Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Muungano wa Afrika Wafichua Sera ya Chuki dhidi ya Raia Wageni ya Serikali ya Denmark

 (Imetafsiriwa)

Habari:

Katika wiki za hivi karibuni, serikali ya Denmark imekabiliwa na upinzani wa kisiasa na kukashifiwa kitaifa na kimataifa kwa mipango yake ya kuwahamisha wakimbizi hadi vituo vya hifadhi nchini Rwanda.

Serikali ya Denmark imekashifu vikali na Muungano wa Afrika, wakati ilipolaani uamuzi huo wa kuwahamisha wakimbizi hadi nchi zilizo nje ya Ulaya, katika taarifa kwa vyombo vya habari kutoka tarehe 2 Agosti. Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari iliitaja mipango hiyo kuwa ya chuki dhidi ya raia wageni na isiyokubalika, na ilitoa nukta kuhusu Makubaliano ya Wakimbizi ya 1951 na majukumu juu ya Denmark kushikamana nayo.

Inaonekana kana kwamba mipango ya serikali ya Denmark itasitishwa, kwani kutolewa kwa taarifa kwa vyombo vya habari yenye kejeli kama hiyo ni ukataaji wa pamoja.

Maoni:

Mipango ya kuwahamisha wakimbizi hadi Rwanda ilianza mwishoni mwa mwezi Aprili wakati serikali ya Denmark ilipowasilisha mswada wa kuwapeleka wakimbizi katika vituo vya hifadhi ng'ambo.

Kabla ya mswada huo kuletwa, Waziri wa Ushirikiano wa Denmark, Mattias Tesfaye na Waziri wa Misaada ya Maendeleo, Flemming Møller Mortensen, walitia saini makubaliano mawili ya ushirikiano na Rwanda kuhusu ushirikiano juu ya sera ya wakimbizi, na kwa hivyo Rwanda ilichaguliwa kama nchi ya kuwapokea wakimbizi hao waliokataliwa wanaohamishwa kutoka Denmark.

Denmark ilikuwa katika mazungumzo na nchi chache za Kiafrika kuhusu ushirikiano wa sera za hifadhi. Bila ya hata chembe maadili, serikali ya Denmark ilidai kwamba sera ya kuwahamisha wakimbizi hadi nchi zengine itakuwa njia ya kibinadamu zaidi ya kutekeleza sera za hifadhi. Mswada huo hatimaye ulipitishwa tarehe 2 Juni 2021 kwa kura nyingi katika bunge la Denmark.

Ama kwa serikali ya Rwanda, inajulikana kwa ukamataji watu kiholela na kuwatesa wakosoaji. Hivi karibuni, vyombo 17 vya habari vya kimataifa, pamoja na The Guardian viliripoti kuwa Rwanda ni moja ya tawala kadhaa za kidikteta kuweza kununua programu ya uchunguzi kutoka kwa kampuni ya teknolojia ya Kizayuni ya NSO Group. Ni spyware ambayo inaweza kufuatilia msururu wa huduma kwenye simu za smartphone na kwa hivyo kufuatilia watumiaji wake. Programu hiyo hutumiwa kwa kuwajasusi wakosoaji wa serikali katika nchi kadhaa na imesaidia tawala kuwadhulumu waandishi wa habari na wanaharakati. Programu ya ujasusi ya kampuni hiyo imehusika hata katika kesi maarufu ya mauaji ya mwandishi wa habari wa Saudia Jamal Khashoggi.

Nchi za Kiafrika, na haswa Rwanda zilikusudiwa kutumiwa kama sehemu ya mashukio ya sera kinyama ya kuwarudisha watu nchini mwao ya serikali ya Denmark. Serikali ya Denmark inakinzana na madai yake ya kile kinachoitwa uvumilivu na kuthamini haki za binadamu kwa majaribio ya kuwafukuza wakimbizi hadi nchi nyengine, ambapo haidhamini usalama kwa wapinzani wa kisiasa, wakosoaji, au wakimbizi.

Sera chafu za serikali ya Denmark hazina uhusiano na ustawi wa wakimbizi na sio nukta inayoijali. Lakini kejeli na uovu wa njia hii ni kwamba, sera yao imejikita katika kuwarudisha wakimbizi kwenye kifo na mateso, na kufanya maisha kuwa magumu kwao iwezekanavyo katika mchakato huo, sambamba na kukua kwa hofu ya Uislamu kutoka kwa wanasiasa, vyama vya siasa, na vyombo vya habari.

Sura mbaya na ya kikatili ya Ulaya ya kidemokrasia na huru imefichuka kwa kila mmoja kuona.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Younes Piskorczyk

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu