Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari - 15/03/2020

Saudi Arabia Inaanzisha Vita vya Kijinga vya Mafuta na Urusi

Hili Ndilo Litakalozamisha Uchumi wa Dunia: dola trilioni 19 ya Madeni Hatari ya Mashirika

Amerika Imeanza Kuondosha Wanajeshi kutoka Afghanistan, asema Afisaa

Maelezo:

Saudi Arabia Inaanzisha Vita vya Kijinga vya Mafuta na Urusi

Katika hatua ya kijinga inayofanana na uongozi wake, Mwana wa Mfalme wa Saudi Mohammad Bin Salman, anayejulikana kama MBS, alibuni janga la mafuta wiki hii lililoshinikiza masoko ya fedha na linaweza kuwaharibia wazalishaji mafuta wa Amerika. Baada ya Saudi Arabia kuashiria kwamba itaongeza uzalishaji wake wa mafuta, bei za mafuta zilishuhudia kuanguka kwa siku moja ndani ya miongo mitatu. The Dow Jones Industrial Average nayo ilianguka kwa nukta 2,000, ikiwa ni nukta kubwa ya kuwahi kuanguka kwake.

Masoko yataweza kujikwamua kutokana na mshtuko wa awali, lakini kiwanda cha mafuta kilichoko na uchangamfu cha Amerika kinaweza kudhuriwa na anayeonekana kama mshirika wa Amerika aliyechupa mipaka katika kuiridhisha. Janga hilo lilitanguliwa na mpango wa pamoja wa Saudi na Urusi wa kupunguza bei za mafuta katika kipindi cha virusi vya corona. Ilhali Uchina na nchi nyingine zikiwa zimefungwa, mahitaji ya mafuta yameshuka kiwango kikubwa, ilhali wazalishaji wa kiulimwengu wanapoendelea kutoa kiwango sawa cha mafuta. Ili kuzuia bei isianguke, OPEC – ikiongozwa na Saudi Arabia na Urusi zilijaribu kufanya mazungumzo ya kupunguza gharama za uzalishaji kwa takribani mapipa milioni 1 kwa siku (bpd). Mazungumzo hayo yalifeli wikendi hii baada ya Urusi kukataa mpango ambao ungeliipelekea kubeba takribani nusu ya upunguzaji. Badala ya kukubaliana kwa mujibu wa hali ya awali na kuifanya imara nidhamu ambayo imekumbwa na mchafuko wa kiuchumi na kijamii, MBS aliamua kuichoma nyumba kabisa. Saudi Arabia ilitangaza kuzidisha uzalishaji wa mafuta kutoka mapipa milioni 9.7 kwa siku hadi mapipa milioni 12.3 kwa siku, kiwango kikubwa ambacho kitapelekea kuingia katika hifadhi yake. Na pia ilitoa kiwango cha upunguzaji bei kwa wanunuzi wa Ulaya, Asia na Amerika – hatua ambayo inalenga kushika mgao wa soko kutoka kwa washindani wake. Kwa upande wa Urusi ilirudi nyuma na kutishia kuongeza uzalishaji wake, ikiweka uwezekano mkubwa wa kushuka kwa masoko ya mafuta. Hatua ya Saudi inaonekana kuwa imelenga kuiadhibu Urusi, lakini ambaye hakuzungumzwa ndiye mlengwa haswa – mzalishaji mkubwa wa mafuta duniani, Amerika. [Chanzo: The Business Insider]

Wasaudi daima wamekuwa wakiutumia vibaya utajiri wa mafuta ya Ummah wa Waislamu ili kuziridhisha nguvu za kigeni.

Hili Ndilo Litakalozamisha Uchumi wa Dunia: Hatari ya Madeni ya Mashirika dola trilioni 19

Kampuni zimetumia miaka tangu kwa janga la kifedha la kiulimwengu kujihusisha na madeni. Sasa, mkurupuko wa virusi vya corona unatishia kuisukuma dunia katika mdororo wa kiuchumi, kwani madeni yatataka kulipwa – kuzidisha madhara kwa uchumi na kuyeyusha masoko ya kifedha. Yakilenga kupatiliza viwango vya chini vya riba, kampuni zilikwenda mbio katika miaka ya hivi karibuni kutoa madeni ambayo malipo yake yangetumiwa kukuza biashara zao. Madeni ya mashirika miongoni mwa yasiyokuwa mabenki yakalipuka kuwa dola trilioni 75 mwishoni mwa 2019 kutoka dola trilioni 48 mwishoni mwa 2009, kwa mujibu wa Taasisi ya Fedha ya Kimataifa. Huku virusi vya corona vikisambaa – vikisababisha kushuka kwa bei za mafuta na kuanguka kwa usafiri na kufungwa kwa viwanda kuanzia Italia hadi Uchina – kuna kuzidi kwa taharuki kwamba makampuni ya kawi, sekta za ukarimu na magari hayatoweza kulipa madeni yao. Hilo linaweza kusababisha upunguzaji wa viwango na kufeli ambako kutapelekea kuvuruga zaidi masoko ya kifedha na kuchanganyika na mshtuko wa kiuchumi. “Kiuhakika hiki ni kiribiti chengine kinachowashwa [karibu] na madeni ya mashirika,” alisema Simon MacAdam, mwanauchumi wa kiulimwengu aliyeko Capital Economics. “Kuna uwezekano mkubwa wa hatari ya kinidhamu.” Katika ripoti yake ya hivi karibuni ya utulivu wa kifedha, Shirika la Fedha la Kimataifa lilitoa ilani kuhusu kuzidi kwa hatari ya madeni ya mashirika, ambapo ilisema yanaweza kuzidisha matatizo na kukithirisha mdororo wa kiuchumi ujao. Shirika hilo lilifanya uchunguzi wa kinadharia kuhusu mshtuko wa kiuchumi ambao ni nusu kiukali kama janga la kiuchumi la 2008. Majibu yaliashiria kwamba madeni ya mashirika yenye thamani ya dola trilioni 19 kutoka katika nchi – Uchina, Amerika, Japan, Uingereza, Ufaransa, Uhispania, Italia na Ujerumani - ipo katika hatari ya kufeli siku za mbeleni ambapo kutakuwa na kiwango kikubwa cha kuanguka kwa sababu kampuni zitakuwa na wakati mgumu kupata kiwango cha kutosha cha fedha ili kulipa. Hiyo itakuwa ni asilimia 40 ya madeni ya masharika. Wimbi la kufeli, au hata mfululizo wa kupunguzwa viwango na ubadilishaji bei, utatingisha nidhamu ya kifedha. “Soko la madeni linakaribia katika nukta isiyokuwa na kurudi nyuma, pale ambapo mzunguko wa madeni hauepukiki na haubadilishiki, kwa kuwa vyanzo vya kifedha vimekauka, wakopeshaji wakikumbana na janga la kutoweza kukopesha kwa kutokuwa na pesa, hasara za madeni zinazidi, wawekezaji wakikimbilia kujitoa na huku wakikumbana na uwezo mchache wa kifedha wakati wanatoka," Oleg Melentyev, mkuu wa mkakati wa mazao ya juu ya mikopo katika Benki ya Amerika, aliwaambia wateja Ijumaa. [Chanzo: CNN]

Kikundi cha mabwenye kimekataa mabadiliko ya kina na kimakusudi kimeiweka nidhamu ya kifedha ya dunia katika msaada wa uhai kupitia kupunguza mihemko. Sasa ambapo virusi vya corona vinazidi kutishia na kuathiri biashara baina ya nchi, wasiwasi umeyakumba masoko ya kifedha kiasi kwamba makampuni mengi hayatoweza kulipa madeni yao hivyo basi kupelekea kuanguka kwa nidhamu ya kifedha duniani.

Amerika Imeanza Kuondosha Wanajeshi kutoka Afghanistan, asema Afisaa

Wanajeshi wa Amerika wameanza kuondoka Afghanistan, kwa awamu ya kwanza ya kuondoshwa kwa wanajeshi kwa mujibu wa makubaliano ya Amerika na Taliban, afisaa wa Amerika alisema mnamo Jumatatu, huku kukiwepo na machafuko ya kisiasa mjini Kabul yanayotishia mpango huo. Mamia ya wanajeshi wanatoka nchini humo kama ilivyopangiliwa awali, lakini hawatobadilishwa kwani Amerika inasonga mbele na mipango yake ya kupunguza vikosi nchini humo kutoka 13,000 hadi 8,600 afisaa huyo alisema. Afisaa huyo alizungumza na The Associated Press kwa sharti asifichuliwe kwani hakutakiwa kujadili harakati hizo kabla kutangazwa hadharani.  Kuondoka huko kuna kuja wakati ambapo viongozi mahasimu wa Afghanistan kila mmoja aliapishwa kama rais katika sherehe tofauti mnamo Jumatatu, wakiweka kizuizi kwa Amerika wakati inapofikiria namna ya kusonga mbele na mpango huo ili kusitisha vita vya miaka 18. Mzozo mkali baina ya Rais Ashraf Ghani, aliyetangazwa mshindi katika uchaguzi uliopita wa Septemba, na hasimu wake Abdullah Abdullah, aliyedai kuwa uchaguzi ulikuwa na udanganyifu pamoja na tume ya malalamishi ya uchaguzi; unatishia hatua zinazofuata na unapelekea kuzusha vurugu jipya. Amerika haikufungamanisha kujitoa huko na utulivu wa kisiasa nchini Afghanistan au matokeo yoyote haswa kutokamana na mazungumzo yote ya amani Afghanistan. Badala yake, inategemea mkutano wa Taliban katika kujifunga na yaliyokubaliwa ili kuzuia “kundi au mtu binafsi yeyote, ikijumuisha al-Qaida, kutotumia ardhi ya Afghanistan kutishia usalama wa Amerika na washirika wake.” Katika makubaliano ya amani, kuondoka kwa wanajeshi wa Amerika kulitakiwa kuanze ndani ya siku 10 baada ya kutiwa saini mpango huo mnamo Feb. 29. Katibu wa Ulinzi Mark Esper alisema mnamo Machi 2 kwamba tayari ashaidhinisha kuanza kujitoa, ambako kisha kutaratibiwa na makamanda wa kijeshi nchini Afghanistan. [Chanzo: Military Times]

Kuna mianya mingi ndani ya mpango huo wa amani kiasi kwamba sio kweli wanajeshi wote wa Amerika wataondoshwa. Katika hali yoyote ile, Amerika itapata udhuru wa kuendeleza uvamizi wake nchini Afghanistan.

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 19 Machi 2020 09:22

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu