Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Silsila ya Maswali Yaliyowasilishwa kwa

Amiri wa Hizb ut Tahrir

Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah Katika Ukurasa Wake wa Facebook

Jibu La Swali:

Je, Riziki (Rizq) ni Kila Chenye Kuzawadiwa Kifedha?
Kwa: Mohd Temiza
(Imetafsiriwa)

Swali:

Assalam Alaikum Wa Rahamtullah Wa Barakatuh, ewe sheikh mwanachuoni mkubwa,

Naomba kwa ukarimu wako ujibu swali ambalo bado sijapata jibu la kuridhisha, namuomba Mwenyezi Mungu jibu lake liwe mikononi mwenu.

Je, riziki inaishia kwenye pesa tu, ikimaanisha kila kitu kinachoweza kumilikiwa kwa sababu ya Kisheria? Au je, mali katika pesa, rasilimali inayohamishika au isiyohamishika ni sehemu tu ya rizq, na haijumuishi kuwa ndio rizq (riziki) pekee? Kwa mfano, je mke mwema ni rizq (riziki)? Na je, afya, mafanikio na kizazi chema ni miongoni mwa rizq (riziki) pia?

Mwenyezi Mungu akulipeni kheri kwa niaba yetu

Mohammad Al Harithy.

Jibu:

Wa Alaikum Assalam Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Rizq (riziki) ni kila chenye kuzawadiwa:

1- Imekuja katika “Lisan Al-Arab”: [Na riziki tunukiwa ni shina la kauli yako, “Mwenyezi Mungu amemruzuku” ... Mvua huenda ikaitwa riziki, na hilo ni kauli ya Mola Mtukufu: ﴿وَمَا أَنزَلَ اللَّهُ مِنَ السَّمَاء مِن رِّزْقٍ فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا] “…a riziki anayo iteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwayo akaifufua ardhi baada ya kufa kwake,…” [Al-Jathiya: 5]. Na Mwenyezi Mungu (swt) asema: [وَفِي السَّمَاء رِزْقُكُمْ وَمَا تُوعَدُونَ]  “Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyo ahidiwa” [Adh-Dhariyat: 22]. Mujahid akasema ni mvua na huu ni upana katika lugha ... na riziki ya wanajeshi ni matamanio yao, na wanatafuta riziki (irtazaqu), na wanaruzukiwa (Al-Razqa) kwa mara moja, na wingi wake ni Al-Razaqaat, ambayo ni matarajio ya wanajeshi... na irtazaqa yaani wanajeshi walichukua riziki zao. Na maana ya neno lake (swt): : [وتَجْعَلونَ رِزْقَكُم أنكم تُكَذِّبونَ] “Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha?” [Al-Waqi’a: 82] yaani kushukuru riziki zenu, mithili ya kauli yao “tuliteremshiwa mvua kubwa” na kama kauli yake (swt): [وَاسْأَلِ الْقَرْيَةَ] “Na kiulizeni kijiji [Yusuf: 82] ikimaanisha wanakijiji. Amiri aliwaruzuku wanajeshi wake (irtazaqu irtizaqan), na husema wanajeshi waliruzukiwa (ruziqa)  riziki moja (raqatan waahidan) pekee, na waliruzukiwa riziki mbili (ruziqu razqatani), yaani mara mbili. Ibn Berri...]

2- Katika Kamusi ya Al Muheet inasema: [Rizq (kwa kasra) maana yake ni kile kinachonufaisha kwacho, kama vile mamluki, na mvua, na wingi ni arzaq, na (kwa fatha) chanzo halisi, na pekee yenye herufi -Ha, wingi wake ni razaqat, ni (Mutaharrik), inahusu matamanio ya askari. Mwenyezi Mungu razaqahu maana yake ni Yeye (swt) aliyemruzuku riziki, na fulani akamshukuru, ni riziki (azdiya), na kutokana na hili Aya: [وتَجْعَلونَ رِزْقَكُم أنكم تُكَذِّبونَ] “Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha?” [Al-Waqi’a: 82].

3- Katika Al-Sihah katika lugha: [Al-Rizq: anachofaidika nacho mtu, na wingi ni Al-Arzaq. Na rizq (riziki) ni kutoa, na ndio chanzo cha usemi wenu: “Mwenyezi Mungu amemruzuku”. Al-Razqa ni kwa fat’ha, kwa umoja, wingi ni Al-Razaqat, ambayo ni matarajio ya askari. Irtazaqa askari maana yake ni kwamba askari walichukua riziki zao. Mwenyezi Mungu anasema: [وتَجْعَلونَ رِزْقَكُم أنكم تُكَذِّبونَ] “Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha?” [Al-Waqi’a: 82] yaani shukrani ya riziki yako. Hii ni kama usemi wake, [الْقَرْيَةَ وَاسْأَلِ] “Na kiulizeni kijiji” [Yusuf: 82] ikimaanisha watu wake. Na mvua yaweza kuitwa rizq, na hayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu (swt): [وَمَا أَنزَلَ اللَّهُ مِنَ السَّمَاء مِن رِّزْقٍ فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ] “… na riziki anayo iteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwayo akaifufua ardhi baada ya kufa kwake …” [Al-Jathiya: 5]. Mwenyezi Mungu (swt) asema: [وَفِي السَّمَاء رِزْقُكُمْ وَمَا تُوعَدُونَ]  “Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyo ahidiwa” [Adh-Dhariyat: 22].

Huu ndio ufafanuzi wa kilugha.]

4- Al-Kurassa inasema kuhusu rizq (riziki): [Ama suala la rizq (riziki), Aya nyingi ni za kukatikiwa na hazimuachii nafasi yule mwenye kuiamini Qur’an isipokuwa aamini kuwa riziki iko mikononi mwa Mwenyezi Mungu (swt), humpa amtakaye. Suala la rizq (riziki) sio suala la Al-Qadar. Al-Qadar ni kwamba Mwenyezi Mungu anajua kwamba jambo fulani litatokea kabla ya kutokea kwa jambo hilo, kwa hiyo limeandikwa na limewekwa. Ama rizq (riziki) sio tu kwamba Mwenyezi Mungu anajua kwamba fulani na fulani atakuwa na riziki, kwa hivyo ameiandika na akaiweka, lakini zaidi ya hayo, amekidhia riziki kwani Mwenye Kuruzuku (Ar-Raziq) ni Mwenyezi Mungu na sio mja. Hivi ndivyo aya zinavyo ashiria: [لَا نَسْأَلُكَ رِزْقاً نَّحْنُ نَرْزُقُكَ وَالْعَاقِبَةُ لِلتَّقْوَى] “Sisi hatukuombi wewe riziki, bali Sisi ndio tunakuruzuku. Na mwisho mwema ni kwa mchamngu.” [Ta-Ha: 132][وَكُلُواْ مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّهُ حَلَالاً طَيِّباً وَاتَّقُواْ اللَّهَ الَّذِي أَنتُم بِهِ مُؤْمِنُونَ] “Na kuleni katika alivyo kuruzukuni Mwenyezi Mungu, halali na vizuri. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye mnamuamini.” [Al-Ma’ida: 88][اللَّهُ لَطِيفٌ بِعِبَادِهِ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ وَهُوَ الْقَوِيُّ الْعَزِيزُ]  “Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake. Humruzuku ampendaye. Naye ni Mwenye nguvu, Mtukufu” [Ash-Shura: 19].

5- Ama yale uliyoyataja zaidi ya yale yaliyotolewa, kama vile: kizazi kizuri, afya njema na ustawi, na kila kinachoingia ndani ya mzunguko unaokutawala, yaani, sio kazi yako ya hiari, ni katika Al-Qadhaa, na hii inajumuisha riziki (rizq) na vitendo vyote vinavyotokea kwako au dhidi yako bila ya hiari yako... Imesemwa katika Al-Kurrasa juu ya mada ya Al-Qadhaa Wa Al-Qadar chini ya kichwa: “Rai Sahihi Juu ya Suala la Matendo ya Watu,” yafuatayo:

[Maoni sahihi juu ya suala hili kuhusiana na matendo ya watu ni kwamba mwanadamu anaishi ndani ya mizunguk miwili: mmoja wapo anaudhibiti, ambao ni mzunguko ambao ndani yake yanaangukia matendo yake na ndani yake kuna wigo wa matendo anayoyafanya kwa hiari yake mwenyewe kutokea. Mzunguko mwengine unamtawala yeye na ni mzunguko ambao anaangukia ndani yake. Matendo ndani yake hayana uhusiano wowote naye, iwe yametokana naye au juu ya kwake. Katika mzunguko huu huangukia vitendo ambavyo yeye havidhibiti, ima vianguke kutoka kwake au juu yake. Matendo yanayotokea katika mzunguko unaomtawala hayana uhusiano wowote naye na uwepo wake haumhusu. Yako aina mbili: sehemu inayotakiwa na kanuni ya ulimwengu, na sehemu ambayo matendo ambayo hayako ndani ya uwezo wake na ambayo hawezi kuyaepuka na hayako katika kanuni ya ulimwengu. Ama yale yanayotakiwa na kanuni ya ulimwengu, yeye husibiwa nayo hivyo anaendelea kulingana nayo bila hiari yoyote, kwa sababu anaishi ndani ya ulimwengu na anaendelea na maisha kulingana na mfumo maalum ambao haubaki nyuma. Kwa hivyo, vitendo vinaanguka ndani ya mzunguko huu nje ya udhibiti wake, na hana nguvu wala hana chaguo ndani yake.

Matendo haya yote yanayotendeka ndani ya mzunguko unaomtawala mwanadamu ndiyo yanaitwa Al-Qadhaa, kwa sababu Mwenyezi Mungu pekee ndiye aliyeyakidhia. Hivyo basi, mja wa Mwenyezi Mungu hahesabiwi kwa matendo haya, haijalishi yanabeba mazuri au mabaya kiasi gani, au kupendwa au kuchukiwa na mwanadamu. Yaani, haijalishi yanabeba uzuri au ubaya kiasi gani kulingana na tafsiri ya mwanadamu kwayo, kwa sababu mwanadamu hana athari juu yake na hajui kuyahusu, wala jinsi ya kuyapata, na hana uwezo wa kuyazuia au kuyaleta hata kidogo, na mwanadamu lazima aamini katika qadhaa hii kwamba imetoka kwa Mwenyezi Mungu (swt)].

Nataraji hili limetosheleza na Mwenyezi Mungu Ndiye Mjuzi Zaidi, Mwingi wa Hekima

Ndugu Yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

11 Safar Al-Khair 1444 H

7/9/2022 M

Link ya jibu hili katika ukurasa wa Amiri wa Facebook.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu