Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ethiopia ilikuwa ni Kito cha Thamani katika Taji la Africa chini ya Khilafah

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 19 Oktoba 2021, BBC iliripoti kwamba shambulizi la anga katika mji wa Tigray nchini Ethiopia liliua raia. Eneo hilo kwa sasa linakabiliwa na taharuki na kundi la waasi la Tigray Peoples Liberation Front (TPLF) linalopambana na serikali iliyoasisiwa ya Ethiopia.

UNICEF inakadiria kuwa zaidi ya watoto 100,000 Kaskazini mwa Ethiopia wako katika hatari ya njaa kutokana na machafuko hayo. Mzozo huo pia umewaweka wanawake katika hali ya ukosefu wa usalama huku ukiukwaji wa haki za binadamu ukienea na mashambulizi dhidi ya wanawake yakiongezeka katika machafuko hayo. Zaidi ya raia milioni 1 pia wamelazimika kuyahama makaazi yao.

Maoni:

Migogoro, vita na njaa sio hali ya kawaida ya eneo hili, ingawa inaonekana kuwa jambo pekee tunalolinasikia kulihusu.

Ethiopia hapo awali ilijulikana kama Abyssinia na ilikuwa nchi pekee katika bara ambayo haijawahi kukoloniwa. Ina historia ya uongozi na nguvu ya kikanda. Kwa kweli, Harar, mji wake wenye ushawishi mkubwa zaidi, ulianzishwa zaidi ya miaka elfu moja iliyopita na eneo hilo likaukubali Uislamu kama mfumo wake wa utawala. Ulikuwa mji wa kwanza ambao Waislamu wa kwanza walihamia baada ya kukimbia Bara Arabu. Harar ulikua na kuwa njia kuu ya biashara kati ya Afrika, India, na Mashariki ya Kati na ulikuwa ni lango wa kuenea kwa Uislamu katika Pembe ya Afrika. Idadi yake ya Wakristo wa dhehebu la Orthodox inathibitisha kwamba watu waliishi kwa maelewano na kuheshimiana kihistoria.

Miundombinu yake iliyoshamiri chini ya Khilafah inathibitishwa kwa kuwa ina mkusanyiko mkubwa zaidi wa misikiti kwa kila kilomita moja mraba duniani. Mara nyingi hujulikana kama mji wa nne mtakatifu zaidi wa Kiislamu na kujulikana kwa Kiarabu kama Madeenat-ul-Awliya (Mji wa Watakatifu). Watu mashuhuri wa Kiislamu, pamoja na watawala waliotumia Quran na Sunnah, waliruhusu eneo hilo kustawi kama mfano mzuri wa hadhara. Bilal ibn Rabah alikuwa mmoja wa Maswahaba wanaotegemewa na waaminifu zaidi wa Mtume Muhammad (saw) ambaye alikuwa mtumwa wa Kihabeshi aliyeachwa huru na akawa mmoja wa maswahaba wa karibu na kutegemewa zaidi wa Mtume (saw). Bilal alikuwa wa kwanza kuteuliwa mwadhini wa swala. Pia aliteuliwa kuwa Mlinzi wa Hazina (Bayt al-Mal).

Ethiopia yenyewe inachangia karibu asilimia 3 ya soko la kahawa la kimataifa. Kahawa sasa inachangia takriban nusu ya mauzo ya nje ya Ethiopia na inaajiri takriban robo ya wakaazi, kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja. Hoja zilizotolewa ni chache tu kuonyesha uwezo mkubwa ambao haujatumika unaodidimizwa na ufisadi na mivutano ya madaraka ya kipote cha wachache wasiozaingatia sheria wanaoendesha nchi.

Ni pale tu taifa hili litakapoachiliwa kutoka katika mkono wa fikra za kiliberali za kirasilimali, na kuikumbatia dini ya kweli Mwenyezi Mungu (swt) aliyoiweka wazi katika mifumo yote, ndipo mfarakano na ukosefu wa utulivu wa eneo hili utaondolewa na uwezo kamili wa taifa hili utaweza kufikiwa.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu