Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Watawala wa Pakistan Hawatabikishi Uislamu Kikamilifu Huku Wakimpigia Domo Tupu Kipenzi Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)

 (Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 10 Oktoba 2021, Waziri Mkuu Imran Khan alitangaza kuanzishwa kwa Mamlaka ya Rehmatul-lil-Alameen (Rehema kwa Wanadamu) nchini ili kuhakikisha utekabikishaji wa mafundisho ya Mtume Mtukufu (saw) katika jamii. "Ni imani yangu kwamba nchi haiwezi kuendelea bila ya kufuata mafundisho ya kweli ya Uislamu kwa sababu mambo kadhaa yameingia katika jamii ya Pakistan kuizuia isisonge mbele," Waziri Mkuu Imran Khan alisema. Mamlaka hiyo itajumuisha mwenyekiti na wanachama sita, huku Waziri Mkuu Imran Khan akiwa kama mlinzi mkuu wa kamati hiyo.

Maoni:

Kwa muda mrefu, Waziri Mkuu wa Pakistan, Imran Khan, amekuwa akisisitiza kwamba kusudi la mapambano yake ni kuifanya Pakistan kuwa dola kama Madina. Amekamilisha miaka mitatu kati ya mitano ya kipindi chake, lakini anasisitiza juu ya udanganyifu wake uliochosha, huku umaarufu wake ukizidi kufifia. Watu wanakabiliwa na shida kubwa ya kiuchumi huku Rupia ikidumu kushuka dhidi ya dolari, kukiwa na ongezeko la ushuru, bei za nishati, gharama ya vyakula vikuu na ukosefu wa ajira kila wakati. Kwa hivyo, mithili ya watawala waliotangulia, Imran Khan anajaribu kuwapumbaza Waislamu wa Pakistan kwa ishara tupu. Ametangaza kuanzishwa kwa Mamlaka ya Rehmatul-lil-Alameen nchini kujifanya kujali mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).

Ni amri ya Mwenyezi Mungu (swt) kuhukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Yeye (swt) kupitia Mtume Wake (saw). Mwenyezi Mungu (swt) asema,

 [فَاحۡكُمۡ بَيۡنَهُمۡ بِمَاۤ اَنۡزَلَ اللّٰهُ]

“Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu” [Surah Al-Maidah 5:48]. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisimamisha dola ya kwanza ya Kiislamu mjini Madina na kuanzia siku ya kwanza kabisa alitabikisha yale yote yaliyokuwa yameteremshwa. Baada ya kukamilika kwa Wahyi, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), Maswahaba zake (ra) na Waislamu waliokuja baada yao, kizazi baada ya kizazi, wote walitabikisha Uislamu kwa ukamilifu na kuulingania Uislamu kupitia Dawah na Jihad. Ikiwa Imran Khan alikuwa mkweli kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ondoa riba, kuziunganisha Pakistan, Afghanistan na Asia ya Kati kama dola moja, angekata muungano na Amerika, kukataa zana za wakoloni kama IMF, kutangaza mafuta, gesi na madini kama mali ya umma, kuondoa ushuru wote kwa masikini na wenye madeni, kuitenganisha sarafu na dolari, kutoa sarafu kwa msingi wa dhahabu na fedha, kuondoa sheria zote za Kiingereza, kuvua sheria zote kutoka kwa Quran na Sunnah, kuondoa demokrasia na kusimamisha Khilafah.

Lakini, badala ya kutawala kulingana na Sunnah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), watawala wa sasa wa Pakistan wanatangaza mdomo mtupu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Rehmat-ul-lilAlamin. Kwa kuufunga ueneaji wa Uislamu kwa juhudi za wanachuoni watukufu, wanatelekeza jukumu lao la kueneza Uislamu kupitia Da’wah na Jihad iliyoandaliwa na dola. Ni Khilafah kwa Njia ya Utume pekee ndiyo itakayotabikisha Uislamu kwa ukamilifu, kuhakikisha kuwa Uislamu unatawala juu ya mifumo mwengine ya maisha. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

 [إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللَّهِ وَالْفَتْحُ * وَرَأَيْتَ النَّاسَ يَدْخُلُونَ فِي دِينِ اللَّهِ أَفْوَاجًا]

“Itakapo kuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ushindi, Na ukaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi.” [Surah An-Nasr 110: 1-2]

 Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
MhandisiShahzad Shaikh
Naibu Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu