Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Silsila ya Maswali Yaliyowasilishwa kwa

Amiri wa Hizb ut Tahrir

Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah Katika Ukurasa Wake wa Facebook

Jibu La Swali:

Uthabiti wa Hadithi, “Mimi Niko Mbali na Wale Walioishi Siku Arubaini baina ya Makafiri”

Kwa: Raja’ Al-Ashhab

(Imetafsiriwa)

Swali:

Assalam Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Ni upi uthabiti wa hadithi ifuatayo: mimi niko mbali na wale wameishi siku arubaini baina ya makafiri? Na nini hukmu ya Kiislamu kwa mtu anayeishi katika nchi ya kikafiri kwa ajili ya kazi, na ipi hukumu ya kisheria kwa mtu anayeishi katika nchi ya kikafiri kwa ajili ya kusoma? Mwenyezi Mungu awalipe kheri.

Jibu:

Hadithi imepokewa na Abu Dawud katika Sunan yake, amesema: Hanad Bin As-sarri alitwambia, Abu Mu’awiyah alitwambia, kutoka kwa Ismail kutoka kwa Qais kutoka kwa Jarir Bin Abdullah alisema kuwa Mtume (saw) alituma msafara wa majeshi Khath’am. Kwa hivyo baadhi ya watu, (waloikuwa wakiishi hapo) wakatafuta usalama kwa kusujudu, lakini walishughulikiwa kwa haraka na kuuwawa. Habari zilimfikia Mtume (saw) na kuamrisha wapewe nusu ya Aql (fidia). Na akasema:

«أَنَا بَرِيءٌ مِنْ كُلِّ مُسْلِمٍ يُقِيمُ بَيْنَ أَظْهُرِ الْمُشْرِكِينَ. قَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ لِمَ؟ قَالَ: لَا تَرَاءَى نَارَاهُمَا»

“Mimi niko mbali na Muislamu yeyote anayeishi baina ya waabudu masanamu (washirikina)” Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Vipi hivyo? Akasema: “hawafai kuziona kambi zao mbili za moto.”

Ili kuifahamu maana iliyokusudiwa, tunataja yafuatayo:

Katika kielelezo cha katiba mjeledi wa pili- katika maelezo ya mada ya 189:

…hukmu za Dar Al-Kufr zinatofautiana kabisa na zile za Dar al-Islam, na hivyo kuna hukmu zake makhsusi:

Ikiwa Muislamu anayeishi katika Dar al-Kufr hawezi kutekeleza Uislamu hapo kwa wazi, basi analazimika kuhamia Dar al-Kufr nyingine ambamo anaweza kufanya hivyo kwa maneno ya Mwenyezi Mungu (swt):

(إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ قَالُوا فِيمَ كُنتُمْ قَالُوا كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِي الأَرْضِ قَالُوا أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَا فَأُوْلَئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ وَسَاءَتْ مَصِيراً)

“Hakika Malaika watawaambia wale ambao wamewafisha nao wamejidhulumu nafsi zao: Mlikuwa vipi? Watasema: Tulikuwa tunaonewa. Watawaambia: Kwani ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa na wasaa wa kuhamia humo? Basi hao makaazi yao ni Jahannamu, nayo ni marejeo mabaya kabisa.”  [An-Nisa: 97]

Hii ni ikiwa hakuna Dar al-Islam kama ilivyo leo. Hata hivyo, hukmu zinazohusiana na kugura kutoka Dar al-Kufr kwenda Dar al-Islam ni kama zifuatavyo:

1- Anayeweza kugura, na hawezi kuutekeleza Uislamu katika nchi yake wala kutekeleza hukmu za Kiislamu kama impasavyo, basi kuguria Dar al-Islam ni faradhi kwake. Katika hali hii hairuhusiwi kwake kuishi katika Dar al-Harb, kwa maana nyengine, Dar al-Kufr. Bali kuguria Dar al-Islam ni faradhi. Dalili ni aya iliyotajwa:

(إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ قَالُوا فِيمَ كُنتُمْ قَالُوا كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِي الأَرْضِ قَالُوا أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَا فَأُوْلَئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ وَسَاءَتْ مَصِيراً)

“Hakika Malaika watawaambia wale ambao wamewafisha nao wamejidhulumu nafsi zao: Mlikuwa vipi? Watasema: Tulikuwa tunaonewa. Watawaambia: Kwani ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa na wasaa wa kuhamia humo? Basi hao makaazi yao ni Jahannamu, nayo ni marejeo mabaya kabisa.” [An-Nisa: 97]. Kama ilivyo mwafaka kuhitimisha hapa. Zaidi, hii imeonyeshwa na kile alichosimulia At-Tirmidhi kutoka kwa Jarir kwamba Mtume (saw) alisema:

«أَنَا بَرِيءٌ مِنْ كُلِّ مُسْلِمٍ يُقِيمُ بَيْنَ أَظْهُرِ الْمُشْرِكِينَ، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَلِمَ؟ قَالَ: لا تَرَايَا نَارَاهُمَ»

“Mimi niko mbali na Muislamu yeyote anayeishi kati ya waabudu masanamu (washirikina)” Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Vipi hivyo? Akasema: “hawafai kuziona kambi zao mbili za moto.” Kumaanisha ikiwa wote wawili watawasha mioto yao huwezi ukaitofautisha, kama fumbo la kutoishi katika makao yao.

Na katika riwaya ya Abu Dawud,

«قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، لِمَ؟ قَالَ: لا تَرَاءَى نَارَاهُمَا»

Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Vipi hivyo? Akasema: “hawafai kuziona kambi zao mbili za moto.”

Vile vile An-Nasa’i amehadithia, na maana ya kuwa moto wao haufai kuonekana kwa wao wawili, kunamaanisha, sio sehemu ambapo moto wao huonekana, na unaweza kuonekana ukiwashwa, ni kinaya cha kutoishi katika ardhi yao.

2- Anayeweza kugura, lakini anaweza kutekeleza dini yake katika nchi yake, na kusimamisha shariah kama impasavyo. Katika hali kama hii kugura ni mandubu na sio faradhi... dalili ikiwa ni kwamba Mtume (saw) alikuwa akihimiza kuguria Makkah kabla ya kufunguliwa huku ikibaki kuwa Dar al-Kufr, na ayah zilizowazi zimeshushwa juu ya hilo kama maneno yake Mwenyezi Mungu (swt):

(إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ أُوْلَئِكَ يَرْجُونَ رَحْمَةَ اللَّهِ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَحِيمٌ)

“Hakika wale walio amini na wale walio hama na wakapigania Njia ya Mwenyezi Mungu, hao ndio wanao taraji rehema za Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu.” [Al-Baqara: 218]

Na akasema (swt):

(ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَهَاجَرُواْ وَجَٰهَدُواْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ بِأَمْوَٰلِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ أَعْظَمُ دَرَجَةً عِندَ ٱللَّهِ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلْفَآئِزُونَ)

“Wale walio amini, na wakahama, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao, hao wana cheo kikubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hao ndio wenye kufuzu.” [At-Tawba: 20] na hizi ni dhahiri katika kuhimiza kugura. Na dalili ya kutokuwa faradhi, hii ni kwa sababu Mtume (saw) aliwaruhusu Waislamu kubaki Makkah. Imepokelewa kwamba wakati Nu’aim Al-Nahhan alitaka kugura, kabila lake Banu Adi walimwambia: baki nasi na ubaki katika dini yako. Alikuwa akiwasaidia mayatima na wajane. Na kwa hivyo alichelewesha kugura kwake kwa muda na kisha akagura baadaye, na Mtume (saw) akamwambia:

«قَوْمُكَ كَانُوا خَيْراً لَكَ مِنْ قَوْمِي لِي، قَوْمِي أَخْرَجُونِي وَأَرَادُوا قَتْلِي، وَقَوْمُكَ حَفِظُوكَ وَمَنَعُوكَ»

“Watu wako walikuwa wazuri kwako kuliko wangu kwangu, watu wangu walinifukuza na kutaka kuniua, wakati ambapo wako walikuangalia na kukulinda” (Imetajwa na Ibn Hajar katika Al-Isabah)

3- Na kwa yule ambaye hana uwezo, basi Mwenyezi Mungu ni mwenye kusamehe, na halazimiki kugura kwa kutoweza kufanya hivyo, ima kwa sababu ya ugonjwa au kulazimishwa kubaki ama udhaifu kama wanawake na watoto na wengineo. Dalili ni maneno yake Mwenyezi Mungu (swt):

(إِلَّا ٱلْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ ٱلرِّجَالِ وَٱلنِّسَآءِ وَٱلْوِلْدَٰنِ لَا يَسْتَطِيعُونَ حِيلَةً وَلَا يَهْتَدُونَ سَبِيلاً)

“Isipokuwa wale waliokuwa wanyonge miongoni mwa wanaume na wanawake na watoto wasio na uweza wa hila ya kuongoza njia ya kuhama.”  [An-Nisa’a: 98]

4- Na kwa yule anaweza kutekeleza dini yake kwa dhahiri katika nchi yake, na kutekeleza hukmu ya shariah zinazomhusu, na wakati huo huo anamiliki uwezo wa kubadilisha Dar al-Kufr na kuwa Dar al-Islam, ni haramu kwake katika hali kama hii kugura Dar al-Kufr kuelekea Dar al-Islam, bila kuzingatia kuwa yeye mwenyewe anamiliki ule uwezo ama kwa kuungana na Waislamu wengine katika nchi yake, au kupitia kupata msaada kutoka kwa Waislamu nje ya nchi yake, au kushirikiana na dola ya Kiislamu, ama kupitia namna yoyote inayoruhusiwa. Ni faradhi juu yake kufanya kazi kubadilisha Dar al-Kufr na kuwa Dar al-Islam, na katika hali kama hii ni haramu kwake kugura toka hapo. Dalili ya haya ni kuwa kufanya kazi ya kuifanya nchi yake kuungana na Dar al-Islam ni faradhi, na ikiwa hataunga mkono ilhali ana uwezo na akawacha kazi ya kuiunganisha na Dar al-Islam na badala yake akagura, basi anakuwa ametenda dhambi sawa sawa na kutotekeleza faradhi nyingine.

Kwa msingi huu, ikiwa kuna Dar al-Islam, kuifanya Dar al-Kufr kuwa makao ya kudumu ni haramu kwa yule mwenye uwezo wa kugura...)

Hatimaye, hadithi iliyotajwa ni katika hali ya kupatikana kwa Dar al-Islam, kwa hivyo ni faradhi kugura toka Dar al-Kufr kwenda Dar al-Islam kulingana na hali zilizopo hapo juu. Lakini kama hakuna Dar al-Islam (Khilafah) kama ilivyo leo, ikiwa mtu anatekeleza dini yake, anaswali na kufunga, nk. basi sio sharti kutoka nchi hiyo. Lakini ikiwa hawezi kutekeleza dini yake, basi ni lazima atoke hiyo Dar al-Kufr na kwenda nyingine ambamo anaweza kutekeleza dini yake.

Ndugu yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

27 Safar Al-Khair 1444 H

23/9/2022 M

Link ya jibu hili katika ukurasa wa Amiri wa Facebook

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu