Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mgogoro wa Mafuta ya Kula Nchini Tanzania

Habari:

Tanzania imeendelea kuwa na upungufu wa mafuta ya kula hali inayopelekea kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo, kufanya maisha kuwa magumu, ikiathiri maisha ya wengi katika wananchi wa kawaida na kupandisha bei za vyakula, kwani biashara ya vyakula hutegemea mafuta ya kula.

Maoni:

Kuanzia mwishoni mwa mwaka uliopita, kumekuwa na kupanda kwa bei ya mafuta ya kula katika maeneo mengi nchini kutokana na uzalishaji mdogo. Hali hii inatarajiwa kuendelea mpaka mwezi wa Mei au Juni baada ya mavuno ya alizeti ya mwaka huu.

Mahitaji ya mwaka ya mafuta ya kula nchini Tanzania ni takriban tani 570,000 na uwezo wa uzalishaji kwa sasa ni takribani tani 230,000, hivyo kuna upungufu wa takribani tani 340,000 ambazo huagizwa nje ya nchi hususan Malaysia na Indonesia.

Hii si mara ya kwanza kupanda bei kwa mafuta ya kula. Mwezi Februari 2019 ulitokea upungufu na bei ikapanda, lakini upungufu wa hivi sasa ulianza Novemba 2020. Kabla ya upungufu wa sasa kutokea, lita moja iliuzwa mpaka Tsh 3500 (takribani dolari moja na nusu) lakini sasa inauzwa mpaka Tsh 5000 (takribani dolari mbili na zaidi).

Mwaka 2018, Tanzania ilitangaza mpango wa kuwekeza katika kilimo cha chikichi, alizeti, na ufuta ili kukabiliana na upungufu huu wa mara kwa mara, lakini bado mgogoro wa bidhaa hiyo unaendelea.

Sera ya serikali iliyopo ya viwanda iliyoanzishwa mwaka 2015 iliyodaiwa kutumika kutatua tatizo hili nayo imeonesha kushindwa kukidhi mahitaji na matarajio ya watu. Bila ya kusahau kuwa kodi kubwa nayo inachangia pia kupanda kwa bei ya mafuta ya kula.

Mfumo wa uchumi wa Kiislamu unachukulia mafuta ya kula kuwa miongoni mwa mahitaji msingi (basic needs). Hivyo, dola ya Kiislamu (Khilafah) itahakikisha inafanya hima kubwa kuzalisha, kuagiza na kuweka bei sahali ambayo kila mtu ataweza kuimudu.

Kuhusu sera ya viwanda ya Kiislamu iko huria kwa kila mtu kwa mujibu wa sharia. Dola haitawabagua watu isipokuwa itahamasisha na kuunga mkono uendelezaji viwanda na ubunifu kwa kila mtu, na itatoa kila msaada unaohitajika kuhakikisha mahitaji yote msingi yanapatikana na yale ya anasa / ziada yanafikiwa kwa kadri ya hali.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Said Bitomwa

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu