Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Amerika ni ya Mwisho Kutetea Haki za Binadamu
(Imetafsiriwa)

Habari:

Huku uhusiano ukizidi kuwa mbaya kati ya Beijing na Washington, Rais Joe Biden alitia saini sheria mpya mnamo siku ya Alhamisi (24 Disemba 2021) ya kupiga marufuku bidhaa zinazotengenezwa katika jimbo la Xinjiang la China kwa sababu ya ukandamizaji wa China kwa idadi yake kubwa ya Waislamu wa Uighur walio wachache.

Ikisukumwa na wanachama wa Bunge la Congress la Amerika, sheria hiyo ilipitishwa katika Baraza la Wawakilishi pamoja na Seneti kwa itifaki ya kura mapema mwezi huu. (Chanzo: Aljazeera)

Maoni:

Hii ni katika wakati ambapo watawala wa Waislamu ni viziwi kwa vilio vya Waislamu wanaoteseka katika eneo la Turkestan Mashariki (Xinjiang), huku wakiimarisha mikono ya China katika kuwatesa Waislamu. Baadhi ya watawala hao Ruwaibidah duni (wapumbavu madhaifu) wanawakabidhi Waislamu wa Uighur, ambao ni wachangamfu katika kutetea familia zao, kwa China, ili iwatese. Kwa mfano, serikali ya Morocco imeazimia kumrejesha nchini China mwanaharakati wa haki za binadamu wa Uighur Yidiresi Aishan (Idris Hasan).

Ni wakati huu ambapo Amerika inapatiliza mateso ya Waislamu kuweka vikwazo zaidi kwa China kwa maslahi yake. Haya yote ni wakati ambapo kimsingi ni juu ya serikali za Ulimwengu wa Kiislamu kuanzisha ususiaji wa kiuchumi na kisiasa wa China, licha ya hapo awali kusihi kutokuwa na uwezo wa kuwasaidia Wauighur walio hatarini, au kutojua masaibu yao. Ususiaji kama huo ungekuwa somo kali la kutosha kwa China kusahau minong'ono ya Shetani. Ususiaji kama huo ungeweka heshima kwa Waislamu wa Turkestan Mashariki huko Beijing. Kwa hakika China ingezuiliwa na tishio tu la kufungua mlango wa Jihad, hata kama ni watu binafsi na vikundi pekee, au kwa kutishia kuvunja uhusiano wa kiuchumi nayo, na nchi jirani kama Pakistan, Afghanistan na Bangladesh ... au na nchi za mbali zaidi kama vile Uturuki, Hijaz na Misri na kwingineko. Hata hivyo, pamoja na kuwa ni jambo dogo kwa Umma wa bilioni mbili, hili ni hitaji kubwa mno kwa serikali ambazo zimekuwa na uadui na Uislamu na Waislamu wenyewe, zinazowanyanyasa Waislamu hata zaidi ya China kuwanyanyasa Waislamu wa Uighur!

Marekani inapatiliza tu mateso ya Waislamu ili kuhudumia maslahi yake ya kimataifa. Biden kutia saini mswada huo sio ushindi kwa Waislamu au kwa haki za binadamu, kama inavyofanywa kuonekana hadharani. Washington ndio kinara wa maovu duniani na kinara wa ukiukaji haki za binadamu duniani. Tangu siku ya uhuru wake, Amerika haijaacha kukiuka haki za binadamu, haswa ikiwa binadamu hao ni Waislamu. Aidha, Waislamu ni mifano tu, huku orodha ya mifano ikiendelea na kuendelea.

Amerika hutumia mbinu ya ulaghai ya kujifanya kuheshimu na kutetea haki za binadamu kwa kuuamuru ulimwengu na kutia shinikizo zaidi kwa China. Inafanya hivyo ili kufikia uhalifu mkubwa na mkubwa zaidi, pamoja na kuishinikiza China kusalimisha matakwa yake na kuwa chini ya matakwa yake. Hii ni sanjari na tangazo la Wizara ya Biashara ya Amerika na Hazina ya Amerika mnamo siku ya Alhamisi kuweka vikwazo vipya dhidi ya bayoteknolojia ya China na makampuni ya teknolojia ya hali ya juu, yanayotuhumiwa kwa kuweka teknolojia yao mikononi mwa serikali ya China, ili kuimarisha udhibiti juu ya Wauighur. Hazina ya Amerika imepiga marufuku raia wa Amerika kufanya biashara na makampuni manane ya teknolojia ya juu, ikiwa ni pamoja na DJI (Da-Jiang Innovations), kampuni ya kwanza duniani kutengeza droni, ambayo imewekwa katika orodha nyeusi na Wizara ya Biashara ya Amerika miaka miwili iliyopita. Kwa hiyo, kama kizibo cha malengo yake halisi, Washington daima huweka vikwazo kwa watu binafsi na makampuni ya China, chini ya kisingizio cha kupinga dhidi ya hali ya haki za binadamu katika eneo la Xinjiang na ukiukaji unaofanywa dhidi ya Waislamu walio wachache wa Uighur.

Usaliti wa watawala wa Waislamu dhidi ya Waislamu wa Uighur na upatilizaji wa Amerika wa mateso yao lazima uushajiishe Umma wa Kiislamu kuwang'oa watawala hawa na kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume mahali pao. Ni Khilafah pekee ndiyo itakayoyahamasisha majeshi kuwasaidia Waislamu wa Uighur. Na siku hiyo iliyo karibu in shaa Allah (swt), Mwenyezi Mungu (swt) atawapa ushindi Waislamu, hata kwa mikono ya kafiri, kinyume na matakwa yake. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

 (إِنَّ اللَّهَ يُدَافِعُ عَنِ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ خَوَّانٍ كَفُورٍ)

“Hakika Mwenyezi Mungu huwakinga walio amini. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila khaini mwingi wa kukanusha mema.” [Surah al-Hajj 22:38].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bilal al-Muhajir – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu