Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 KURUDI KWA HADHI YA HAGIA SOPHIA KUWA MSIKITI NI ISHARA YA MWELEKEO WA MABADILIKO YA KIHISTORIA KATIKA ULIMWENGU WA KIISLAMU

Habari:

Maelfu ya Waislamu walishiriki katika swala ya Ijumaa katika Hagia Sophia jijini Istanbul kwa mara ya kwanza katika miaka 86. Mapema Julai, mamlaka za Uturuki kwa mara nyengine tena zililigeuza jengo hili la karne ya sita, ambalo limekuwa ni mahafala tangu 1934, kuwa msikiti. (https://ru.euronews.com/2020/07/24/hagia-sophia-reax-status-edit-laptop-1280)

Maoni:

Pasi na shaka, Ummah mzima wa Kiislamu unafurahia kurudi kwa hadhi ya Hagia Sophia kuwa msikiti. Marufuku ya kuswali swala za Ijumaa na jamaa ndani ya msikiti huu imekuweko katika miaka yote 86 iliyo tangulia.

Baadhi ya wanamaoni waligundua wazi kuwa uamuzi wa Erdogan wa kuibadilisha hadhi ya Hagia Sophia kuwa msikiti baada ya miaka 18 ya utawala katika siasa za Kituruki ni jaribio la kujishindia ushawishi juu ya mpiga kura wa Kituruki.

Mnamo 2019 kwa ushindi wake katika uchaguzi wa meya wa Istanbul, E. Imamoglu, kutoka Chama cha Kijamhuri cha Ummah ambacho kiliundwa na Ataturk kilikipa pigo chama tawala cha Raisi R.T. Erdogan cha Uadilifu na Maendeleo ambacho nyadhifa zake zilionekana kutotingishika.

Ni mara ya kwanza tangu kuwepo mamlakani miaka 17 iliyopita kwa chama cha Erdogan kushindwa katika uchaguzi wa meya jijini Istanbul. Fauka ya hayo, wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanywa mnamo Aprili 31, 2019 chama cha Erdogan kilipoteza viti vikuu katika miji mingine miwili mikubwa – Ankara na Izmir. Kiasi ambacho siku kadhaa baadaye watu walitaja maneno ya Erdogan yafuatayo ambayo alisema kuhusu kuwa meya wa Istanbul: "Mtu anayeimiliki Istanbul, humiliki Uturuki yote." "Yeyote anayeimiliki Istanbul anaimiliki Uturuki."

Pasi na shaka, amri iliyotiwa saini na Erdogan mnamo Julai 10, 2020 juu ya kuregea kwa hadhi ya msikiti wa Hagia Sophia itakuwa na athari chanya juu ya kumuorodhesha Erdogan na chama chake miongoni mwa Waislamu wa Uturuki. Lakini, hapa ni muhimu kutoweka umakini sana katika maelezo ya sera ya ndani ya Kituruki, bali katika upande muhimu zaidi wa tukio hili. Kuregea kwa swala za Ijumaa na jamaa katika Msikiti wa Hagia Sophia ni natija ya mwamko wa Kiislamu katika Ummah wa Kiislamu. Hususan, hali ya sasa ya Waislamu nchini Uturuki, hamu yao ya kuurudisha Uislamu na vima vyake ndio mtindo mkuu katika siasa za Uturuki ya zama hizi.

Na katika hali hii, kukwea mamlaka katika nchi za Waislamu ambapo usekula ndio kitovu chake, ilhali kinje zinadhihirisha nguvu za kisiasa za Kiislamu, ni natija na athari ya mchakato huu usio badilishika katika Ummah wa Kiislamu. Juhudi kubwa ambazo dola za kikoloni za Kimagharibi zinatoa ili kuwaweka mbali Waislamu kutokana na Uislamu wao zimeambulia patupu.            

Katika miongo yote hii ya kukosekana utawala wa Sharia katika ulimwengu wa Kiislamu juu ya Waislamu, fikra za utaifa wa Kiarabu na wa Kituruki, vuguvugu la kisiasa la kutaka kuundwa dola moja ya Waarabu (pan-Arabism), Ujamaa wa Kiarabu(Ba'athism), fikra ya ujamaa ya Nasseriya, Ukomunisti, Ujamaa, usekula na demokrasia zilitabikishwa kwa moto na upanga.

Mbali na hayo, licha ya juhudi hizi za wakoloni wazungu, yanayojiri katika ulimwengu wa Kiislamu yanafikia hitimisho lake la kimantiki, nalo ni ushindi mkubwa wa Uislamu, ishara ambayo ni mwisho wa enzi ya watawala kama Abdel Nasser, waliolikejeli vazi la Sharia la mwanamke wa Kiislamu na kuwatia sumu Waislamu kwa fikra za utaifa wa Kiarabu. Leo ni enzi ya wale wanaoitwa Waislamu wa kati na kati bila ya Uislamu, wanaoendelea kuuvaa usekula, kutekeleza vifungu fulani pekee vya Kiislamu, kwa lengo la kuwapotosha Waislamu.

Hata Abdel Fattah al-Sisi, aliyempindua Muhammad Mursi, analazimika kwenda Hajj ili kupata uungwaji mkono na Waislamu wa Misri. Ni kweli, hakuweza kuficha ujinga wake, na akamuomba Mwenyezi Mungu sio kwa kuuelekeza uso wake katika Kaaba, bali mgongo wake, kana kwamba Kaaba ni kivutio cha watalii ambacho upigaji picha wa kibinafsi unapaswa kufanywa dhidi yake.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika Qur'an:

[إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنْفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ لِيَصُدُّوا عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ فَسَيُنْفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ وَالَّذِينَ كَفَرُوا إِلَى جَهَنَّمَ يُحْشَرُونَ]

“Hakika wale walio kufuru hutoa mali yao ili kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watayatoa, kisha yatakuwa juu yao majuto, na kisha watashindwa. Na wale walio kufuru watakusanywa kwenye Jahannam.” [TMQ 8:36]

Wakati umekaribia wa kuondolewa kwa madikteta katika ardhi za Waislamu, na wakati ambapo Waislamu watapata haki yao ya kuishi kwa mujibu wa Uislamu, utajiri wao wa kimfumo na wa kihistoria. Hii ndio itakayo kuwa sababu ya Ummah wa Kiislamu kurudisha utukufu wao wa awali, maendeleo ya kiuchumi na kisayansi, yatakayo uruhusu kwa mara nyengine tena kuwa mwenge wa uadilifu na maendeleo ndani ya bwawa la kiulimwengu la nidhamu zilizo tungwa na mwanadamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Fazil Amzaev

Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Ukraine

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu