Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Utiifu wa Hasina kwa Maadui wa Mwenyezi Mungu hauwezi kumzuia Kuanguka kwake Kuliko Karibu

 (Imetafsiriwa)

Habari:

Mpango wa sherehe ya golden jubilee wa Bangladesh uligeuka kuwa kumchungu wakati maandamano makubwa yalipotokea dhidi ya Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, ambaye aliwasili Dhaka mnamo Machi 26 kama mgeni mkuu. Angalau watu 10 waliuawa na makumi kujeruhiwa katika maandamano ya kupinga Modi. Waziri mkuu huyo wa India alialikwa kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa taifa hili la Asia Kusini. Serikali ya Bangladesh ililazimika kupeleka vikosi vyake vya usalama vya mipakani kote nchini kudumisha amani na utulivu. Pia ilizuia matumizi ya Facebook na programu yake ya kutuma ujumbe ili kuzuia uhamasishaji rahisi wa waandamanaji. Waandamanaji hao walimkosoa Modi kwa dori yake inalodaiwa katika mauaji ya watu huko Gujarat mnamo 2002, ambapo watu wasiopungua 1000, wengi wao wakiwa Waislamu, waliuawa. Waandamanaji pia walimkashifu waziri mkuu huyo wa India kwa kuzorota kwa hali ya haki za binadamu huko Jammu na Kashmir, New Delhi na maeneo mengine ya India (TRT World, 29 March 2021).

Maoni:

Waislamu nchini Bangladesh wanakuuza chuki kubwa dhidi ya dola hiyo adui ya Kishirikina na India, ambayo kamwe haikosi kutuletea madhara katika kila fursa. Ni Imani ya watu ndiyo inayowafanya wawachukie wabaguzi dhidi ya Waislamu kama Modi:

]يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ تُلْقُونَ إِلَيْهِمْ بِالْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا بِمَا جَاءَكُمْ مِنَ الْحَقِّ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki mkiwapa mapenzi, na hali wao wamekwisha ikataa haki iliyo kujieni” [Sura Al-Mumtahanah, Ayah 1]. Lakini mithili ya watawala vibaraka wa ulimwengu wote wa Kiislamu, Sheikh Hasina pia anataka kuwa mamlakani kwa kufanya urafiki na maadui hawa makafiri. Anadai kwamba mauaji ya Waislamu huko Gujarat na Kashmir na kubomolewa kwa Msikiti wa Babri na Modi sio kadhia zake. Anapofumbia macho mauaji ya kinyama ya raia wasio na silaha wa Bangladesh na kikosi cha mpaka wa India, damu na utakatifu wa Waislamu nchini India haina thamani kwa kiongozi huyu wa dola kitaifa ya kisekula. Badala yake, alisongea hatua moja mbele na kumwaga damu ya Waislamu waliokuwa wakipinga kwa amani ziara ya Modi nchini Bangladesh. Hii ni muhimu kutambua kwamba hakukuwa na mashambulizi hayo ya vurugu yaliyopangwa mapema kwa vyama vya mrengo wa kushoto ambavyo pia vilikuwa vikipinga ziara ya Modi wakati huo. Kwa hivyo, shambulizi baya la ghafla dhidi ya Waislamu wa kawaida na majambazi wa mrengo wa wanafunzi wa chama cha serikali (Bangladesh Chatra League) na jeshi lake la kijambazi la polisi lilikuwa la makusudi kabisa ili kuwaonyesha Waislamu wanaoandamana kwa amani kama watu wa vurugu na kujenga hofu juu ya Uislamu. Huu ni mtazamo wa mkoloni kafiri wa 'vita dhidi ya ugaidi' aka 'vita dhidi ya Uislamu' ambavyo kwavyo Hasina anataka ulimwengu uwatazame Waislamu wenye ikhlasi wa Bangladesh. Na, kwa kufanya hivyo, anataka kuwahakikishia mabwana wake wa kikoloni wa Kimagharibi kwamba hakuna chaguo kwao isipokuwa yeye kukabiliana na Waislamu nchini Bangladesh. Hivi ndivyo anavyokusudia kutoshea ndani ya njama ya wakoloni ya kukandamiza Uislamu na kuwa kama nguzo yao kubwa zaidi hapa ya kuchelewesha kurudi kwa Khilafah iliyokaribia.

Huku Ummah nchini Bangladesh ukiwa umesimama kidete na kumtegemea Mwenyezi Mungu Azza Wa Jal, Sheikh Hasina ana papatika sana kukwamia madaraka kwa kuwaridhisha maadui zetu makafiri-Washirikina. Mapambano haya yataendelea hadi ushindi wa karibu kutoka kwa Mwenyezi Mungu utakapokuja na tumebarikiwe tena na Khilafah Rashida ili isimamishe tena hukmu ya Mwenyezi Mungu duniani:

]وَمَا جَعَلَهُ اللَّهُ إِلَّا بُشْرَى لَكُمْ وَلِتَطْمَئِنَّ قُلُوبُكُمْ بِهِ وَمَا النَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِنْدِ اللَّهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ]

“Na Mwenyezi Mungu hakufanya haya ila kuwa ni bishara na ili nyoyo zenu zituwe. Na haupatikani ushindi ila kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, na Mwenye hikima.” [Al-Anfaal: 10].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imadul Amin
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu