Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Jibu la Swali:

Ubebaji wa Da'wah ni Faradhi ya lazima ama ni Faradhi ya Kutoshelezana?
Kwa: Abdulrahman Al-May

(Imetafsiriwa)

Swali:

Assalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuhu

Mwenyezi Mungu akulipe kheri kwa niaba yetu na Mwenyezi Mungu aunusuru Uislamu na Waislamu kupitia mikono yako.

Swali langu ni, Je kubeba Daawah ni Faradhi ya lazima ama ni Faradhi ya kutoshelezana na je kubeba Daawah pamoja na kundi yachukua sifa ya kubeba daawah kama mtu binafsi.

Wabaaraka Llahu fiik

Jibu:

Waalaykum salam Warahmatullahi Wabarakaatuh

1- Kazi ya kusimamisha Khilafah ni Faradhi hadi itakaposimamishwa, Na kazi ya kurudisha maisha ya Kiislamu ni Faradhi mpaka yatakaporudishwa. Na kazi ya kurudisha Khilafah haiwezekani ila kwa kikundi "Kutla", Na Muislamu kuwapo katika kikundi kinachofanya kazi ya kurudisha maisha ya Kiislamu ni Faradhi, Lakini ni Faradhi ya kutoshelezana wala haipomoki kwa mwenye kukalifishwa na sheria (mukallaf) mwenye uweza mpaka yatakaporudishwa maisha ya Kiislamu kwa kusimamishwa Khilafah.

2- Ama kwanini ni Faradhi, ni kwa kauli yake Subhanahu:

(وَلۡتَكُن مِّنكُمۡ أُمَّةࣱ یَدۡعُونَ إِلَى ٱلۡخَیۡرِ وَیَأۡمُرُونَ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَیَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡمُنكَرِۚ وَأُو۟لَـٰۤىِٕكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ)

"Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa." [Aali-Imran: 104]

Imekuja katika kitabu cha Utambulisho (Al Taarif) kuhusu tafsiri ya aya hii:

[... Mwenyezi Mungu ameawaamrisha Waislamu katika aya hii liwe miongoni mwao kundi lenye muundo, linalosimama mambo mawili:

La kwanza: Kulingania katika kheri,yaani Daawah kwa Uislamu.

Na pili: Kuamrisha mema, na kukataza muovu.

Na hii amri ya kusimamisha kundi lenye muundo ni mujarad wa ombi (Talab), lakini kumepatikana kiunganishi (Qarina) kinachotambulisha kuwa ni Amri ya lazima (Twalab Jaazim), kwani kazi ambayo imebainishwa na aya ili lisimame nayo hili kundi lenye muundo - kuanzia kulingania Uislamu, kuamrisha mema na kukataza maovu - ni jambo la Faradhi kwa Waislamu wasimame nalo, kama vile ambavyo imethibiti katika aya nyingi na hadith zinazotambulisha hayo, Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«وَالَّذِي نَفْسِي بيَده لَتَأْمُرُنَّ بالْمَعْرُوفِ وَلَتَنْهَوُنَّ عَنِ الْمُنْكَرِ أو لَيُوشِكَنَّ اللَّهُ أَنْ يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عِقَاباً من عِنْده ثُمَّ لَتَدْعُنَّهُ فَلاَ يَسْتَجِيبُ لَكُمْ»

 "Na apa na yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake mtaamrisha mema na mtakataza maovu au hivi karibuni Mwenyezi Mungu atawateremshia adhabu kutoka kwake kisha mtamuomba na hatowakubalia" [Amepokea Ahmad] Kwa hiyo itakuwa hicho kiunganishi (Qarina) cha ombi (Twalab) ni cha lazima (Jazim) na amri kwayo itakuwa ni ya wajibu...] Mwisho.

3- Ama kwa nini ni Faradhi ya kutoshelezana, ni kwa kuwa aya ina maandishi ya neno ((منكم (Miongoni mwenu) basi hapo Faradhi katika hali hiyo ni ya kutoshelezana yaani kundi lenye muundo miongoni mwenu linalolingania kwa Uislamu (Wanalingania katika kheri). Na imekuja kwa maarifa kwa "Alif" na "Lam" kwa hiyo ni kwa ujumla yaani kwa Uislamu wote, na la juu zaidi Dola yake..

4- Ama uhalisia wa Faradhi ya kutoshelezana…

A- Imekuja katika Shakhsiya ya Kiislamu Juzuu ya Tatu mlango wa Wajib:

[Ama Faradhi kwa upande wa kusimama nayo ni vigawanyo viwili: Faradhi ya lazima, na Faradhi ya kutoshelezana, na hakuna tofauti kati yake katika uwajibu; Kwa kuwa uwajibu ni mmoja kwazo, nayo ni kwa kuwa Faradhi ya lazima imetakwa ifanywe na kila mmoja mwenyewe, Na Faradhi ya kutoshelezana imetakwa ifanywe na Waislamu wote, Ikiwa imefikiwa kutoshelezana kwa kusimamisha basi Faradhi imepatikana, Sawa iwe amesimamisha kila mmoja miongoni mwao, au wakasimama nayo baadhi yao, na isipofikiwa kutoshelezana kwa kusimama nayo basi Faradhi inaendelea kusimama kwa kila mmoja miongoni mwao mpaka ifanywe ile faradhi].

B- Na imekuja katika Shakhsiya ya Kiislamu Juzuu ya Pili:

(Kwamba kumsimamisha Khalifah ili asimamishe Hukmu za Uislamu na kubeba Daawah yake ni Faradhi kwa Waislamu na ni jambo lisilo na tashwishi (shubha) katika kuthubutu kwake katika nususi za kisheria sahihi, juu ya kuwa ni Faradhi kwa upande unaolazimishwa na Faradhi ambayo Uislamu umefaradhisha juu ya Waislamu kusimamisha hukmu ya Uislamu na kulinda yai la Waislamu, Isipokua hii Faradhi ni Faradhi ya kutoshelezana, wakisimamisha baadhi Faradhi imepatikana na kupomoka kwa waliobakia, na ikiwa baadhi hawakuweza kuisimamisha na hata kama wamesimama na kazi za kuisimamisha basi itabakia kuwa ni Faradhi kwa Waislamu wote, Na wala haipomoki Faradhi kwa Muislamu madam Waislamu hawana Khalifa.)

C- Na imekuja katika kitabu cha Fikra ya Kiislamu:

(.. Faradhi ni hotuba ya Al shaari' inayoambatana na kutaka kufanywa kitendo matakwa ya lazima, kama kauli yake taa'la

 (أَقِيمُوا الصَّلاةَ)

"Na shikeni Swala" [Al-Baqara: 43].

((ٱنفِرُوا۟ خِفَافࣰا وَثِقَالࣰا وَجَـٰهِدُوا۟ بِأَمۡوَ ٰلِكُمۡ وَأَنفُسِكُمۡ فِی سَبِیلِ ٱللَّهِۚ ))

"Nendeni mtoke, mkiwa wepesi na wazito, na piganeni Jihadi kwa mali yenu na nafsi zenu katika Njia ya Mwenyezi Mungu." [At-Tawba: 41].

Na kama kauli yake (saw):

«إِنَّمَا جُعِلَ الْإِمَامُ لِيُؤْتَمَّ بِهِ»

"Hakika amewekwa imamu ili watu wamfuate - watimize Swala wakiwa nyuma yake"

«مَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّة»

"Atakayekufa na katika shingo yake hana ahadi ya utiifu (Ba'yah) amekufa kifo cha kijahilia".

Hizi nususi zote ni hotuba kutoka kwa Al Shaari' inayoambatana na ombi la lazima la kufanywa kitendo. Na kiunganishi (Qarina), ndio inayolifanya ombi kuwa la lazima ambayo imekuja kuhusiana na ombi hilo (talab) na ikalifanya kuwa la lazima (jazim), hivyo ni wajib kutekelezwa...

Na juu ya hayo ni makosa kusema kuwa Faradhi ya kutoshelezana ni ile ambayo wakisimama nayo baadhi inapomoka kwa waliobakia, Bali Faradhi ya kutoshelezana (Fardhu Kifaya) ni ile ambayo wakiisimamisha baadhi hupomoka kwa waliobakia. Na kupomoka kwake wakati huo ni jambo la kiuhalisia, kwani kitendo kilichotakiwa kufanywa kimesimama, na kikapatikana, Na hakuna nafasi ya kubakia kitendo hicho, Hii ndio Faradhi ya kutoshelezana, nayo ni kama Faradhi ya lazima (Fardhu A'in) sawa kwa sawa...)

Nataraji iwe haya yanatosheleza na Allah anajua zaidi na ni mwenye hikma zaidi.

Ndugu Yenu

Ata Bin Khalil Abu Rashtah

 

22 Muharam Al Haraam 1443 H

30/08/2021M

Link ya jibu hili kutoka ukurasa wa Amiri wa Facebook

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu