Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mashirika ya Leo ya Vyombo vya Habari si Chochote isipokuwa ni Chombo cha Dola Ovu za Kilimwengu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Chaneli ya Australia, ‘60 Minutes’, ilisema kwamba, “Vifo vya raia wasio na hatia ni vya kuhuzunisha. Uharibifu wa miji na vijiji ni wa kutisha. Kinachotokea Gaza, kufuatia shambulizi la mauaji la Hamas nchini 'Israel' Oktoba iliyopita, ni janga ambalo linavuruga ulimwengu wote. Nchini Australia, maandamano ya mara kwa mara yanayounga mkono pande zote mbili za mzozo hadi sasa yamekuwa ya amani. Lakini katika uchunguzi wa pamoja na ‘The Sydney Morning Herald’ na ‘The Age’, ‘60 Minutes’ unaonyesha ushahidi wa kutatanisha unaopendekeza kwamba yote yanaweza kubadilika. Kundi moja la Kiislamu, lenye misimamo mikali, limejipenyeza kwenye mikutano ya wanafunzi katika vyuo vikuu nchini Australia, na kama Nick McKenzie anavyoripoti, lina ajenda fiche mbaya sana.” ‘The Age’ yenyewe ilisema, “Uchunguzi huu wa ‘Masthead’ na ’60 Minutes’ umegundua operesheni kali ya kisasa ya wafuasi wa Hizb ut Tahrir nchini Australia.”

(Chanzo: https://www.youtube.com/watch?v=LrCLf57juLs
https://www.theage.com.au/national/they-prey-on-people-group-banned-in-the-uk-eyes-australian-division-over-war-20240613-p5jlgq.html)

Maoni:

Ingawa vyombo vya habari vinaitwa “nguzo ya nne ya demokrasia,” vikionyesha kutoegemea upande wowote na fikra yake, kama mamlaka ya mahakama kwa mfano, uhalifu uliofanywa na serikali ya Kiyahudi huko Gaza, na katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, ulitosha kufichua madai haya. Uhalifu huo ulifichua ukweli kuhusu vyombo vya habari na wanahabari. Jinai hizo zilionyesha wazi kwamba hakuna mamlaka ya kimaadili au uhalali, bali kwa ajili ya nguvu ya unyama, inayowakilishwa na dola za kimataifa na silaha zao duniani, ikiwemo Ulimwengu wa Kiislamu, ikiwa ni pamoja na watawala, serikali, na taasisi za vyombo vya habari.

Ingawa vyombo vya habari vya Magharibi, na vile vile vya Australia, vinadai kutoegemea upande wowote na vyenye taaluma, matukio ya Gaza yameonyesha tofauti kwa umma. Ni wazi kwamba wanataaluma hao wa vyombo vya habari si chochote zaidi ya vipashio vya kulipwa kwa Wazayuni, Makruseda, na mabepari. makundi haya hayajali maadili yoyote. Yanajishughulisha tu na kutumikia maslahi yao ya kimwili, hata kama hii ni kwa gharama ya watu wanaokandamizwa na kufanywa watumwa, Magharibi na Mashariki. Kwa kweli, ni kesi karibu ya kipekee. Hakika hawasikii furaha ya dopamine katika damu yao, isipokuwa kwa kumwaga damu ya watu wasio na hatia duniani, hasa damu ya Waislamu, watoto, wanawake na wazee!

Ripoti ya uongo na potofu ya ‘60 Minutes’ sio ya kwanza wala ya mwisho. Inaanza ripoti zake kwa maneno ambayo yanaonekana kuwa yasiyo ya upande wowote, ili iweze kuvutia mtazamaji kwenye udanganyifu. Kwanza inaonyesha mauaji ya serikali ya Kiyahudi, kama inavyoonekana kwenye skrini za televisheni na mitandao ya kijamii. Baada ya utangulizi wa chaneli hiyo unaoonekana kutoegemea upande wowote, inaanza matangazo yake ya kukusudiwa. Inatumia mazingira ya chuki dhidi ya Uislamu yaliyoundwa na vyombo vya habari vyenyewe, kwa kuhalalisha, na kisha kumpa udhuru, mchinjaji na uhalifu wake. Vinaweka aina zote za lawama kwa mhasiriwa na mnyonge, hadi kufikia hatua ya kumtuhumu kila anayeishutumu dola ya Kiyahudi kwa jinai zake. Wanamtaja yule anayeshutumu uhalifu huo kuwa gaidi, au mwenye “ajenda fiche mbaya.” Hii ni, bila shaka, bila kutaja hii inayoitwa ajenda fiche mbaya. Wanajua vyema kwamba wakifichua ajenda hii, ambayo ni rahisi kwa wale wanaowatawala wanyonge na wasio na ulinzi, basi jambo lao litafichuka. Hapo itadhihirika kwa watazamaji kwamba ajenda wanayozungumzia ni adhimu, kubwa, na imeteremshwa kutoka mbinguni.

Baada ya zaidi ya karne kumi na nne, fikra ya Shetani haikuweza kutunga uongo mpya, mbali na kashfa ambayo Waarabu wajinga wa kabla ya Uislamu, walitunga waliposema uongo dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Walimtuhumu (saw) kwa uongo na uchawi bila ushahidi. Badala yake, hii ilikuwa ni kinyume na uaminifu na ukweli ambao Mtume (saw) alijulikana kwao. Kadhalika, msimamo wa Hizb ut Tahrir kinyume na Wamagharibi wajinga. Hizb inajulikana katika fikra, njia, au madhumuni. Badala yake, Hizb ut Tahrir inatangaza hadharani yote hayo. Inawalingania watu kwa hayo yote, asubuhi na jioni, kwa hekima, mahubiri mazuri, na majadiliano kwa njia iliyo bora zaidi. Wale wanaosimamia chaneli, kipindi, na wataalamu wengine wa vyombo vya habari wanajua hili vyema. Hata hivyo, wanadai kwamba ajenda ya Hizb imefichwa, na hata ni mbaya. Ni kashfa ya wazi dhidi ya Hizb ut Tahrir, ambayo imebeba Uislamu, Dini ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ameichagua kwa ajili ya watu wote. Ni kufilisika kiakili kwa Magharibi “iliyostaarabika”, na taswira yake huru ya vyombo vya habari, ambayo inaisukuma kuwakashifu wabebaji ujumbe mtukufu wa Uislamu. Hawana uwezo wa kujadiliana kwa hoja na Uislamu, mdahalo na Uislamu, na kuupinga Uislamu kiafikra na kimantiki. Inajulikana kwa uhakika kwamba kufilisika na kutoweza huku ndiko kunakowasukuma kusema uongo na kashfa za moja kwa moja.

Suala la Mwenyezi Mungu (swt) kuifanya Dini yake na wabebaji wa Ujumbe Wake kuwa washindi ni suala la muda tu. Kisha watu wa Mashariki, na mbele yao wale wa Magharibi, watavihukumu vyombo vya uongo vya habari, na udanganyifu utageuka dhidi ya wadanganyifu. Kisha, ujasiri wa wale wanaofahamu uhalisia na ukweli wa Uislamu utaongezeka. Kisha watu wataingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu (swt) makundi kwa makundi. Hakuna chochote juu ya wabebaji wa ujumbe huu adhimu na Dini tukufu isipokuwa subira na kusonga mbele katika njia hii mpaka Mwenyezi Mungu (swt) aifanye Dini yake itawale juu ya mifumo yote ya maisha, hata kama wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu (swt) watachukia hilo.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bilal Al-Muhajir – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu