Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Tume ya Amerika ya Uhuru wa Kidini wa Kimataifa (USCIRF): Zaidi ya Wafungwa wa Kidini 2,000 wako katika Magereza ya Uzbekistan
(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 13/10/2021, RFE / RL ilichapisha yafuatayo: “Mnamo Oktoba 13, Tume ya Amerika ya Uhuru wa Kidini wa Kimataifa (USCIRF) ilichapisha ripoti yake ya mara kwa mara juu ya Uzbekistan. Ripoti hiyo inasema kuwa kuna wafungwa zaidi ya 2,000 wa kidini wanaozuiliwa katika magereza ya Uzbekistan, 81 kati yao wametambuliwa.”

Mwandishi wa ripoti hiyo, Steve Swerdlow, ripota wa Kongamano la Haki za Binadamu katika Asia ya Kati, alisema kuwa kati ya waumini 81, wengi wao waliteswa au kukumbwa na aina nyengine za udhalilishwaji.

Ripoti ya sasa ya Tume ya Amerika ya Uhuru wa Kidini wa Kimataifa ilikuwa na kichwa: "Wafungwa wa Kidini na Kisiasa wa Uzbekistan: Kushughulikia Urithi wa Ukandamizaji."

Maoni:

Ni kana kwamba kamati hii ya Amerika imegundua tu sasa kwamba kuna wafungwa zaidi ya 2,000 wa kidini katika magereza ya Uzbekistan!! Miaka 20 ya umwagaji damu wa Amerika na kiu ya damu nchini Afghanistan - ingawa ilipigana kwa zana za kijeshi zenye nguvu zaidi ulimwenguni - haikupata ushindi; badala yake Amerika ilifurushwa kutoka nchi hii kama Umoja wa Kisovyeti ulivyofurushwa, bali kwa unyanyapaa uchungu zaidi. Na majaribio yote ya kuficha aibu yake hayakuregesha sifa yake ya zamani. Ilihisi shauku ya Mujahidina wa Ummah katika mashambulizi ya Taliban. Wameona wazi nguvu ya Ummah huu ambao utaibuka ikiwa mipaka bandia ambayo makafiri wameiweka kati ya Afghanistan, Pakistan, Asia ya Kati na nchi zengine itaondolewa. Kwa hivyo, wanachukua kila hatua mbaya kuzuia Ummah huu kupata nguvu yake ya zamani isiyoweza kudhibitiwa. Uthibitisho wa hatua hizo za aibu za Amerika ni kwamba wanatoa malalamishi juu ya wafungwa katika magereza ya Uzbekistan ambao waliteswa, kuuawa na kuhukumiwa kifungo miaka 20 iliyopita, kana kwamba wanalijua hili leo tu! Haki za Binadamu nchini Uzbekistan zimekiukwa kwa muda mrefu, na sio leo tu. Kama ilivyo katika nchi zote za Kiislamu ambapo zimekiukwa kwa miaka mingi. Ajabu ilioje hii!!!

Je! Ni kwa nini makauboi wanaozungumza kuhusu 'hali kwenye sayari ya Mars' ghafla wanahitaji kuwakumbuka wanachama wa Hizb ut Tahrir na ndugu zetu wengine ambao waliteseka na bado wanateseka katika bahari ya shida mbaya kwa robo ya karne iliyopita?! Je! Hali dola hii ya aibu, ambayo imezoea kupiga kelele na kukuza upuuzi juu ya haki za binadamu, haioni hali mbaya na ya kinyama ya Waislamu wa Uyghur huko Turkestan Mashariki?! Je, haisikii kilio cha mateso ya Waislamu katika nchi kama Syria, Yemen na Palestina?! Ilhali ulimwengu wote unapiga kengele juu ya hili! Ama sivyo?! Ni wazi kwamba Amerika, Urusi, China na dola zengine za kikoloni za kikafiri zinaiangalia Asia ya Kati ikiwemo Uzbekistan kwa sababu ya rasilimali zake ya kujaza vinywa mate. Amerika haijali kwamba Waislamu bado wako kizuizini nchini Uzbekistan na kwamba rais wa sasa pia anaendeleza kiu ya mtangulizi wake ya damu. Badala yake, inaogopa kuungana tena kwa Umma mzima na kurudi kwenye nguvu zake za zamani kwa karne kumi na tatu. Kwa hivyo ‘Haki za Binadamu’ ni kisingizio tu!!

Enyi Waislamu nchini Uzbekistan: Msidanganywe na makafiri wa kikoloni wanaopiga kelele juu ya ukiukaji wa Haki za Binadamu kwa kuwakasirikia watawala vibaraka kwenye ardhi yenu safi na juu ya tishio la kushambuliwa na ndugu zenu katika nchi jirani! Nyinyi ni kiungo kisichoweza kutenganishwa cha Ummah mtukufu na mwili wa Uislamu usioweza kushindwa. Azma yenu imetoka katika Uislamu na katika imani! Sababu pekee ya Wamagharibi walafi na wenye tamaa ya kuwazungukeni ni hofu yao kwa Khilafah ya Kiislamu ambayo inaonyesha dalili za kurudi kwake katika jukwaa la kimataifa. Namna wanavyojitahidi kwa nguvu vipi kuzuia njia ya kurudi Khilafah, Khilafah Rashida hakika atarudi ulimwenguni tena, Mwenyezi Mungu akipenda.

 [وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Islam Abu Khalil – Uzbekistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu