Jumapili, 27 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Operesheni Nyengine Dhidi ya Ugaidi

(Imetafsiriwa)

Habari:

Uongozi wa juu wa Pakistan umeidhinisha kuanzishwa kwa operesheni mpya ya kijeshi Inayoitwa Azm-e-Istehkam. Mpango huo mpya wa kijeshi unatarajiwa kuangazia vitisho vya usalama wa ndani na wapiganaji wenye silaha wanaovuka kutoka Afghanistan, huku kukiwa na taharuki inayoongezeka kati ya Islamabad na watawala wa Taliban jijini Kabul. Mipango ni “kuongeza” juhudi za kupunguza “magaidi” kupitia ushirikiano wa kieneo na majirani wa Pakistan. (aljazeera.com)

Maoni:

Pakistan na Marekani zilianzisha uhusiano huu wa kiushirikiano uliopotoka, ambao uligeuka kuwa uhusiano mbaya baada ya 9/11, kila moja ikiwa na maslahi yake ya kina tofauti. Hii ilisababisha Pakistan kuzindua operesheni kadhaa za kijeshi tangu 2000 ikiwa ni pamoja na Operesheni Radul Fasad na Operesheni Zarb e Azb. Tukitazama nyuma mwanzoni mwa miaka ya thamanini, tunaona kwamba ‘gaidi’ wa leo alionyeshwa kuwa Mujahid anayepigana vita, ambavyo vilionyeshwa kama Uislamu dhidi ya Ukomunisti na kwa hili kupata uungwaji mkono kutoka kwa watu wa Pakistan ilikuwa rahisi. Kwa vile ndani ya nyoyo zao Waislamu wana kupendana wao kwa wao na wamekuwa wakishuhudia manyanyaso na udhalilishaji wa Waislamu duniani kote tangu kuondolewa kwa Khilafah. Katika hali hii, uungaji mkono wa Jeshi la Pakistan kwa upinzani wa Afghanistan uliwapa hadhi ya heshima machoni pa watu. Watu waliunga mkono kwa furaha dori ya Pakistan katika mapambano haya. Kuanzia mafunzo hadi msaada wa kimwili na silaha, kila kitu kilitolewa na Jeshi la Pakistan kwa usaidizi kamili wa Marekani kwani wakati huo misheni ilikuwa kuishinda USSR. Kufikia 1988, tulishuhudia wanajeshi wa Soviet wakianza kujiondoa, kuashiria mwanzo wa mwisho wa uvamizi wa muda mrefu, wa umwagaji damu na usio na matunda wa Soviet nchini Afghanistan. Hamu ya Marekani ya kuwa dola kuu pekee haikuwa ndoto tena na wasaliti wanaodhibiti nguvu walifikiri kuwa ni jambo lisiloepukika kwa ajili ya kuendelea kuwepo kwa dola kuu pekee duniani. Katika safari hii Pakistan na Afghanistan zilitawaliwa na watu waliojali zaidi maslahi yao ya kibinafsi na kuifanya Marekani kuwa na furaha kuliko kuwajali watu wao ambao walikuwa wahasiriwa wa kuzorota kwa kila nyanja ya maisha. Kuanzia 1989-2000, Afghanistan ilikabiliwa na mzozo wa madaraka ambapo makundi ya upinzani hayakuwa tayari kujisalimisha kwa watawala vibaraka. Huu ndio wakati ambapo Mullah Omar alionekana kama mwokozi kwa watu wenye nia ya Kiislamu ya kihafidhina na mapambano mapya yakaanza na adui mpya alitangazwa na Marekani iliingia rasmi Afghanistan baada ya 9/11 na uongozi wa Pakistan ulikumbatia kwa furaha kucheza dori ya msaidizi wa Marekani.

Tangu 2001, operesheni kumi na tano (zinazoripotiwa) zimefanywa katika KPK kuwalenga ‘magaidi’. Nyingi za operesheni hizi zilipangwa, zikilenga eneo ambalo lilionekana kuwa na matatizo. Kwa mfano, Operesheni Rah-e-Rast na Rah-e-Haq zilikuwa katika eneo la Swat, Sherdil ilikuwa Bajaur na Rah-e-Nijaat ilikuwa katika wakala wa Waziristan Kusini. Operesheni mbili kubwa katika nyanja pana zaidi zilikuwa Zarb-e-Azb, iliyoanzia Kaskazini mwa Waziristan na kisha kupanuliwa hadi majimbo mengine, ikifuatiwa na Radd-ul-Fassad ambayo ilikuwa operesheni ya kijasusi zaidi ya kushambulia mitandao ya kigaidi ambayo ilikuwa imeenea kote Pakistan. Kwa tangazo la operesheni hii ya 16, tunahitaji kutazama kile ambacho tumefanikiwa katika miaka hii 23 ya kupambana na adui wa ndani.

Pamoja na hali mbaya ya kisiasa ya kijografia, kipengee cha China pia kimeingia kwenye mizani na serikali sasa inasafiri ndani ya boti mbili na kuziridhisha pande zote mbili kwa wakati mmoja haiwezekani. Kwa kuuawa kwa raia watano wa China mnamo Machi 2024, Pakistan inakabiliwa na shinikizo hili kutoka kwa China kuwalinda wafanyikazi wa China, kutokana na mashambulizi kama hayo, ambayo kulingana na jeshi la Pakistan raia mmoja wa Afghanistan aliyafanya na magaidi walioko Afghanistan walikuwa wameyapanga.

Ikiwa tutaangalia historia ya vita katika Uislamu, tutaona jinsi lengo lilikuwa wazi, jinsi hatua zilipigiwa hesabu zilichukuliwa na jinsi matokeo yalivyokuwa ya uwazi. Katika operesheni zilizotangazwa na kutekelezwa, tunaweza kuwa tumepoteza mengi lakini hatujapata chochote. Ni vigumu kukubali kwamba Jeshi ambalo linasimama miongoni ya majeshi 10 ya juu yenye nguvu zaid kati ya 145 duniani linapata hasara kila wakati huku likipigana na upande ilio na silaha duni, uliofunza watu wake wenyewe. Heshima na hadhi ambayo jeshi la Pakistan lilipata katika kukabiliana na kuwasaidia Waafghani katika kuifukuza USSR na kuunga mkono Jihad ya Kashmir dhidi ya India ilipotea mahali fulani kati ya kubadilishana dori. Watu wenye ruwaza wangeweza kuona yatakuwa matokeo ya vita hivi dhidi ya watu wao wenyewe. Watu mnaoshirikiana kiimani nao, watu ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu amewatangaza kuwa ni ndugu zenu na ameharamisha damu yao.

Hivi sasa, mgogoro mkubwa unaowakabili Waislamu ni mauaji yanayoendelea ya watu wa Gaza. Huu inapaswa kuwa uwanja wa vita kwa jeshi lolote la Kiislamu. Hakuna mgogoro mwingine usioonekana ambayo ni muhimu zaidi kuliko huu na hapa viongozi wetu wanashughulika kutekeleza maandishi yaliyoandikwa na kuelekezwa na adui. Imepokewa kutoka kwa Anas: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«انْصُرْ أَخَاكَ ظَالِمًاأَوْ مَظْلُومًا» قَالُوا:يَارَسُولَ اللَّهِ، هَذَانَنْصُرُهُ مَظْلُومًا، فَكَيْفَ نَنْصُرُهُ ظَالِمًا؟قَالَ: «تَأْخُذُ فَوْقَ يَدَيْهِ»‏

“Mnusuru ndugu yako, akiwa dhalimu au aliyedhulumiwa.” Watu wakauliza, “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)! Huyu tutamnusuru ikiwa amedhulumiwa, vipi basi ikiwa amedhulumu?” Mtume (saw) akasema, “Kwa kumzuia asidhulumu wengine.” [Sahih al-Bukhari]

Kama Waislamu tulio na ufahamu, hili ni jukumu letu kupaza sauti zetu na kuwataka askari katika majeshi yetu waangalie ni nani wanayemnyanyulia silaha, kwani kitendo hiki hiki cha kupigana kinaweza kuwajengea njia ya kuelekea Jannah au Jahannam. Watu ambao ni wa makundi tofauti ya upinzani wote ni Waislamu. Wamedhuriwa na watu wao wenyewe na huenda wamewadhuru ndugu zao Waislamu katika vikosi. Bado tuna muda wa kupigana vita halisi na kuinua bendera ya Rasul Allah (saw). Chini ya bendera hii, tutakuwa na uongozi wa kweli utakaowalinda Waislamu wa dunia hii na kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ikhlaq Jehan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu