Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali
Athari za Virusi vya Korona

(Imetafsiriwa)

Swali:

China ilitangaza kwa mara ya kwanza mnamo 4/1/2020, hususan jijini Wuhan, kuwa watu kadhaa waliambukizwa na maradhi ya virusi vya Korona, yaliopewa lakabu ya COVID-19, kisha yakaenea takriban katika nchi zote za ulimwengu, na nchi nyingi zikalazimisha kufungwa kwa mipaka na marufuku ya kutoka nje usiku, na kisha zikasitisha swala za Ijumaa na jamaa. Uchumi wa kiulimwengu ulipata pigo kwa maradhi haya, na Amerika ikaanza kutupiana tuhma na China. 

Ni nini chanzo cha janga hili? Je, athari yake halisi ni kiasi gani juu ya uchumi wa kiulimwengu? Na ni lipi suluhisho lake sahihi? Je, inajuzu kusitisha swala, za Ijumaa na jamaa kwa sababu ya ugonjwa huu?

Jibu:

Virusi vya Korona vimepewa jina hili kwa Kiingereza (Taji) na linamaanisha taji kwa Kiarabu, kwa sababu umbile lake ni mithili ya taji vinapo tazamwa kupitia darubini ya kielektroniki, na viligunduliwa kwa mara ya kwanza mnamo 1960 kama Coronaviridae. Kutokana na familia ya virusi hivi, vya kwanza vilijitokeza mnamo 2003 eneo la China la Hong Kong, vinavyo itwa SARS na kunakili maambukizi 8,422 ikiwemo vifo 916, na mnamo 2004 na 2005 mivutano ikajitokeza, na hivyo kuanza kujitokeza katika miaka iliyo fuata, hususan mnamo 2012 na 2014, lakini katika baadhi ya nchi ikawa imefungika kwa asilimia chache. Vilijitokeza tena mwanzoni mwa Disemba 2019 jijini Wuhan, China, na kwa sura ya virusi vya SARS 2 kwa asilimia 96. Maambukizi mengi ya mwanzo yalihusishwa na soko la vyakula vya baharini na nyama jijini Wuhan, nchini China. Vikaenea nchini nyingi jirani, na kuonekana kufanana na virusi vya Korona vya popo kwa asilimia 96, ambapo kwa kiasi kikubwa asili yake ni kutoka kwa popo.    

Idadi ya vifo ikaongezeka, vingi yao vikiwa nchini China hadi idadi ya wale walio ambukizwa ikafikia zaidi ya kesi 81,193, kwa zaidi ya vifo 3000, ikifuatiwa na Italy, Iran, Uhispania, Ufaransa na Amerika, na hofu ikatanda kote ulimwenguni kwa sababu ya kuenea kwake kwa kasi hadi idadi ya walio ambukizwa ikifikia takriban kesi 404,000 zilizo thibitishwa na vifo vikikaribia 20,000 mnamo 24/3/2020 (Chanzo: Deutsche Welle, 25/3/2020), na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akasame: "Janga la Covid-19 huenda likauwa mamilioni ya watu endapo kuenea kwake hakutadhibitiwa" (Chanzo: Euro News, 19/3/2020). Hii ndio sababu nchi nyingi zimepiga marufuku shule, vyuo vikuu, na mikusanyiko, na kutoa wito wa marufuku ya kutoka nje usiku, karantini jumla, na kusitisha swali za Ijumaa na za jamaa. Hili limesabanisha mambo kuhitaji ufafanuzi:

Kwanza: Je, maradhi haya yamesababisha na kitendo maalumu, au ni maradhi kama maradhi mengine, Qadhaa kutoka kwa Mwenyezi Mungu iliyo sababishwa na mikono ya watu?

Pili: Je, ulimwengu wa Kirasilimali unaikabili kadhia hii kisawa sawa? Ni ipi tiba ya Kisheria katika hali kama hii?

Tatu: Ni ipi athari ya maradhi haya ya virusi vya Korona juu ya bei za mafuta na uchumi ya kiulimwengu?

Nne: Je, inajuzu kutokana na maradhi haya kuzuia swala za jamaa na za Ijumaa?

Kwanza: Kuzuka kwa maradhi haya na wale walio nyuma yake:

1- Mwanzo wa kuenea virusi vya Korona [COVID-19] ilikuwa ni kutoka China, na tafiti za kisayansi na kimatibabu zinasema kwamba yalitoka kwa wanyama na kuingia kwa wanadamu, kwa sababu nchini China, ni jambo la kawaida kula aina zote za wanyama hata wale wachafu, kwani wao ni makafiri wapagani ambao hawatofautishi kati ya uchafu na uzuri. Kama tulivyo taja awali, ripoti za vyombo vya habari zimetaja kuwa jiji la China la Wuhan eneo la Hubei ni kituo cha biashara ya nyama hizi chafu, na ndio kitovu cha mkurupuko wa maradhi haya.

Hivyo basi, maradhi ya virusi vya Korona yameenea nchini China na kisha kuingia Iran kupitia Wachina wanaofanya kazi huko katika Shirika la Reli la China, ambalo linajenga reli kupitia jiji la Qom. Iran inakadiriwa kama kitovu cha mkurupuko huu eneo la Mashariki ya Kati. Italy pia imefungua kundi la sekta za uwekezaji wa China, kuanzia miundo msingi hadi usafiri. Ripoti zinaashiria kuwa Lombardy na Tuscany ni maeneo mawili ambayo yameshuhudia kiwango kikubwa sana cha uwekezaji wa China. Eneo la Lombardy limeshuhudia maambukizi ya kwanza mnamo 21 ya Februari iliyo pita, na ni mojawapo ya maeneo yaliyo athirika zaidi.

2- Amerika iliishambulia China kwa kushindwa kwake kupambana na janga hili na kulificha tangu kuanza kwake na kushindwa kwake kukabiliana nalo. Hivyo basi, msemaji wa Wizara ya Kigeni ya China Zhao Li Jian alijibu kwa hasira na kuandika katika akaunti yake ya mtandao wa Twitter mnamo 13/3/2020 akisema: "Jeshi la Amerika huenda ndilo lililo leta virusi vya Korona katika jiji la China la Wuhan" …(Chanzo: Al-Sharq Al-Awsat, 13/3/2020). Raisi Trump wa Amerika alirudia shambulizi lake kwa China, akisema: "Ulimwengu unalipia gharama kubwa kwa yale walioyafanya (akikusudia mwendo wa kinyonga wa China katika kutoa habari kuhusu virusi hivi vipya vya Korona)" (Chanzo: Euro News, 19/3/2020) Trump aliviita virusi hivi vya Korona kuwa ni virusi vya China alipo tuma nukuu katika mtandao wa Twitter mnamo 16/3/2020: "Amerika itavisaidia kwa nguvu vile viwanda, kama Mashirika ya ndege na vyenginevyo, ambavyo haswa vimeathirika na Virusi hivi vya China." China ikajibu kupitia msemaji wa Wizara yake ya Kigeni mnamo 17/3/2020 na kusema: "Maoni haya yanaharibu sura ya China. Tumekasirishwa mno nayo na tunayapinga vikali." (Chanzo: Russia Today, 18/3/2020) 

Na pindi China ilipo anza kueneza tuhma kuwa mwanzoni iliitaja Amerika kuwa nyuma ya kuenea kwa virusi hivi, Washington ilimwita balozi wake jijini Beijing mnamo 13/3/2020 na afisa mmoja katika Wizara ya Kigeni ya Amerika alisema: "China inatafuta kuzipotezea kashfa kwa dori yake katika 'kuanzisha janga la kiulimwengu na kutouambia ulimwengu.' Uenezaji wa nadharia za khiyana ni hatari na wa kipuuzi." Afisa huyo alisema, "Tulitaka kuipa ilani serikali hiyo kuwa kamwe hatutaivumilia kwa manufaa ya watu wa China na ulimwengu." Shirika la Xinhua lilithibitisha "kuwa matendo ya Beijing, ikiwemo kulazimisha karantini kali juu ya mamilioni ya watu, yameupa ulimwengu "muda muwafaka" wa kujitayarisha, unaotambuliwa na jamii ya kimataifa." (Chanzo: Russia Today, 15/3/2020).

3- Hivyo basi, vita vya maneno vimezuka katika ya Amerika na China kwa sababu ya mkurupuko wa virusi vya Covid-19 (SARS-CoV2), na nchi zote mbili zinatuhumiana kuwa mhusika wa moja kwa moja katika kueneza maradhi haya, na ingawa nidhamu zote mbili zinazo tabikishwa nchini China na Amerika haziwezi kuepushwa kutokana na uwezekano wa kuwa nyuma ya kuenea kwa virusi hivi, lakini, baada ya utafiti kuna uwezekano kuwa hakuna ushahidi wa nguvu kuwa Amerika wala China ndizo zilizo enea maambukizi au kuunda virusi hivi na kisha kuvieneza katika nchi nyenginezo kwa moja ya sababu mbili dhahiri:

Kwanza ni kuwa nchi zote mbili zimezama jii ndani ya maradhi haya!

Nchini China, ikiongezewa na yale tuliyo tangulia kuyataja nyuma kuhusiana nayo, kiwango cha juu cha maradhi ya virusi vya Korona ni: idadi ya walio ambukizwa imefikia 81272, na idadi ya walio kufa ni 3273 kama ilivyo elezwa katika tangazo la Kamati ya Kitaifa ya Afya nchini China. (Chanzo: Youm7, 23/3/2020), hata kama China ingekuwa iko nyuma ya kuenea kwa ugonjwa huu, ingaa basi ingejilinda yenyewe.    

Ama Amerika, kwa mujibu wa takwimu za wale walio athirika na maradhi ya virusi vya Korona kwa mujibu wa shirika la Afya la CNN, idadi ya vifo kutokana na virusi hivi imeongezeka hadi 704, huku kesi jumla zilizo thibitishwa zikifikia 52976 (Chanzo: (CNN Arabic, 25/3/2020). Amerika inaorodheshwa ya tatu kuhusiana na idadi ya maambukizi ya virusi hivi baada ya China na Italy. Chini ya vipimo vya hivi majuzi, thuluthi moja ya Waamerika wanakabiliwa na amri ya kubaki nyumbani katika majimbo saba, huku majimbo ya Louisiana na Ohio yakitangaza mnamo Jumapili kurefusha marufuku ya kutoka nje usiku, hivyo basi yakiungana na majimbo ya New York, California, Illinois, Connecticut na New Jersey. (Chanzo: Al-Jazeera, 23/3/2020), na vilevile, lau kama Amerika ingekuwa nyuma ya kuenea kwa ugonjwa huu, basi angaa ingelijilinda yenyewe kutokana nao.   

Pili ni kuwa sio sahihi kusema kwamba moja ya nchi hizi ndiyo iliyo viunda, kwa sababu hakuna ushahidi kuwa virusi hivi viliundwa katika maabara. Jarida la Nature Medicine linasema, "Kupitia kulinganisha mpangilio wa data wa genome uliopo na hofu maarufu ya virusi vya Korona, tunaweza kuthibitisha kwa nguvu kuwa virusi vya Korona chimbuko lake ni kupitia michakato ya kimaumbile." Jarida hilo pia linasema, "Mtazamo huu ulitiliwa nguvu na data juu ya uti wa mgongo wa virusi hivi na muundo wake wa viini, na yeyote anaye taka kuunda virusi hivi, hii lingeonekana katika uti wa mgongo wa virusi hivi." (Chanzo: https://www.npr.org)  Hili pia linatabikika kwa nchi nyengine yoyote kama vile Urusi, Ulaya, Iran na biladi nyenginezo za Waislamu, utengezaji huo huathiriwa na moja ya nchi mbili hizi, China na Amerika, kuhusiana na usambazaji wa maradhi haya.  

Hivyo basi, yanayo bakia ni yale anayo yasema Mwenyezi Mungu pekee:

 [ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ لِيُذِيقَهُمْ بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ]

“Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyo yafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyo yatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu.” [Ar-Rum: 41].

Sote tunatambua uovu wa warasilimali na mfano wake ulio fanywa ulimwenguni, kwani wao hawathamini ila maslahi na matarajio yao. Watawala wa Amerika, China, Urusi, Ulaya, nk., ndio sababu ya mateso ulimwenguni na mateso ya watu, na uhalifu wao dhidi ya wanadamu ni mwingi. Wao ndio walio walipua watu wasio na silaha kwa mabomu ya kinuklia, wakaifuja urani, na kuchoma mabomu ya napalm na wakayafanya watumwa kinyama makabila ya Kiafrika na kuyafanya ndio viwanja vyao vya majaribio ya kibaolojia na kemikali. Vita vya mauwaji ya Waafrika wanati ni alama za aibu katika mabapa ya nyuso zao, na uhalifu wa China dhidi ya Waislamu wa Uyghur umefika kote duniani. Uhalifu wa Urusi na Waserbi dhidi ya Waislamu wa Asia ya Kati, Balkan na Ash-Sham ungali unaendelea, na uhalifu wa Uingereza nchini India dhidi ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu bado matokeo yake yangalipo hadi leo. Uhalifu huu unathibitisha kuwa watawala hawa wanao wadhibiti watu ulimwenguni ndio chanzo cha mateso ya wanadamu. Kwa hivyo, ndio, Mwingi wa nguvu (swt) asema:

 [فَأَصَابَهُمْ سَيِّئَاتُ مَا كَسَبُوا وَالَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْ هَؤُلَاءِ سَيُصِيبُهُمْ سَيِّئَاتُ مَا كَسَبُوا وَمَا هُمْ بِمُعْجِزِينَ]

“Basi ukawasibu uovu wa waliyo yachuma. Na wale walio dhulumu miongoni mwa hawa utawasibu uovu wa waliyo yachuma vile vile. Nao si wenye kushinda.” [Az-Zumar: 51].

Pili: Dosari ya suluhisho la kirasilimali na mithili yake kwa kadhia hii, na kwamba tiba sahihi ni ile ya Shariah:

Warasilimali na mithili yao wamekabiliana na kadhia hii katika hatua tatu:

Ya kwanza ni kuificha kadhia hii:

1- (Ripoti ya China inafichua kwamba mamlaka za China zimeificha China na ulimwengu ukweli wa maradhi haya hatari ambayo mamlaka hayo yaligundua kuenea kwake kabla ya katikati mwa Disemba 2019, lakini wakalifanya jambo hili kuwa siri na hawakuyatambua hadi mwishoni mwa mwaka huo baada ya kuongezeka kwa idadi ya kesi. Ripota wa vyombo vya habari vya China na Amerika Shang Wei Wang alisisitiza kuwa mamlaka hayo hayakulifunga soko moja kutokana na kuuza chakula cha baharini jijini Wuhan, mbapo ilisababisha kuenea kwa maradhi haya hadi Januari. Ripoti hiyo imefichua kwamba raia 8 walikamatwa kwa kusambaza habari kuhusu ugonjwa huu mwanzoni mwa janga hili na kuwakadiria kuwa wahalifu kupitia kueneza habari ambazo hazijathibitishwa. Aliendelea kuwa mamlaka za eneo jijini Wuhan zingali zinadai kuwa mambo yako katika hali ya kawaida na kuruhusu matambiko ya baadhi ya tamaduni za eneo hilo kufanyika mnamo Januari 18, ambazo zilihudhuriwa na takriban familia elfu 40." (Chanzo: Ibid 01/02/2020)

2- Vilevile, [maafisa wa China hawakuonya watu juu ya uzito wa janga hili mnamo Disemba hadi Disemba 31, wakati ambapo Beijing ililiarifu Shirika la Afya Duniani. Wakati huo, serikali ya China ilisema, "Maradhi haya yanaweza kukingwa na kudhibitiwa." Mnamo Januari 23, mamlaka hayo yalifunga shughuli za kila siku za jiji la Wuhan, na marufuku kamili ya usafiri ikatolewa. (Chanzo: Masrawy, 23/3/2020)]

 Pili ni karantini na utengaji watu kusio kamilifu

1- [Maafisa kutoka idara ya afya nchini Amerika walithibitisha, mnamo Jumamosi, kesi ya nane ya virusi vipya vya Korona, na Wizara ya Ulinzi ya Amerika ikasema kuwa itatoa makaazi kwa wageni wanao wasili ambao huenda wakahitajika kuwekwa karantini… Jiji la Wuhan na mkoa wa Hubei eneo la kati mwa China, ambako virusi hivi vimejitokeza, yanakabiliwa na karantini halisi (Chanzo: Sky News, 21/2/2020)]

2- Nchini Amerika, Gavana wa Jimbo la New York, Andrew Cuomo, alisema, "Tuko katika karantini," akisisitiza kuwa "Ndio hatua kali zaidi ambayo tunaweza kuchukua." Huku kukiwa na ulazimishaji wa karantini jijini New York, California, New Jersey na Illinois, zaidi ya watu milioni 85 sasa wanalazimika kukaa nyumbani, isipokuwa kwenda madukani na matembezi mafupi (Chanzo: Deutsche Welle, 21/3/2020)]

Tatu ni takriban watu kutengwa kikamilifu majumbani

[Mamilioni ya watu kote ulimwenguni wametengwa majumbani mwao kwa matumaini ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Korona, ambavyo vimewauwa zaidi ya watu elfu kumi na moja. Hatua kali, ambazo hazijawahi kuonekana katika historia ya wanadamu, zinatabikishwa katika viwango tofauti tofauti kulingana na nchi… zaidi ya watu milioni 80 katika zaidi ya nchi 30 wanahitajika kubakia majumbani mwao, ima kutokana na maamuzi ya karantini umma, mapendekezo, marufuku ya kutoka nje usiku, kwa mujibu wa sensa iliyo fanywa na AFP… Nchini Ujerumani, mamlaka zinakadiria kukazanisha hatua za maisha thabiti ya umma na kuwawajibisha wakaazi wengi kujifungia majumbani mwao… Italy, nchi iliyo athirika pakubwa na virusi hivi barani Ulaya ambavyo vimewauwa watu 4,000 na ndio nchi ya kwanza katika bara hilo la wazee kuamuru watu wafanyiwe karantini, inafanya kazi kutilia nguvu hatua zake machoni mwa maradhi haya. Itafunga mabustani na sehemu zote za umma wikendi hii, na vizingiti vyengine vitawekwa ili kuwasukuma wataliani kubakia majumbani mwao, baada ya mamlaka kutangaza kuwa watu 627 wamekufa kutokana na virusi hivi ndani ya masaa 24 nchini humo, ikifikia kileleni tangu kuanza kwa janga hili (chanzo: Deutsche Welle,21/3/2020)]   

• Kupitia kupangilia tiba hizi tatu, imedhihirika kuwa hazitatui tatizo hili, bali zinaongeza kufeli kwa uchumi zaidi, kisha zinayaongeza maradhi haya zaidi na kukosa la kufanya na subra yanayo wakumbwa watu, kama kesi tulizo sikia katika mujtamaa wa Kirasilimali.

Hivyo basi, tiba sahihi ya maradhi haya ni, kama ilivyo elezwa katika sheria ya Mwenyezi Mungu (swt), kuwa dola huyafuatilizia maradhi kuanzia mwanzo wake na kufanya kazi kuyadhibiti hadi sehemu yalipo anzia, na watu wasio wagonjwa katika maeneo mengine huendelea kufanya kazi kuzalisha.

Imesimuliwa na Bukhari katika Sahih yake kutoka kwa Usama Bin Zaid kutoka kwa Mtume (saw) kwamba amesema:

«إِذَا سَمِعْتُمْ بِالطَّاعُونِ بِأَرْضٍ فَلَا تَدْخُلُوهَا وَإِذَا وَقَعَ بِأَرْضٍ وَأَنْتُمْ بِهَا فَلَا تَخْرُجُوا مِنْهَا»

“Pindi mutakapo sikia mkurupuko wa maradhi ya tauni katika ardhi fulani, basi musiingie; na pindi yatakapo tokea katika ardhi muliyoko, basi msitoke humo.” Katika Hadith nyengine katika Bukhari na Muslim, na riwaya yake ni kutoka kwa Muslim kutoka kwa Usama Bin Zaid, kwamba Mtume (saw) amesema:

«الطَّاعُونُ رِجْزٌ أَوْ عَذَابٌ أُرْسِلَ عَلَى بَنِي إِسْرَائِيلَ أَوْ عَلَى مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ فَإِذَا سَمِعْتُمْ بِهِ بِأَرْضٍ فَلَا تَقْدَمُوا عَلَيْهِ وَإِذَا وَقَعَ بِأَرْضٍ وَأَنْتُمْ بِهَا فَلَا تَخْرُجُوا فِرَاراً مِنْهُ»

“Tauni ni janga lililoletwa kwa Bani Israil au kwa wale waliokuwa kabla yenu. Basi mutakapoisikia katika ardhi fulani musiende huko, na itakapo tokea katika ardhi muliomo ndani yake, musikimbie kutoka humo.” Katika riwaya nyengine ya Bukhari kutoka kwa Aisha (ra), mke wa Mtume (saw), kuwa alisema "Nilimuuliza Mtume (saw) kuhusu tauni. Naye akaniambia kuwa:

«أَنَّهُ عَذَابٌ يَبْعَثُهُ اللَّهُ عَلَى مَنْ يَشَاءُ وَأَنَّ اللَّهَ جَعَلَهُ رَحْمَةً لِلْمُؤْمِنِينَ لَيْسَ مِنْ أَحَدٍ يَقَعُ الطَّاعُونُ فَيَمْكُثُ فِي بَلَدِهِ صَابِراً مُحْتَسِباً يَعْلَمُ أَنَّهُ لَا يُصِيبُهُ إِلَّا مَا كَتَبَ اللَّهُ لَهُ إِلَّا كَانَ لَهُ مِثْلُ أَجْرِ شَهِيدٍ»

'Hakika hiyo ni adhabu iliyo tumwa na Mwenyezi Mungu kwa yule amtakaye na hakika Mwenyezi Mungu ameijaaliya iwe ni rehma kwa waumini; hakuna yeyote atakaye patikana na tauni kisha akabakia ndani ya biladi yake huku akisubiri, akitarajia mema, akijua kwamba hakuna litakalomsibu ila lile alilo andikiwa na Mwenyezi Mungu isipokuwa atapata ujira mithili ya shahidi.'"

Hii ndio aina ya karantini katika dola ambayo ilikuwa yaongoza nchi zote, na ndani ya dola hii iliyo staarabika nambari moja, ambayo kiongozi wake ni Nabii wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake (saw), ambaye anapokea wahyi huku akiutabikisha Uislamu ili kuwa kiigizo chema katika utabikishaji. Ibn Hajar ametaja katika Fath Al-Bari kuwa Umar, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, alitoka kwenda Ash-Sham, alipofika Serg, alipewa habari kuwa janga limetokea Ash-Sham, na Abd al-Rahman bin Auf akamwambia kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«إِذَا سَمِعْتُمْ بِهِ بِأَرْضٍ فَلَا تَقْدَمُوا عَلَيْهِ، وَإِذَا وَقَعَ بِأَرْضٍ وَأَنْتُمْ بِهَا فَلَا تَخْرُجُوا فِرَارًا مِنْهُ»

“Pindi mutakapo sikia mkurupuko wa maradhi ya tauni katika ardhi fulani, basi musiingie; na pindi yatakapo tokea katika ardhi muliyoko, basi msitoke humo.” Kisha Omar bin al-Khattab akarudi; ikimaanisha, pindi habari zilipo kuja kwamba tauni imeenea, alirudi na Waislamu.

Kwa hayo, dola ya Uislamu ni lazima iudhibiti ugonjwa pale ulipo na wakaazi wake kubakia ndani yake na wakaazi wengine wasiingie kwao, na kutekeleza jukumu lake la KiShariah, kwani ni dola ya uangalizi na uaminifu. Kama ambavyo inatekeleza hatua hizi wakati wa mikurupuko ya maradhi ya maambukizi, inatoa huduma za afya na matibabu na madawa bila ya malipo kwa raia wote na kujenga Hospitali, maabara na mahitaji msingi mengineyo ya raia wa biladi, kama vile elimu na kudumisha usalama.

Hivyo basi, mapangilio sahihi ni kuyadhibiti maradhi ya maambukizi mahali pake yalipo na kuwaweka wagonjwa katika karantini na kufuatilizia kwa uangalizi na tiba bila ya malipo, huku walio wazima wakiendelea na kazi zao, na maisha ya kijamii na kiuchumi yakiendelea kama yalivyo kuwa kabla ya maradhi hayo ya maambukizi. Haisitishi maisha jumla ya watu, wala hawazuiwi majumbani mwao na kusababisha kulemaa kwa maisha ya kiuchumi au kukaribia kulemaa ikizidisha kudorora kwa janga hili, na kuibuka kwa matatizo mengineyo.

Tatu: Athari ya maradhi haya (virusi vya Korona) juu ya bei za mafuta na hatimaye juu ya uchumi wa kiulimwengu:

Ukuwaji wa uchumi wa kiulimwengu uko kwa mwendo wa taratibu hata katika dhurufu za kawaida bila ya janga hili. Hivyo basi ni vipi hali itakuwa wakati hatua za kiulimwengu zinaelekea katika karantini na utengaji kamili na usio kamili? Hatua hizi zitapunguza zaidi uchumi wa kiulimwengu kama si kupelekea kuporomoka kwake:

Virusi hivi vimelemaza biashara ya kiulimwengu na kusababisha bei za mafuta kushuka chini mno, kwani bei za mafuta zimeanguka chini mno.  Na imesababisha vita vya bei kati ya urusi na Saudi Arabia, kwa sababu Urusi ililazimika kuongeza uzalishaji wake wa mafuta kwani inayategemea pakubwa, na Amerika ikaisukuma Saudi Arabia kuongeza uzalishaji wake ili kukabiliana na Urusi. Mnamo 19/3/2020, Raisi wa Amerika Trump aliitishia Urusi, akisema, "Ataingilia kati vita hivi vya bei baina ya Saudi Arabia na Urusi wakati mwafaka utakapo wadia" (Chanzo: Al-Hurra (American) 19/3/2020)

Saudi Arabia inapigana vita vya Amerika dhidi ya Urusi juu ya mgao wa soko, baada ya makubaliano yake ya awali, yaliyo chukua miaka mitatu, ili kuzuia kuporomoka kwa uzalishaji mwezi huu. Nchi hizi mbili zinajaza mafuta kwa uwezo wao wote katika wakati ambapo mahitaji ya kiulimwengu yanashuka mno kutokana na kuenea kwa virusi vya Korona, hivyo bei zimeshuka viwango vya chini mno wiki hii kwa karibu miaka 20. Bei ya pipa ilianguka hadi $ 28.75 kwa mafuta ya Brent. Na licha ya utambuzi wa Urusi juu ya mafungamano ya Saudi Arabia na Amerika, (msemaji wa Rosneft, Mikhail Leontyev aliliambia Shirika la Habari la Urusi (idadi yote ya mafuta, ambayo yalipunguzwa kutokana na kurefushwa kwa makubaliano ya OPEC + mara kadhaa, yalifidiwa kikamilifu na kwa haraka katika soko la kiulimwengu pamoja na mafuta ya Kiamerika ya Shale) Reuters 8/3/2020] 

Lakini, hawakuchukua hatua yoyote juu ya hilo. Hakika, Saudi Arabia ililizorotesha zaidi  janga hili kwa Urusi kupitia kuamua kutorefusha makubaliano ya awali (kupunguza mapipa 2.1 milioni) na kuamua kuongeza uzalishaji (bei za mafuta zilipoteza hadi thuluthi moja ya thamani yake mnamo Jumatatu katika hasara yake kubwa zaidi ya kila siku tangu Vita vya Ghuba mnamo 1991… hivyo basi, bei ya mafuta ghafi ya Brent ilishuka kwa asilimia 22 kwa $37.05 kwa pipa, baada ya awali kushuka kwa asilimia 31 hadi $31.02, kiwango cha chini zaidi tangu Februari 12, 2016. (Chanzo: Reuters 9/3/2020)) Kisha ikapunguza bei ya mafuta kwa wateja wake barani Asia kwa $6! Leo, Urusi inatafuta njia ya kurudi katika makubaliano ya OPEC Plus na inaonyesha uwezekano wa upunguzaji mpya!  

Hivyo, uchumi wa kiulimwengu umetingishwa vikali na kuenea kwa virusi vya Korona na kisha kushuka kwa bei za mafuta. Endapo hali hii itaendelea, uchumi wa kiulimwengu utakaribia kuporomoka.

Nne: Je, inajuzu kuzuia swala za Ijumaa na jamaa misikitini?

Kusitisha swala za Ijumaa na jamaa kunapotokea kuenea kwa majanga ya maambukizi hakufanywi kwa njia ya kijumla, bali wagonjwa ndio hutengwa na hawaruhusiwi kuingia misikitini kwa swala ya jamaa au Ijumaa, na hatua zote huchukuliwa kuanzia usafi na kuuwa virusi na kuvaa barakoa endapo itahitajika, na kadhalika. Kisha watu walio wazima wataendela kuswali Ijumaa na jamaa pasi na kuwazuia, na ikiwa kuna haja ya timu za madaktari misikitini ili kuangalia ni nani anaye shukiwa kuwa mgonjwa miongoni mwa wenye kuabudu, basi hatua hiyo yaweza kuchukuliwa, lakini bila ya kukatiza swala za Ijumaa na jamaa kwa Waislamu walio wazima. Dalili za swala za jamaa na Ijumaa hazijumuishi ukatizaji wa kudumu, bali hazihitaji idadi kubwa ya ili kutekelezwa kwake kama tutakavyo eleza, na baadhi ya Waislamu wamepewa udhuru wa kutozihudhuria, kwa sababu zinazo wahusu wao tu, kama ifuatavyo:

1-  Ama swala ya jamaa, ni faradhi ya kutoshelezana (kifayah):

Swala ya jamaa ni faradhi ya kutoshelezana ambayo ni lazima ionyeshwe kwa watu, kwa sababu Abu Darda, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, amesimulia kwamba Mtume (saw) amesema:

«مَا مِنْ ثَلَاثَةٍ فِي قَرْيَةٍ وَلَا بَدْوٍ لَا تُقَامُ فِيهِمْ الصَّلَاةُ إِلَّا قَدْ اسْتَحْوَذَ عَلَيْهِمْ الشَّيْطَانُ، عَلَيْكَ بِالْجَمَاعَةِ فَإِنَّمَا يَأْخُذُ الذِّئْبُ مِنَ الْغَنَمِ الْقَاصِيَةَ»

“Ikiwa kuna watu watatu katika kijiji au jangwani na wasisimamishe swala (kwa jamaa), shetani amechukua ubwana juu yao; shikamana na jamaa, kwani mbwa mwitu humnyakua kondoo aliye peke yake.” Imesimuliwa na Abu Dawood kwa Isnad (silsila) iliyo Hasan, na ni kuhusu swala ya jamaa. Ni faradhi ya kutoshelezana; baadhi ya Waislamu walichelewa kuswali jamaa pamoja na Mtume (saw) na Mtume akawaacha baada ya kutishia kuwachoma. Al-Bukhari amesimulia kwamba Abu Huraira amesema kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,   

«وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَقَدْ هَمَمْتُ أَنْ آمُرَ بِحَطَبٍ فَيُحْطَبَ ثُمَّ آمُرَ بِالصَّلَاةِ فَيُؤَذَّنَ لَهَا ثُمَّ آمُرَ رَجُلاً فَيَؤُمَّ النَّاسَ ثُمَّ أُخَالِفَ إِلَى رِجَالٍ فَأُحَرِّقَ عَلَيْهِمْ بُيُوتَهُمْ وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَوْ يَعْلَمُ أَحَدُهُمْ أَنَّهُ يَجِدُ عَرْقاً سَمِيناً أَوْ مِرْمَاتَيْنِ حَسَنَتَيْنِ لَشَهِدَ الْعِشَاءَ»

"Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, nilikaribia kuamrisha kuni zikusanywe na kisha namrishe mtu aadhini kisha ni mwamrishe mtu aswalishe kisha niende kwa nyuma hadi kwa wale wanaume wasio swali kwa jamaa nizichome moto nyumba zao.  Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, lau mmoja wenu angejua kwamba angepata mfupa uliojaa nyama nzuri au vipande viwili vya nyama katikati ya mbavu mbili, angehudhuria swala ya Ishaa.”

Na ikiwa ni fardh ya lazima ('Ain) kwa kila Muislamu, hangewaacha waswali yeye aondoke, kwani hii ilikuwa ni swala ya jamaa kupitia kutajwa swala ya Ishaa. Na jamaa kwa uchache inapaswa angaa watu wawili, imam na maamuma (mmoja anaye ongozwa) kutokana na Hadith ya Malik bin Al-Houwarith, aliye sema:

«أَتَيْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم أَنَا وَصَاحِبٌ لِي فَلَمَّا أَرَدْنَا الْإِقْفَالَ مِنْ عِنْدِهِ قَالَ لَنَا إِذَا حَضَرَتْ الصَّلَاةُ فَأَذِّنَا ثُمَّ أَقِيمَا وَلْيَؤُمَّكُمَا أَكْبَرُكُمَا»

Nilikuja kwa Mtume (saw) mimi na mwenzangu, na tulipokuwa tunataka kuondoka kutoka kwake, alisema: 'Pindi wakati wa swala unapo fika, basi adhinini, kisha mkubwa wenu kwa umri awe ndo imamu wenu.'” Imesimuliwa na Muslim. Na swala ya jamaa haiondolewi isipokuwa kwa udhuru wa kisheria, ambao kwao kuna andiko kama baridi au usiku wenye mvua, kwani Hadith ya Bukhari ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«كَانَ يَأْمُرُ مُؤَذِّناً يُؤَذِّنُ ثُمَّ يَقُولُ عَلَى إِثْرِهِ أَلَا صَلُّوا فِي الرِّحَالِ فِي اللَّيْلَةِ الْبَارِدَةِ أَوْ الْمَطِيرَةِ فِي السَّفَرِ»

“Alikuwa akimwamuru muadhini aadhini kisha aseme mwisho wake, "Swalini majumbani katika usiku wenye baridi au mvua au katika safari."

2-  Ama swala ya Ijumaa, ni swala ya faradhi ya lazima (Fardh Ain), na hairuhusiwi kuondolewa isipokuwa kwa udhuru, na dalili ya hilo ziko nyingi, ikiwemo:

Maneno ya Mwenyezi Mungu (swt)

 [إِذَا نُودِي لِلصَّلاَةِ مِنْ يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَى ذِكْرِ اللَّهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ]

“Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara.” [Al-Jumu’a: 9] Ombi lililo katika ayah hii ni la wajib kutokana na dalili ya Qareenah (kiashiria) cha katazo la kufanya lililo mubah, ishara ya ombi la kukatikiwa (jazim). Na Al-Hakim amesimulia katika Al-Mustadrak juu ya Al-Sahihain kutoka kwa Tariq bin Shihab, kutoka kwa Abu Musa, kutoka kwa Mtume (saw) kwamba yeye amesema: 

«الْجُمُعَةُ حَقٌّ وَاجِبٌ عَلَى كُلِّ مُسْلِمٍ فِي جَمَاعَةٍ إِلَّا أَرْبَعَةٌ: عَبْدٌ مَمْلُوكٌ، أَوِ امْرَأَةٌ، أَوْ صَبِيٌّ، أَوْ مَرِيضٌ»

"Swala ya Ijumaa kwa jamaa ni wajib kwa kila Muislamu, isipokuwa watu wanne: mtumwa anaye milikiwa, au mwanamke, au mtoto, au mgonjwa." Al-Hakim amesema: "Ni Hadith Sahih kwa masharti ya masheikh wawili." Na sio wajib kwa yule aliye hofu, kutokana na yale yaliyo simuliwa na Ibn Abbas, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kwamba Mtume (saw) amesea:

«مَنْ سَمِعَ النِّدَاءَ فَلَمْ يُجِبْهُ فَلَا صَلَاةَ لَهُ إلَّا مِنْ عُذْرٍ، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ وَمَا الْعُذْرُ؟ قَالَ: خَوْفٌ أَوْ مَرَضٌ»

“Yeyote anaye sikia adhana basi na aitikiye kwani hakuna swala isipokuwa kwa mwenye udhuru. Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu na ni upi udhuru? Akasema: hofu na maradhi.” Imepokewa na Al-Bayhaqi katika Al-Sunan Al-Kubra. Hivyo, swala ya Ijumaa ni wajib kwa kila Muislamu, isipokuwa kwa wale ambao kuna andiko (nasi) la kisheria linalo watoa, huku wengine wasiokuwa wao ambao hawana andiko la kuwatoa, Jum'a ni faradhi ya lazima (Fardh Ain) juu yao. Hizi ndizo nyudhuru za kisheria na qiyas haipimwi juu yake. Udhuru wa Kisheria ni ule ulio tajwa katika andiko la kisheria na haujumuishi vitendo vyovyote vya ibada, kwa sababu hazina 'illa (sababu ya kisheria) hivyo qiyas haiwezi kuvuliwa kutokamana nazo. Na inahitajika kwa swala ya Ijumaa kuwa na idadi ya Waislamu, na Maswahaba walikubaliana kuwa ni lazima kuwe na idadi fulani ya kutekeleza swala ya Ijumaa, kwa hivyo ndani yake ni lazima kuwe na idadi fulani (ya watu). Haihitajiki idadi maalumu, kwa hiyo idadi yoyote huitwa jamaa na hukadiriwa kuwa idadi na itaifanya swala ya Ijumaa kuwa halali maadamu idadi hiyo inakadiriwa kuwa ni jamaa, kwa sababu jamaa katika swala ya Ijumaa imefungwa kupitia hadith ya Tariq: 

«الْجُمُعَةُ حَقٌّ وَاجِبٌ عَلَى كُلِّ مُسْلِمٍ فِي جَمَاعَةٍ»

“Swala ya Ijumaa kwa jamaa ni wajib kwa kila Muislamu.” Na kwa sababu idadi yake imefungwa kwa ijmaa ya Maswahaba, na hakuna hadith katika hadhi ya kukadiria inayo ashiria idadi maalumu ya kusimamisha swala ya Ijumaa. Lakini, kwa sababu kufikia jamaa na idadi ni muhimu, na hili laweza kupatikana pekee kupitia watu watatu au zaidi, kwani wawili hawakadiriwi kuwa ni jamaa. Kutokana na haya, watu watatu wale wanao pelekea kusimama kwa swala ya Ijumaa wanahitajika ili swala ya Ijumaa iwe sahihi. Ikiwa watakuwa wachache kuliko hao, itakuwa sio sahihi na haitaitwa swala ya Ijumaa kwa sababu idadi haijafika, na ijmaa ilikuwa ni kwamba ni lazima kuwepo na idadi (watu) kwa swala ya Ijumaa.

Hivyo, katika dola ya Khilafah, swala ya Ijumaa au jamaa haisitishwi. Bali, yule ambaye ana udhuru wa kisheria yeye ndio hatahudhuria na walio bakia watahudhuria. Ama kusema kuwa kuna uwezekano kwa uchache wa shaka kuwa kila mmoja yuko hatarini kuambukizwa na hawezi kuepushwa licha ya hatua au tahadhari zitakazo chukuliwa, ni uwezekano dhaifu, hususan kwa kuwa idadi ya chini ya swala ya jamaa ni watu wawili na swala ya Ijumaa ni watu watu, na hili kupatikana kwake lawezekana kabisa. Endapo tutadhania kuwa uwezekano upo, itashughulikiwa katika eneo lake ipasavyo, hivyo basi, jambo hilo ni lazima lidhibitiwe barabara na kwa ikhlasi. Ikiwa idadi itapatikana kwa uchache wa shaka, basi swala ya Ijumaa na jamaa hazitasitishwa, bali hatua na tahadhari zote zitachukuliwa. Kuchukua tahadhari hakumaanishi kuacha faradhi, bali ni hutekelezwa pamoja na kuchukua tahadhari na hatua ili kuzuia maambukizi.

Hii ndio hukmu iliyo na nguvu zaidi katika jambo hili. Endapo dola itafunga misikiti pasi na kufanya kila juhudi kuthibitisha uchache wa shaka (ghalabat adh-Dhan) kama tulivyo onyesha juu, kisha ikawazuia watu kutokana na kuhudhuria misikitini kwa swala za Ijumaa na jamaa, hapo itakuwa imefanya dhambi kubwa la kukatiza swala za Ijumaa na jamaa.

Kwa kutamatisha, hakika ni uchungu kwamba watawala katika biladi za Waislamu wanafuata hatua za wakoloni makafiri, shubiri kwa shubiri na dhiraa kwa dhiraa, na ikiwa nchi hizo zinatatizika kutafuta tiba ya maradhi fulani, wao huziiga, na endapo watapendekeza suluhisho, hata kama halifai, watawala hawa katika biladi za Waislamu huwashangilia, na hulikadiria hilo kuwa afya na tiba! Ni uchungu kwamba janga hili (virusi vya Korona) vimesababisha nchi na watu wake kusimama na kukwama, hata maisha ya umma ya kila siku yamekaribia kusimama. Hii ndio hali licha ya biladi za Waislamu kuwahi kupitia hali sawa na hii: zilikumbwa na tauni huku zikiwa vitani na Waruni katika Ash-Sham mwaka wa kumi na nane Hijria, na Umma kupata mtihani katikati mwa karne ya sita Hijria kwa janga la "Al-Shaqfa" na sasa inaitwa majipu, ambayo yalienea kuanzia Ash-Sham mpaka Morocco, ambayo yanakadiriwa kuwa ni vidonda vinavyo tokana na ngozi kuathiriwa na staphylococcus bakteria (aina ya bakteria). Waislamu pia walipata mtihani katikati mwa karne ya nane Hijria (749 H) kwa ile inayoitwa Tauni Kubwa jijini Damascus, na katika kesi zote hizi misikiti kamwe haikufungwa wala swala za Ijumaa na jamaa hazikusitishwa. Na watu hawakufungiwa majumbani mwao, bali wagonjwa ndio walio tengwa, na wazima waliendelea na shughuli zao, za jihad na kuimarisha ardhi. Walikwenda misikitini kuswali na kumuomba Mwenyezi Mungu dua ili awalinde kutokana na shari ya maradhi haya, hii ni pamoja na kufuata tiba ya kiafya kwa wagonjwa. Huu ndio ukweli    

 [فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ]

“Na kipo kitu gani baada ya haki, isipokuwa upotovu tu?” [Yunus: 32].

02 Sha’ban 1441 H

26/3/2020 M

#Covid19    #Korona         كورونا#

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 04 Aprili 2020 14:51

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu