Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Habari na Maoni

Kutarajia Maendeleo Kutoka kwa Sera za Uchumi wa Kirasilimali ni Ndoto

Habari:

Kwa mujibu wa shirika la msaada la Oxfam, matajiri 26 wanamiliki mali za watu bilioni 3.8 ambao wanajumuisha nusu ya watu masikini duniani. Utajiri wa asilimia 1 ya matajiri ni sawa na jumla ya utajiri asilimia 99 iliyobakia. Ndani ya miaka 10 tangu kuweko kwa janga la kiuchumi, idadi ya mabilionea imekuwa mara dufu. Utajiri wa mabilionea umezidi kwa dola za marekani bilioni 900 mnamo 2018. Mtu tajiri duniani, Jeff Bezos, mmiliki wa Amazon, utajiri wake ulizidi hadi dola za marekani bilioni 112. Asilimia 1 ya utajiri wake ni sawa na bajeti ya afya ya Ethiopia nchi iliyo na watu milioni 105. Masikini wanalipa ushuru wa juu kuliko matajiri. Takribani watu 10,000 kwa siku wanakufa kutokana na ukosefu wa huduma ya afya na milioni 262 ya watoto hawako shule kwa sababu wazazi wao hawawezi kumudu ada, sare na vitabu. Wanawake wanafariki kutokana na ukosefu wa huduma za uzazi na watoto wananyimwa elimu ambayo inaweza kuwa ndiyo njia yao ya kujikwamua kutoka katika umasikini. Mkurugenzi wa Oxfam wa kampeni na sera: Matthew Spencer, alisema: "Namna uchumi wetu ulivyopangiliwa inaamisha kuwa utajiri unazidi na unafungika kwa watu binafsi wachache ilhali mamilioni ya watu wanajitahidi tu kuishi. […]" Baada ya utafiti wote shirika la msaada Oxfam likapigia debe utozwaji ushuru wa asilimia 1 ili kupambana na umasikini. Hilo litapelekea kupatikana kwa takribani dola za marekani bilioni 418 kwa mwaka –ambazo zatoshwa kusomesha kila mtoto ambaye hayuko shule na kutoa huduma ya afya ambayo itaepusha vifo milioni 3. (theguardian.com)

Maoni:

Mwito wa Oxfam wa kuongeza mapato kupitia utozwaji ushuru wa asilimia 1 kwa matajiri kikweli itapelekea kupatikana kwa mahitaji msingi ya kila mujtama duniani. Lakini lengo kama hilo litabakia kuwa ndoto chini ya sera za uchumi wa kirasilimali. Kwani sera za uchumi wa kirasilimali zimekitwa juu ya kuzikabidhi mali za dunia kwa warasilimali wachache, urundikaji wa utajiri kwa wachache na kuwakandamiza wengi ili kumakinisha nidhamu za utawala wa kirasilimali. Pindi mashirika kama IMF na Benki ya Dunia yataendelea kuwepo, hakuna mujtama utakaoweza kufikia maendeleo isipokuwa dola za kirasilimali zenyewe.

Siasa ya uchumi wa Kiislamu inatoa mpangilio kuliko ndoto ya Oxfam ya asilimia 1 ya ushuru. Hii inaitwa Zaka. Zaka ni kiwango kinachochukuliwa kutokana na (Nisab) ambayo inazidi "mahitaji msingi" ndani ya mzunguko wa mwaka mmoja. Zaka ni amrisho la Mwenyezi Mungu (swt). Dola ya Kiislamu inakusanya kiwango cha 1/40 cha dhahabu, fedha, pesa na bidhaa za biashara; na kiwango cha 1/30 kutoka kwa mifugo, na kiwango cha 1/10 kutoka kwa mazao ya ukulima. Waislamu hawahitaji kulazimishwa ili kulipa Zaka; wanatoa kwa moyo mkunjufu kwani Waislamu wanaamini kuwa Zaka inawasafisha na ubakhili, uchafu na madhambi. Na serikali inasambaza mapato hayo ya Zaka kwa vikundi vinane vya watu wanaostahiki kwa mujibu wa Qur'an.

Ulimwengu haujawahi kuona nidhamu inayolenga kuwapatia mahitaji msingi binadamu mpaka walipo uona Uislamu. Siasa ya uchumi wa Kiislamu kufaulu kwake kunatokamana na lengo lake nalo ni kumsimamia kila binadamu pasi na kujali dini, lugha, rangi au jinsia. Lengo lake la kwanza ni kuwasimamia na kuhakikisha mahitaji YOTE msingi ya KILA binadamu na pili mahitaji yake ya ziada kwa kadri ya uwezo wake. Kinyume na urasilimali, lengo la siasa ya uchumi wa Kiislamu sio kuongeza mapato ya taifa au kuzidisha uzalishaji, bali ni usambazaji wa rasilimali kwa njia ya kuhakikisha kuwa mahitaji msingi na ziada yanapatikana kwa kiwango cha juu.

Urasilimali na uhuru wake wa kufanya kazi na kumiliki mali umempelekea mwanadamu katika maangamivu, ukiritimba na ukandamizaji. Umewafanya watu kuvizia mali kwa kila njia na kupelekea kupata mali kupitia uhalifu, udanganyifu, kamare, madawa ya kulevya, ukiritimba, uzalishaji na biashara za aina zote za madawa, umalaya na vitendo vyote haramu na ukandamizaji wa wanyonge. Lakini siasa ya uchumi wa Kiislamu ina hakikisha kuwa kutawala na kumakinisha kwa maadili mema katika mahusiano kati ya watu pamoja na kuwasimamia watu maisha yao.

Katika Uislamu, usimamizi wa mahitaji ya watu binafsi ni jukumu la wanaume wa familia. Lau watashindwa kufanya hivyo, dola itaingilia kati. Kando na mahitaji msingi ya watu binafsi, mujtama nao pia unayo mahitaji kama usalama, afya na elimu. Rasulallah (saw) alisema,

«فَالإِمَامُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهْوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ»

“Imamu (mtawala) wa watu ni mchunga na anajukumu juu ya anaowasimamia).”

Dola za kirasilimali zinajisimamia kupitia ushuru zinazo watoza raia kwa nguvu. Masikini asilimia 10 ya Waingereza wanalipa zaidi ushuru kuliko matajiri asilimilia 10 kutokana na VAT. Katika Uislamu hakuna VAT au ushuru wowote uliowekwa. Uislamu umepiga marufuku faini za mahakama, ushuru wa nyumba na aina zote za ushuru na ada. Uislamu unazitizama kama ukandamizaji. Matumizi yote juu ya mahitaji ya mujtama yanasimamiwa kupitia mapato maalumu kutoka katika Zaka, jizya, kharaj na ushr. Zaidi ya hapo, wasiokuwa Waislamu hawalipi chochote isipokuwa jizya ambayo kiwango chake ni kidogo ukilinganisha na Zaka wanayolipa Waislamu. Uislamu umepiga marufuku aina yoyote ya riba. Riba na Ushuru ndiyo sababu msingi wa gharama ya maisha kuwa juu duniani.

Leo, mtu yeyote mwenye akili anatafuta njia ya kuepukana na nidhamu ya kiuchumi ya kirasilimali. Uislamu unakupa nidhamu ya kiuchumi bora na mbadala yenye kufaulu! Kwa hiyo wasubiri nini? Watu wa Madina nao walitamani wapate njia waachane na vita na ukandamizaji wa kiuchumi uliowakumba kwa miaka mingi. Kisha wakakutana na Uislamu. Wakaikubali nidhamu ya Uislamu kwa asilimia 100 na kutoa ahadi ya utiifu kwa Uislamu na Mtume (saw) ambayo iliwafanya kuwa mfano wa kuigwa wa mujtama ulioendelea.

Waislamu wana funguo ya kuwakomboa wanadamu kutoka katika idhilali ya siasa za kirasilimali na uchumi wake. Zaidi ya hilo, Uislamu unayo nidhamu inayodhamini maisha ya dunia ambayo wasiokuwa Waislamu wanayatamani. Mtu yeyote aliye na akili afanye kazi ya kusimamisha tena serikali ambayo itatekeleza nidhamu hii ya kiuchumi. Au asiweke kikwazo katika kazi hii adhimu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Zehra Malik

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Agosti 2020 06:40

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu