Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Habari na Maoni
Mateso ya Waislamu wa Uyghur: Afrika ni Mshirika Katika Uhalifu

Habari:
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa (UN) zaidi wa Waislamu wa Uighur milioni moja wamekadiriwa kuwekwa kizuizini ndani ya kambi ambamo wanalazimishwa kuikashifu dini yao na kutoa ahadi ya utiifu kwa Chama tawala cha Kikomunisti cha kikafiri. Mashirika ya utetezi wa haki yameilaumu Uchina kwa muendelezo wa kampeni ya usafishaji kabila. Mnamo Agosti, shirika la habari la Washington Post lilisema kwamba ulimwengu "hauwezi kujitia hamnazo" kuhusiana na kampeni dhidi ya Waislamu. Matukufu ya Kiislamu mfano kibla katika misikiti ikibomolewa, na kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, shule za dini na masomo ya Kiarabu yamepigwa marufuku na watoto kutoruhusiwa kushiriki katika shughuli za Waislamu. (https://www.aljazeera.com, 05/01/2019)

Maoni:
Ulimwengu wote umejumuika katika kuikashifu kisanii Uchina kutokana na sera zake za ukandamizaji wa ndugu zetu wapendwa Waislamu wa Uyghur wanaoishi Mashariki ya Turkistan. Kwa upande mwingine, Bara la Afrika limenyamaza kimya! Uongozi wa Afrika wa watawala vibaraka wamejiunga na vibaraka wenzao Waislamu kutoka katika Ulimwengu wa Waislamu ambao wamo katika hali kama yao ya kunyamaza kimya! Hakuna kiongozi ambaye amejaribu kunyanyua sauti yake au kuiotesha kidole Uchina!

Hatua ya Afrika juu ya sera za Uchina kuhusiana na Waislamu wa Uyghur inatokamana na eti ushirika wa kiuchumi kati ya bara hili na Uchina. Kufikia mwaka 2014, Uchina iliipita Amerika kwa kuwa muwekezaji Na.1 ndani ya Afrika huku takwimu rasmi zikionyesha kuwa Uchina imerekodi zaidi ya dola za marekani bilioni 250 za ushirikiano wa kibiashara na Afrika. Zaidi ya hayo, Uchina ndiyo mshirika wa kibiashara Na.1 wa nchi 138 kati ya mataifa 200 duniani. Muungano wa BRICS ulizindua Benki Mpya ya Maendeleo (NDB) iliyo na makao makuu Mjini Shanghai, Uchina na hivi majuzi 17 Agosti 2017, NDB ilifungua rasmi Kitengo cha Eneo la Afrika (ARC) mjini Johannesburg, Afrika Kusini. Benki hiyo inalenga kuifanya ARC kuwa mchangiaji mkubwa katika maendeleo ya miundo mbinu ndani ya Afrika Kusini na mshiriki muhimu katika ajenda ya maendelo ya Bara hili. Kongamano la mwisho la Ushirikiano wa Uchina na Afrika lililofanyika 3 – 4 Septemba 2018, rais wa China Xi Jinping aliahidi dola za marekani bilioni 60 kwa Bara la Afrika ikijumuisha mikopo, ruzuku na udhamini wa fedha za maendeleo. Pia Xi alitangaza mikakati minane inayolenga kuboresha mahusiano ya Uchina na Afrika ikijumuisha uwekezaji katika masuala ya afya, elimu, usalama, ubadilishanaji tamaduni na kuzidisha usafirishaji wa bidhaa zisizokuwa mali ghafi kutoka Afrika.

Ziada ni kuwa Bara la Afrika ni mjumuiko wa makoloni mengi yanayo simamiwa na watawala vibaraka watumwa waliouza roho zao kwa mabwana zao masekula wakoloni wamagharibi wakiongozwa na Marekani, Uingereza, Ufaransa na washirika wao ikijumuisha Urusi na wengineo. Wamagharibi na washirika wao hivi sasa wanapigia debe na kupitisha sheria na sera za kidhalimu za kimauaji ndani ya nchi zao zikilenga kupambana na misimamo mikali na ugaidi! Sheria na sera zao zimechukuliwa na watawala vibaraka wa Bara hili. Mfano kieneno, Makubaliano ya OAU ya Kujikinga na Kupambana na Ugaidi ya 1999, utekelezaji wa Mpango wa AU wa Kujikinga na Kupambana na Ugaidi wa 2002 na utekelezaji wa Sheria Kielekezi ya Afrika ya Kujikinga na Kupambana na Ugaidi ya 2011. Sheria Kielekezi ambayo ilibuniwa ili kuzisaidia Dola wanachama katika utekelezaji wa vipengee vilivyoko ndani ya nyenzo tofauti tofauti za kibara na kimataifa kuhusiana na kupambana na ugaidi. Hivyo basi kitaifa nchi zikapitisha sheria ikiwemo Kenya ilipitisha sheria ya Kupambana na Ugaidi ya 2012 na Mikakati ya Kitaifa ya Kupambana na Misimamo Mikali ya 2016.

Hakika yote hayo hapo juu yanadhibitisha kuwa Afrika na uongozi wake wa vibaraka watumwa hawana hadhi ya kiutu na kisiasa kuzihesabu sera za kinyama za Uchina kwa kuwa wenyewe wanajihusisha na maovu kama hayo dhidi ya raia zao Barani mote! Zaidi ya hayo, inadhibitisha kuwa Afrika haina mtizamo safi na makini wa kimfumo juu ya ulimwengu, binadamu na uhai. Kwa kuwa mfumo unaotawala ni ule batil wa kisekula wa kikoloni wa kirasilimali unaotokamana na akili finyu unaopigiwa debe na maadui wa Mwenyezi Mungu (swt) ikiongozwa na Amerika na washirika wake. Mfumo huu feki na sheria na sera zake za fujo ndio msingi wa majanga ulimwenguni kote ikiwemo majanga ya kisiasa-kijamii-kiuchumi yanayo shuhudiwa kuanzia Mashariki hadi Magharibi! Afrika imeurithi kipofupofu mfumo huu fisadi na nidhamu zake kutoka kwa mabwana zake; na hivyo hatua yake ni sawa na akili yake iliyojaa sumu na ambayo inaipa kipaombele thamani ya kiuchumi/kimada dhidi ya thamani za utu na ubinadamu!

Hatua ya dharura na msingi ambayo Afrika inatakiwa kuchukua ili kujiepusha na ushirika wa kihalifu ni kukata mahusiano na Uchina, US, UK, Ufaransa, Urusi, Ujerumani n.k ambao wote ni washirika katika kupora mali za Afrika na kuwapiga vita Waislamu na Uislamu kwa kisingizio cha kupambana na misimamo mikali na ugaidi. Pia, wakumbatie mwito wa Khilafah ili kuikomboa Afrika kutoka katika utumwa na kusakama kisiasa-kijamii-kiuchumi hadi kupata utulivu wa kweli unaotokamana na ustawi wa kweli wa kisiasa-kijamii-kiuchumi kwa kutekeleza/kutabikisha Shari'ah (Qur'an na Sunnah) inayotoka kwa Muumba wa viumbe. Ni chini ya Khilafah pekee ambapo Afrika, Waislamu na Uislamu utapata kiukweli hifadhi ya maisha na mali zao dhidi ya wamwagaji damu duniani! Kwa kuwaunganisha wapenzi wa Jihadi ili kuwakomboa waliomo katika utumwa wa sumu ya mfumo wa kisekula wa kirasilimali .«وَإِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika Kiongozi ni ngao nyuma yake mnapigana na munajilinda kupitia yeye."

Link ya Kampeni:
http://www.hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/hizbuttahrir/16793.html

Hashtag ya Kampeni:

#الخلافة_تحرر_تركستان_الشرقية
#Khilafah_Liberates_EastTurkestan

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ali Nassoro Ali
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Agosti 2020 06:38

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu