Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari - 11/03/2020

Mwana Mrithi wa Ufalme Ajiimarishia Udhibiti

Lebanon Imeshindwa kulipa Deni lake

Saudi Yabwaga Bei ya Mafuta

Maelezo:

Mwana Mrithi wa Ufalme Ajiimarishia Udhibiti

Hii ni kufuatia msururu wa kuwakamata wanawa wafalme wa ngazi za juu, Mwana Mrithi wa Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammad bin Salman aliwaweka chini ya ulinzi wana wafalme wakuu. Mwana mfalme Mohammed bin Nayef, aliyekuwa mwana mrithi wa ufalme wa zamani; kaka yake, mwana mfalme Nawaf bin Nayef; mwana mfalme Ahmed bin Abdulaziz, mwenye miaka 78 ambaye ni kaka wa Mfalme Salman; na mwana mfalme Nayef bin Ahmed, na mtoto wa mwana mfalme Ahmed na mkuu wa zamani wa ujasusi - wote hao walikamatwa na vikosi vya usalama vya Saudi Arabia. Na mamia ya maafisa wa ngazi za chini waliwekwa kizuizini.

Kukamatwa huko kusingelitokea pasi na Mwana Mrithi wa Ufalme Mohammad kutokuwa na udhibiti wa vikosi vya usalama wa ndani pamoja na uungwaji mkono na babake, Mfalme Salman, ambako kunaashiria kuondoshwa huko ni kuimarisha vyeo vyao na kwamba mpangilio wa makubaliano uliokuwa ukitekelezwa na Wafalme wa zamani sasa umekufa.

Lebanon Imeshindwa kulipa Deni lake

Lebanon ni taifa la hivi karibuni kushindwa kulipa madeni yake. Waziri Mkuu wa Lebanon Hassan Diab alitangaza kwamba serikali yake imesitisha malipo ya deni la Eurobond dola bilioni 1.2 lililotakiwa kulipwa mnamo Machi 9, Diab alisema Lebanon itatafuta kupangilia upya deni hilo kubwa. Lebanon kwa mara ya kwanza kushindwa kulipa deni hilo la serikali kutaipelekea kuanguka kiuchumi. Serikali ya Diab imekuwa ikikumbwa na majanga makali ya kifedha na kiuchumi yaliyopelekea miezi ya maandamano na ukosefu wa imani kwa nidhamu ya benki. Suala la ulipaji wa deni la Eurobond dola bilioni 1.2 lilikuwa ni moja katika maamuzi mazito ya baraza lake kuchukua.

Saudi Yabwaga Bei ya Mafuta

Bei ya mafuta ilianguka kufuatia Saudi Arabia na Urusi kutokubaliana kuhusu upunguzaji wa uzalishaji kufuatia athari za virusi vya corona kwa uchumi wa kiulimwengu. Saudi Arabia ilizishtua nchi za OPEC kwa kusukuma kiuwazi kuwa kufanyike upunguzaji huo mkubwa na kwa muda mrefu kuliko matarajio. Urusi ilihisi mshtuko kutoka kwa Saudi Arabia katika mkutano wa OPEC, lakini siku iliyofuata, Saudi Arabia ilijibu kwa kupunguza bei zake za mafuta na kuahidi kwamba itazidisha uzalishaji. Wakati ambapo bei ya mafuta imeshuka hadi nusu ya bei yake ilivyokuwa mwanzoni mwa Januari. Saudi Arabia inategemea zaidi mafuta kuliko Urusi na hivyo kushuka kwa bei hakuisaidii Saudi Arabia, hususan wakati ambapo uchumi wake umeendelea kudorora. Na huku Urusi ikitaabika kiuchumi kwa miaka sasa kutokana na vikwazo vya Amerika kwa hiyo muda huu ni mbaya zaidi kwa bei za mafuta kushuka.

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 19 Machi 2020 09:21

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu