Jumatano, 08 Rajab 1446 | 2025/01/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Nani Anayeishajiisha Kyrgyzstan Kuondoka kutoka katika Ushawishi wa Putin?

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo Oktoba 9, IA 24.KG, ikitoa mfano wa Wizara ya Ulinzi ya Kyrgyzstan, iliripoti kwamba mazoezi ya "Udugu Usioweza Kuvunjika - 2022" huko Balykchy yalifutiliwa mbali. "Amri na mazoezi ya majeshi "Udugu Usioweza Kuvunjika - 2022", ambayo yalipaswa kufanywa kuanzia Oktoba 10 hadi 14 katika kituo cha mafunzo cha Edelweiss cha kitengo cha kijeshi Na. 20636 huko Balykchy, yalifutiliwa mbali na Wizara ya Ulinzi ya Kyrgyzstan. Sababu ya kughairiwa bado haijajulikana.

Katika mazoezi haya, kama ilivyopangwa, wanajeshi wa Tajikistan walipaswa kushiriki. Walakini, baada ya uchokozi wa kijeshi wa Emomali Rahmon, Wakirgyzstan wengi, pamoja na manaibu wa Jogorku Kenesh, walitaka kwamba wawakilishi wa Vikosi vya Wanajeshi wa Jamhuri ya Tajikistan wasiruhusiwe kushiriki katika mazoezi hayo.”

“Pia, kikosi cha Kyrgyzstan hakishiriki katika mazoezi ya CSTO "Frontier-2022" nchini Tajikistan, ambayo yalifanyika kuanzia Oktoba 17 hadi 21. Taarifa kuhusu hili ilithibitishwa kwa shirika la habari la 24.kg na huduma ya vyombo vya habari ya Wizara ya Ulinzi ya Jamhuri ya Kyrgyz.”

Maoni:

Rais wa Kyrgyzstan Sadyr Zhaparov hakwenda kwenye hafla ya siku ya kuzaliwa ya V. Putin, ambayo ilifanyika katika mkutano usio rasmi wa viongozi wa CIS huko St. Petersburg mnamo Oktoba 7. Ukweli kwamba rais wa Kyrgyzstan alikataa mwaliko huo, vyombo vya habari vilianza kuandika siku moja kabla ya rais wa Urusi kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 70.

Kwa dhahiri, Sadyr Zhaparov aliuchukulia mkutano pamoja na Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Elizabeth Kennedy-Trudeau kuwa muhimu zaidi kuliko mkutano na V. Putin. Tarehe 7 Oktoba, maafisa muhimu wa Marekani waliwasili nchini Kyrgyzstan ili kujadili makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Katika mahojiano yake na vyombo vya habari, Elizabeth Trudeau alisema: "Marekani inaiona Kyrgyzstan kama mshirika imara. Tuko tayari kuendelea na mazungumzo. Kila nchi huru inaweza kuchagua mshirika wake yenyewe. Kyrgyzstan pia inaweza kuchagua mshirika wake. Marekani iko tayari kuwa mshirika huyo.”

Kwa muda mrefu Marekani imeanzisha mpango wa kutenganisha Asia ya Kati na ushawishi wa Kremlin, na hivyo kuanzisha utawala wake juu ya rasilimali asili na rasilimali watu za ardhi hizi. Leo hii, wakati Putin amekwama kabisa katika mzozo wa kijeshi na Ukraine na vikwazo vya kiuchumi vya Magharibi, Marekani iliona ni fursa nzuri kwake yenyewe kufikia mipango yake.

Inaonekana kwamba mamlaka za Kyrgyzstan ni miongoni mwa za kwanza katika eneo hilo kufuata uongozi wa Marekani, wakiachana na sera ya Kremlin. Na hii inajidhihirisha katika nyanja nyingi. Kwa mfano, ushirikiano wa kijeshi. Tunajua kwamba CSTO ni chombo kilichoundwa na Kremlin kama uwiano wa NATO, iliyoundwa na Marekani. Na tunaona jinsi kwa mara ya kwanza, katika historia nzima ya CSTO, mwanachama wa mkataba amekataa kufanya mazoezi katika eneo lake, na pia kushiriki katika mazoezi pamoja na majirani. Zaidi ya hayo, Kyrgyzstan inadai kwamba CSTO inahitaji kurekebishwa.

Kwa sababu ya mzozo kwenye mpaka na Tajikistan, ambao umekuwa ukiendelea kwa miaka mingi, mwaka huu Kyrgyzstan ilisimamisha usambazaji wa makaa ya mawe kwa Tajikistan, na kuongeza usambazaji kwa China na Uzbekistan. Ilisaini makubaliano ya kiuchumi na China na Uzbekistan, inaunda reli ya Uzbekistan-Kyrgyzstan-China, ambayo ujenzi wake unapingwa sana na Kremlin, kwani bidhaa zitakwenda moja kwa moja kwa nchi tofauti tofauti, kupita Kremlin. Baadhi ya benki nchini Kyrgyzstan zimeanza kukataa kutoa huduma kwa kadi za malipo za Kirusi.

Kwa bahati mbaya, mamlaka za Kyrgyzstan, zikishajiishwa na ahadi za Marekani, zilianza kuondoka kwa mpangilio kutoka kwa Kremlin. Lakini huku ni kujidanganya. Kuachana na sera ya mkoloni mmoja, kuingia kwenye mikono ya mkoloni mwingine hakutatui matatizo ya nchi na wananchi.

Watu wa Kyrgyzstan, kwa kuwa ni Waislamu, ni sehemu ya Umma wa Kiislamu, ambayo ina maana kwamba tatizo la Ummah ni tatizo la Kyrgyz, na tatizo la Waislamu wa Kyrgyz ni tatizo la Umma wa Kiislamu. Leo, Waislamu wa Kyrgyzstan wana matatizo sawa na matatizo ya Umma mzima wa Kiislamu, na hili ni ukosefu wa serikali kwa mujibu wa sheria za Mwenyezi Mungu Mtukufu - kukosekana Khilafah. Hii ina maana kwamba suluhu ya matatizo ya Waislamu wa Kyrgyzstan itakuwa ni kuhuisha Dola ya Khilafah Rashida ya Pili kwa njia ya Utume.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Kitabu Chake Kitukufu:

(وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ)

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [24:55].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Eldar Khamzin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu