Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ni Fedheha Kubwa Kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Mkuu wa Magaidi Marekani mwenye Kiu ya Umwagaji Damu!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken kwanza alizuru Uturuki kama sehemu ya ziara yake ya Mashariki ya Kati. Baada ya kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje Hakan Fidan, Blinken alipokelewa na Rais Recep Tayyip Erdoğan.

Maoni:

Blinken alizuru Uturuki kwa mara ya pili kama sehemu ya ziara yake ya Mashariki ya Kati kufuatia kuzuka kwa Vita vya Gaza mnamo Oktoba 7. Blinken, ambaye alikuwa amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje Hakan Fidan wakati wa ziara yake ya kwanza, alifanya mkutano na Rais Erdoğan wakati huu.

Mada kuu zilizojadiliwa wakati wa mkutano huo zilikuwa kuingia kwa Uswidi katika NATO na uuzaji wa ndege 40 za kivita aina ya F-16 kwa Uturuki. Inaelezwa kuwa Marekani ilitia shinikizo kwa Uturuki kutochelewesha zaidi kuingia kwa Uswidi katika NATO. Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka kwa vyanzo, mada kuu ya mkutano ilikuwa Gaza. Waziri Fidan alisisitiza haja ya kusitisha mapigano haraka na misaada ya kibinadamu isiyoingiliwa kupelekwa Gaza na akatoa wito wa mazungumzo juu ya suluhisho la dola mbili kuanza haraka iwezekanavyo.

Kukaribishwa kwa Waziri wa dola ya kigaidi mwenye kiu ya umwagaji damu nchini Uturuki ni fedheha ya kihakika. Ni aibu kwa serikali kuushika mkono wa uliojaa damu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Mkuu wa Magaidi, Marekani, ambayo inalisaidia umbile vamizi la Kiyahudi kwa nguvu zake zote kuendelea zaidi kuwauwa Waislamu wa Palestina na ndiye mlinzi wa umbile hilo la Kiyahudi. Hususan kuleta kwa Waziri wa Mambo ya Nje Hakan Fidan suluhisho la dola mbili, ambao ni mpango muovu wa Marekani na unajumuisha mradi wa usaliti, na kutumia nguvu zake zote kwa ajili ya utekelezaji wake ni usaliti kwa upinzani mtukufu wa Waislamu wa Gaza.

Serikali inajaribu kuruhusu maneno yazungumze zaidi kuliko vitendo. Ni kujaribu kuwalisha Waislamu wa Gaza maneno matupu na kuwaokoa Waislamu wa Gaza kutokana na mabomu kwa domo tupu. Licha ya wito wote wa Waislamu wa Uturuki kukomesha shughuli zote za kidiplomasia na kibiashara na umbile la Kiyahudi na kupeleka majeshi hadi Al-Aqsa, serikali imejitia uziwi kwa matakwa yote haya. Imebaki kutojali na isiyoitika wito huu. Badala yake, imedumisha mahusiano ya kidiplomasia na kibiashara na umbile katili vamizi la Kiyahudi linalowauwa Waislamu kwa halaiki. Wakati ilipaswa kukomesha mahusiano haya ya kibiashara, badala yake, iliendelea kutuma meli zilizobeba mafuta na chakula kutoka bandari za Kituruki hadi bandari za umbile la Kiyahudi. Serikali, ambayo imelilisha umbile la Kiyahudi linalowauwa Waislamu wa Palestina meli ilizozituma, inawalaani Waislamu huko Gaza kwa njaa na mateso. Wakati meli zilizobeba mafuta na chakula kwa umbile vamizi la Kiyahudi zikifichuliwa, serikali ilijaribu kujitoa kwa kusema kwamba meli hizi ni za kampuni binafsi na hazina uhusiano wowote na dola hiyo.

Serikali, ambayo inafanya juhudi kubwa ya kupata maslahi ya Marekani katika eneo hilo, inajifanya kuwa Mbuni mbele ya mashambulizi na mateso ya Waislamu. Haiinui hata kidole. Serikali, ambayo inahamasisha njia zake zote kwa kusudi hili pindi Marekani inapotaka, imeyafunga majeshi ambavyo yatamaliza ukatili huko Gaza na kuling’oa umbile la Kiyahudi kutoka kwa Ardhi zilizobarikiwa. Kwa upande mwingine, serikali hiyo hiyo haisiti kupeleka jeshi lake maeneo mingi pindi Marekani inapotaka.

Kwa jumla, heshima na hadhi ya Waislamu haiwezi kamwe kuhamiwa na viongozi hawa waliokufa. Unyanyasaji na mauaji ya halaiki ya umbile nyakuzi la Kiyahudi kamwe hayawezi kukomeshwa. Badala yake, uvamizi huu unaweza kumalizwa na Makhalifa wa Waongofu ambao huiona damu, hadhi na heshima ya Waislamu kama damu yao wenyewe, kama hadhi yao wenyewe na kama heshima yao wenyewe, na wakoloni wote makafiri wanaolilinda umbile vamizi la Kiyahudi watawekwa mahali pao wanapostahili.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yılmaz Çelik

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu