بسم الله الرحمن الرحيم
Jua kuhusu mwokozi wa maisha, Hizb ut Tahrir, ulinganizi wao kwa Uislamu, Khilafah na njia yake
(Imetafsiriwa)
Mnamo tarehe 10 Mei 2023, baadhi ya majukwaa ya habari yakiwemo ya maandishi na televisheni yaliripoti kuhusu kuzuiliwa kwa hadi Waislamu 16 katika miji miwili - Bhopal na Hyderabad. Madai hayo ya kashfa yaliishambulia Hizb ut Tahrir kama shirika la 'Kigaidi' linalokusudia kufanya 'Jihad' dhidi ya India. Maregeleo yaliyotolewa kwa vyanzo 'visivyojulikana' kwa mashirika tofauti tofauti ya kijasusi (serikali na muungano) ikiwemo baadhi ya mashirika ya 'kigeni'. Umiliki wa machapisho ya vitabu vya Hizb ut Tahrir kwa wale waliowekwa kizuizini ulifanywa kuwa ndio msingi wa madai hayo. Tangu wakati huo riwaya tofauti za madai hayo zimekuwa zikienea mtandaoni, ikiwa ni pamoja na kuwahusisha Waislamu 16 waliokamatwa na kesi inayoendelea ya wanachama wa Hizb ut Tahrir katika jimbo la Tamil Nadu. Hata majukwaa mashuhuri ya habari kama vile ‘India Today’ au ‘Economic Times of India’ hayakuweza kuzingatia kanuni msingi za maadili, ambazo huchapishwa kwenye tovuti zao wenyewe, na kuvuta kwa urahisi 'simulizi' walizopewa bila kuchunguza ukweli wa kimsingi kuhusu Hizb ut Tahrir! Hivyo huu hapa ni utangulizi mfupi kuhusu Khilafah na Hizb ut Tahrir. Hizb ut Tahrir (Chama cha Ukombozi) ni chama cha kisiasa kinachofanya kazi ya kusimamisha tena Khilafah, mfumo wa utawala wa Kiislamu, katika ulimwengu wa Kiislamu kwa kuiga mfano wa Mtume (saw) kama njia yake.
Kuhusu Khilafah: Mfumo wa utawala wa Khilafah si mfumo usiojulikana ambao ulimwengu au watu wa India, hawaujui. India ilitawaliwa na mfumo huu wa utawala kwa karne nyingi ambao uliingiza India katika zama zake za dhahabu; kwani mfumo wa Kiislamu ulijenga usalama, amani, na ustawi kiasi kwamba India ilijulikana kama kapu la chakula la dunia. Hisa ya uzalishaji ya India ilikuwa zaidi ya 25% ya uzalishaji wa ulimwengu. Khilafah (kwa Kiarabu) ni mfumo wa Utawala wa Kiislamu uliowekwa na Mtume Muhammad (saw) mwenyewe, kama taasisi ya utawala kuendelea baada ya zama za Mtume (saw) mjini Madinah ambako alikuwa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mkuu wa Dola. Katika taasisi hii Khalifa (kwa Kiarabu) ni mtu aliyechaguliwa kuongoza Serikali katika maeneo yote yanayotawaliwa na dola inayojumuisha ya Waislamu na Dhimmi (Wasio Waislamu). Khalifa ana mamlaka ya kuteua wasaidizi wake (katika kutawala), makadhi na pia wakuu wa idara mbalimbali za utawala au idara, ambazo pia anaweza kuziwakilisha. Khalifa pia huchukua chombo cha ushauri kilichochaguliwa kinachojulikana kama Shura (baraza la mashauriano). Huona kuwa ni jukumu jumla kuishi na kutekeleza Shariah katika maisha yao kwa Waislamu limekabidhiwa kwa pamoja kama amana kwa Khalifa na Waislamu katika kile kinachojulikana kama Bayah (ahadi ya utiifu). Khalifa anatarajiwa kutabikisha Shariah (sheria iliyomo ndani ya Quran na Hadith za Mtume). Shariah zinatawala mambo ya kibinafsi na ya umma. Masuala ya umma yanasimamia mambo ya utawala, uchumi, jamii na mahusiano ya kimataifa. Ama kuhusu mambo ya Kibinafsi hakuna kulazimishwa katika dini na ibada na kuhusu mambo ya kibinafsi yanayojumuisha ushiriki wa utawala, uchumi na jamii yanatawaliwa na mipaka ya Shariah.
Historia ya Khilafah: Ni ukweli uliothibitishwa wa historia kwamba taasisi ya Khilafah kama mfumo wa Utawala wa ulimwengu wa Kiislamu ilianza Madina baada ya zama za Mtume (saw) na kuendelea hadi 1924 ilipoondolewa rasmi na Mustafa Kemal Pasha huko Uturuki. Kwa kuzungumza kwa upana, baada ya Makhalifa 5 wa kwanza waliokuwa miongoni mwa maswahaba wa Mtume (saw), taasisi hiyo ilibakia mikononi mwa Bani Umayya (katika Syria ya leo), Abbasiyya (katika Iraq na Iran ya leo), na Uthmaniyya (katika Uturuki ya leo). Muendelezo wa Khilafah chini ya Khalifa mmoja ni kwa maelekezo ya moja kwa moja ya Mtume (saw) katika Hadith (maneno yake); kwa kushindwa kufanya hivyo kulionekana kuwa ni dhambi kwa Waislamu. Kulikuwa na nyakati fupi katika historia ambapo umoja wa Khalifa ulibishaniwa na kusuluhishwa na vizazi vilivyofuata. Wakati wa upanuzi wa ukoloni wa dola za Ulaya kama matokeo ya mapinduzi ya Viwanda katika karne ya 19, baadhi ya maeneo ya Afrika na Asia yalitawaliwa na dola za kikoloni ingawa yalipingwa kote na Khilafah wakati huohuko Uturuki. WW1 vilishuhudia Khilafah ikiungana na Ujerumani mwaka 1914 kupigana dhidi ya Uingereza na Ufaransa na baada ya kushindwa, maeneo ya Khilafah yaligawanywa katika mamlaka mbalimbali ambazo baadaye zilikuja kuwa dola zilizoshindwa katika nchi zinazojulikana sasa kama nchi kubwa za Kiislamu katika Afrika Kaskazini, Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini. Asia hasa kwa kukusudia India, 1918 (baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia) hadi 1924 kilikuwa kipindi cha mashaka makubwa wakati suala la kuendelea kwa Khilafah lilikuwa ni wasiwasi mkubwa kwa Waislamu ulimwenguni kote pamoja na India. Hapo ndipo Harakati maarufu ya Khilafat ilipozinduliwa na viongozi wa Kiislamu kama vile ndugu Ali ambapo hata Wasiokuwa Waislamu waliunga mkono wito huo. Ilikuwa ni wakati huo ambapo Mahatma Gandhi aliandika katika ‘Young India’ mnamo Juni 1921 kuitetea Khilafah dhidi ya vikwazo vyote hata kama hakukuwa na Muslimaan (Waislamu) nchini
India; kwa mtazamo wake kuhusu dori ya Khilafah katika kuondoa dhulma za kikoloni ilikuwa dhahiri sana. Vitabu kuhusu Khilafah na hukmu zake za Shariah vimeandikwa katika kipindi chote cha miaka 1400 kutoka duniani kote kwa lugha nyingi sana. Leo vinapatikana mara kwa mara katika maduka ya vitabu na mtandaoni. Hata hivyo, sheria ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, inayotaka kuendelea kwa mapambano kati ya haki na batili, iliwafanya watu wa batili kukosa dori ya Uislamu chini ya dola yake kwa karne nyingi za historia ya batili ambayo wanawafundisha watoto wao, licha ya kutambuliwa na watu wengi wenye fikra adilifu duniani kwamba wanadamu wote wana deni kwa Uislamu na Waislamu kwa mabadiliko angavu waliyoyaleta katika maisha ya watu.
Kuhusu Hizb-ut-Tahrir: Hizb-ut-Tahrir (Chama cha Ukombozi) ni chama cha kisiasa kilichoanzishwa mwaka wa 1953 na mwanachuoni mkubwa, mwanafikra wa kisiasa na kadhi Sheikh Taqiuddin Nabhani. Hizb inafanya kazi ya kujenga rai jumla katika nchi za Kiislamu kupendelea mfumo wa utawala wa Kiislamu, Khilafah, kwa kuiga mfano wa Mtume (saw). Hii inahusisha kuwasilisha masuluhisho ya Kiislamu ili kushughulikia matatizo ya kisasa, harakati za kisiasa na hatimaye kufanya kazi kwa ajili ya mabadiliko ya kisiasa katika nchi za Kiislamu kwa njia isiyo ya vurugu. Katika nchi zisizo kubwa za Kiislamu, hizb inahimiza jamii ya Waislamu kuwa watetezi wa Uislamu na kulinda kitambulisho chake cha Kiislamu. Uanaharakati ni pamoja na kusoma masuluhisho ya Kiislamu ya matatizo ya kisasa ya kiuchumi, kijamii na kiutawala kwa upande wa Shariah, kutoa wito kwa makundi yote ya watu dhidi ya dhulma za kipote cha watawala, ambao wengi wao wanafurahia ufadhili wa dola za kikoloni kwa nia ya kukandamiza aina yoyote ya mwamko wa kisiasa katika ulimwengu wa Kiislamu. Uanaharakati duniani kote unajifunga na njia za kifikra kama wajibu wa Sharia kuhusiana na njia ya mwamko wa watu. Aina yoyote ya ghasia za watu binafsi au makundi kwa ajili ya mabadiliko ya kisiasa inaonekana kama ukiukaji wa njia ya mwamko wa watu. Hizb imechapisha rasimu ya katiba inayozingatia kanuni za Shariah na kuifanya ipatikane kama pendekezo kwa Khilafah ijayo. Rai na mitazamo ya hizb iko hadharani kikamilifu, mradi tu nchi hazizuii tovuti au wachapishaji, na hakuna rai, maoni au vitendo tofauti vya hizb na yale yaliyosemwa hadharani. Hizb inaweka hili kuwa sharti kwa wafuasi wake, kufanya kazi na hizb. Leo hizb ipo katika zaidi ya nchi 40 zikiwemo baadhi za nje ya ulimwengu wa Kiislamu; na tangu kuanzishwa kwake, haijakengeuka katika njia yake.
Enyi Watu! Hizb ut Tahrir ni mchungaji (kiongozi) asiyelidanganya kundi lake (watu), na lengo lake imedhamiria kuwaokoa wanadamu kutokana na utumwa wa ubepari na kuporomoka kwa maadili yake hadi kwenye uadilifu wa Uislamu ambao kamwe hauwadhulumu, na inafanya kazi hii adhimu bila malipo yoyote kutoka kwa watu, kwa kufuata mfano wa manabii na mitume; wanaoongozwa na bwana wa viumbe, Muhammad, rehma na amani zimshukie. Hizb ut Tahrir haiogopi dhulma ya madhalimu, na haiogopi lawama ya mwenye kulaumu, na inajua kwamba dola za Magharibi na vibaraka wao duniani wanafanya kazi kwa bidii ili kuwazuia watu kutafuta njia badali ya kihadhara ambayo itawaokoa kutoka kwenye makucha ya ulafi, machafuko na ubaguzi wa rangi wa kisekula. Kwa hiyo nguvu hizi ovu zinaficha ukweli wa Uislamu na ukweli wa Hizb ut Tahrir inayobeba Uislamu huu. Bali wanaipotosha sura yake ili watu waliodhulumiwa wasiongozwe kwenye yale ambayo yamo mikononi mwa kundi la kheri kubwa, na yanayobebwa na Hizb ut Tahrir ni njia badali ya kihadhara inayowaokoa watu kutokana na majanga waliyomo ndani yake yaliyosababishwa na tawala za kibinadamu. Kwa hivyo ni wajibu kwa kila mwokozi mwaminifu na asiye na upendeleo, awe Muislamu au asiye Muislamu, mwanamume au mwanamke, msomi au aalim, mwana usalama au mwanasheria, mhadhiri au profesa, kufanya kazi kwa bidii ili kuutabanni Uislamu mtukufu kama mfumo kamili wa maisha. Mwenyezi Mungu (swt) asema katika Kitabu chake,
[هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ]
“Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [9:33].
H. 15 Dhu al-Hijjah 1444
M. : Jumapili, 25 Juni 2023
Hizb-ut-Tahrir
Afisi Kuu ya Habari