ]

“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu.” [5:49].

[وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللّهُ فَأُوْلَـئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ]

“Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri.” [5:44].

Hatutapata hata hukmu moja ya Shariah katika nidhamu ya kijamii, nidhamu ya kiuchumi, nidhamu ya elimu au nidhamu ya kisiasa za Jamhuri ya Uzbekistan. Kwa nini? Labda kwa sababu huu ndio mfumo wa Taghut, na Sh. Mirziyayev anajifikiria kuwa Farauni mpya ambaye ametangaza vita dhidi ya Uislamu na Waislamu!

Hakuna hata mmoja wa maimamu hawa wafisadi, wanaojifanya kama wawakilishi wa Uislamu, atakayemwambia dhalimu huyu kwamba lazima atawale kulingana na sheria za Mwenyezi Mungu. Hakuna hata mmoja wa maimamu hawa wafisadi atakayemwambia dhalimu huyu kwamba ni kosa kubwa kuwatesa na kuwaua Waislamu ili kuwafanya waachane na dini yao. Na kuna mifano mingi kama hiyo.

Waislamu! Mwenyezi Mungu anatutosha sisi kama mlinzi! Mwenyezi Mungu atatusaidia kuondokana na serikali hii ya kihalifu na maimamu wake wafisadi! Jiungeni na kazi ya Hizb ut Tahrir juu ya mwamko wa Dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume! Mwenyezi Mungu Mtukufu asema katika Kitabu Chake Kitukufu:

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [47:7].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Eldar Khamzin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu