- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Marekani Yamiliki kwa Kiburi Uhalifu Wote wa Umbile la Kizayuni huko Palestina
(Imetafsiriwa)
Habari:
Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani Jake Sullivan alikutana na maafisa wa 'Israel' akiwemo Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu mnamo tarehe 15 Disemba, 2023. Shirika la habari la Reuters liliripoti kwamba aliwaambia waandishi wa habari kwamba: "Kutakuwa na mpito kwa awamu nyingine ya vita hivi, ambayo inalenga kwa njia sahihi zaidi kulenga uongozi na shughuli zinazoendeshwa kijasusi ... Ni lini hasa hilo litafanyika na chini ya hali gani hasa kutakuwa na mjadala wa kina kati ya Marekani na Israel." Reuters pia iliripoti kwamba "Biden alionya wiki hii kwamba maoni ya kimataifa yalikuwa yanabadilika dhidi ya Israel kwa sababu ya vifo vingi vya raia huko Gaza."
Maoni:
Lugha iliyotumiwa na Sullivan inaonyesha jinsi Marekani inavyochukulia vita hivi kuwa vyake. Badala ya kusema kwa mwelekeo wa ‘Israel inatuhakikishia kwamba...’, alisema kwa majivuno kama ukweli mielekeo mipya ya vita: “Kutakuwa na mpito.” Hata uharibifu wa kutisha huko Gaza ambao umbile la Kizayuni limeufanya unachukuliwa kuwa mwepesi. Shida kulingana na Biden ni kwamba maoni ya kimataifa yanaweza "kuyumba dhidi ya Israel", sio kwamba maelfu ya wanawake na watoto wasio na hatia wameuawa kikatili katika milipuko ya mabomu ambayo inarudiwa siku hadi siku, hata saa kwa saa. Maneno hayana uwezo wa kuonyesha hasira ya haki dhidi ya uhalifu huu ambao mtu yeyote mwenye moyo na akili anaweza kuona kama anataka. Hili ndilo umbile la Kizayuni: lililojengwa juu ya mauaji ya kimbari, lilidumishwa na ubaguzi wa rangi, na sasa linatafuta kutekeleza 'suluhisho la mwisho' kama waNazi walivyofanya hapo awali. Waislamu hawatasahau wala kusamehe. Lakini ni nani ambaye hapaswi kusamehewa?
Wakati aina ya mbegu mbaya ya mbwa inapoingia katika nyumba ya jirani yake na kuwaua watoto wa jirani hadi kufa, kwa hakika mbwa huyo ni lazima auwawe, lakini jirani hatalala usiku akiuliza kwa nini mbwa alifanya kile alichofanya; lilifanya kama mbwa wakali wanavyoweza kufanya. Atamlaumu mwenye mbwa huyo na atafute fidia kutoka kwake. Mmiliki wa mbwa aliyewaita Wapalestina "wanyama watu" na kusema kuwa ataipunguza Gaza na kila siku alitoa matangazo ya mauaji, na kila siku kuua watu wasio na hatia; kulenga nyumba, hospitali na shule, misikiti na makanisa, kukata umeme, maji na chakula ndiye anayepaswa kuhusisha umakini wetu zaidi. Mmiliki ni Marekani ambayo inashikilia kamba ya umbile la Kizayuni na ililipa kila silaha lililoomba na inaendelea kufanya hivyo. Marekani, kwa hiyo, inamiliki uhalifu wake wote.
Biden aliwaambia Wamarekani wa Kiyahudi katika Ikulu ya White House mnamo tarehe 11 Disemba, "Nilipata shida, nilikosolewa vibaya sana na sehemu ya kusini ya jimbo langu na baadhi ya maeneo ya kusini mwa nchi, wakati miaka 35 iliyopita nilisema, 'Wewe. sio lazima kuwa Myahudi ili kuwa Mzayuni. Na mimi ni Mzayuni." Marekani inatoa uungaji mkono wa kidiplomasia usioyumbayumba na ndiye mjumbe pekee aliyepinga azimio la hivi karibuni la Baraza la Usalama la kutaka kusitishwa kwa mapigano huko Gaza. Maoni pekee ya Umoja wa Mataifa yenye uzito wowote ni maoni yake, ambayo yanasisitiza uwongo wa kile kinachoitwa jumuiya ya kimataifa ambayo inaweka na kudumisha sheria za kimataifa.
Wakati tawala za vibaraka wa Marekani katika Mashariki ya Kati zitaendelea kufuata amri za bwana wao hadi zitakapong'olewa, itakuwa ni aibu ikiwa ubeberu wa kithaqafa wa Marekani utapata masikio ya kutaka miongoni mwa vijana na mabinti watukufu wa Umma wa Kiislamu baada ya kuwa wameshuhudia siku hizi za undumilakuwili na unafiki wa maadili wa Magharibi katika vitendo.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdullah Robin