Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  17 Muharram 1440 Na: 1440/001
M.  Alhamisi, 27 Septemba 2018

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Raisi wa Mauritania Anajiunga na Vita vya Msalaba Kuupiga Vita Uislamu
(Imetafsiriwa)

Inajulikana kuwa mwanajeshi Mohamed Ould Abdel Aziz, ambaye hakupokea shahada ya “Bakaloriasi” ya shule ya upili lakini “waundaji wake” walimsaidia na kumfanya apate usajili katika chuo cha kijeshi, licha ya yeye kuhitimu na elimu ya wastani shuleni, alimpindua, katika mapinduzi ya kijeshi ya mnamo 6 Agosti 2008, raisi wa kwanza aliye chaguliwa nchini Mauritania (Sidi Mohamed Ould Cheikh Abdallah), baada ya Sidi kutoa uamuzi wa uraisi wa kumuondoa yeye kutoka katika uongozi wa walinzi wa raisi. Na ingawa Ould Cheikh alikuwa amempandisha madaraka ya cheo cha Jenerali, cheo kikubwa zaidi ya vyeo vya jeshi la Mauritania, na kumteua kushikilia wadhifa wa mkuu wa majeshi ya Raisi wa Jamhuri, lakini kiu ya mamlaka na utawala juu ya nchi hiyo na watu wake ilimsukuma kumng’oa Ould Cheikh. 

Leo, huku anapotoa njia ya marekebisho ya katiba ya Mauritania ili kujipatia muhula wa tatu mwakani, anafanya kazi ya kueneza mazingira ya ukandamizaji na kulazimisha utawala chini ya sura ya kuupiga vita Uislamu (walio na misimamo mikali)! Anasema “kuingiza siasa katika dini kumesababisha janga kubwa kuliko lile lililosababishwa na “Israel”, na kwamba biladi za Kiarabu zimeangamizwa na Uislamu wa kisiasa, ambao wanachama wa Baathi, na wafuasi wa Nasser wala wakomunisti hawakuwahi kuyafanya.” Alisema katika mtandao wa Twitter: “Watu waovu zaidi ni wale wanaoutumia Uislamu au dini kama kisingizio cha kufikia utawala na watu wa Mauritania wanajua vyema kuwa Uislamu ni dini na wala sio chama cha kisiasa.”    

Na kama methali inavyo sema: “amenituhumu kuwa na ugonjwa wake na yeye akatoroka,” yeyote anayeruhusu uchafuzi wa matukufu na umwagaji damu kwa kiu ya utawala, ataona kuwa mbinu za karibu zaidi za kupata usaidizi kutoka kwa wapiganaji vita vya msalaba kwa utawala wake wa kiimla ni kuanzisha kampeni dhidi ya Uislamu. Kwa hivyo, pindi Sheikh Mohamed Al-Hassan Al Dedew alipoijibu taarifa yake katika khutba ya Ijumaa iliyopita katika mojawapo ya misikiti ya Nouakchott, Ould Abdel Aziz aliagiza taasisi ya maulama (Markaz Takwin al-Ulama) kufungwa, taasisi ya kisayansi inayo simamiwa na Sheikh Al Dedew, bila ya ilani, chini ya kisingizio kuwa taasisi hiyo inaeneza fikra ya ‘misimamo mikali’!   

Hivyo basi, Ould Abdel Aziz anajiunga waziwazi na vita vya msalaba vinavyopanga njama dhidi ya Uislamu na watu wake, na viongozi madhalimu wanaompinga Allah na Mtume Wake.

Na huku tukimtahadharisha na hasira za Allah Ta’ala, tunatoa wito kwa waumini wenye ikhlasi nchini Mauritania kumuondoa dhalimu huyu. Imeelezwa katika Hadith Sahih kuwa Mtume (saw) amesema:

«إِنَّ النَّاسَ إِذَا رَأَوا الظَّالِمَ فَلَمْ يَأْخُذُوا عَلَى يَدَيْهِ أَوْشَكَ أَنْ يَعُمَّهُمُ اللَّه بِعِقَابٍ مِنْهُ»

“Hakika watu pindi wanapomuona dhalimu na wasiizuie mikono yake (kudhulumu) watakaribia wote kusombwa na adhabu itokayo Kwake.”

Na yeye (saw) amesema:

«كَلَّا، وَاللَّه لَتَأْمُرُنَّ بِالْمَعْرُوفِ، وَلَتَنْهَوُنَّ عَنِ الْمُنْكَرِ، ولتَأْخُذُنَّ عَلَى يَدِ الظَّالِمِ، ولَتَأْطرُنَّهُ عَلَى الْحَقِّ أَطْرًا، ولَتَقْصُرُنَّهُ عَلَى الْحَقِّ قَصْرًا، أَوْ لَيَضْرِبَنَّ اللَّه بقُلُوبِ بَعْضِكُمْ عَلَى بَعْضٍ، ثُمَّ ليَلْعَنكُمْ كَمَا لَعَنَهُمْ»

“La, Wallahi, hamutaacha kuamrishana mema wala hamutaacha kukatazana mabaya, na wala hamutaizuia mikono ya dhalimu (asidhulumu) na kumfanya afuate na ajifunge haki, ila, Allah atazigonganisha nyoyo zenu nyinyi kwa nyinyi kisha atawalaani kama alivyo walaani wao (yaani banu Israel).

Ewe Allah, zama za utawala wa kidhalimu zimerefuka na madikteta wamekuwa wengi, iandalie Dini hii kwa wale watakao nyanyua bendera yake, wasaidie wanaobeba haki na yaangamize majeshi ya upotofu, na rehma na amani ziwe juu ya Mtume wako aliyesema:

«...ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ ثُمَّ سَكَتَ»

“...kisha utakuweko utawala wa kutenzana nguvu na utakuweko vile apendavyo Allah uweko kisha atauondoa apendapo kuuondoa, kisha itakuweko Khilafah katika njia ya Utume kisha akanyamaza.”

Dkt. Osman Bakhach
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahr

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu