Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  12 Rajab 1445 Na: 1445 H / 022
M.  Jumatano, 24 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali ya Rishi Sunak Yaipiga Marufuku Hizb ut Tahrir na Kuisingizia Uongo, Kuibandika Upanga wa "Kuchukia Mayahudi" dhidi ya wale Wanaopinga Mauaji Yanayofanywa na umbile la Kiyahudi huko Gaza

(Imetafsiriwa)

Alhamisi iliyopita, Januari 18, 2024, serikali ya Uingereza ilipigia kura Bungeni ombi la kupiga marufuku Hizb ut Tahrir, ambapo marufuku hiyo iliidhinishwa na wabunge wachache waliokuwepo kwenye kikao hicho. Hii ni baada ya kutekeleza kile kilichoitwa kwa uwongo mjadala wa azimio lililopendekezwa, wakati uhalisia ni mkusanyiko wa hotuba za kisiasa za kuhadaa rai jumla, ili kutoa kibali kwa umbile la Kiyahudi kuendelea na mauaji yake ya kila siku dhidi ya watu wa Palestina, na kubandika upanga wa "chuki dhidi ya Mayahudi" dhidi ya rai jumla ili isionyeshe au kutaka upinzani dhidi ya uvamizi huo.

Kwa hivyo, kwa urahisi kabisa, hizb imepigwa marufuku baada ya kufanya kazi kwa uwazi nchini Uingereza katika miongo minne yote, kwani haikurekodiwa kwamba ilifanya vitendo vyovyote vya kisilaha nchini Uingereza au popote duniani katika kipindi hiki. Na wale waliokuwa na upendeleo dhidi yake, hawakuweza kuthibitisha uwongo wao na kashfa kwamba Hizb ut Tahrir ina uhusiano wowote na ugaidi. Na leo hii hapa, serikali ya Rishi Sunak na kisingizio kibaya, kwamba Hizb ni shirika la kigaidi kwa sababu ya msimamo wake juu ya vita vya Gaza!

Waziri wa Usalama wa Rishi Sunak hakuweza kuwasilisha katika kikao hicho ushahidi halisi wa kuwepo kwa vitendo vya kigaidi, bali alichosema ni kwamba Hizb iliyataka majeshi ya Kiislamu kunyanyuka na kupigana na jeshi la umbile la Kiyahudi. Ama kuhusu “ushahidi” wake uliosalia, si chochote ila ni rekodi ile ile iliyovunjwa ya utetezi wa Wazayuni nchini Uingereza, ambao ulimpatia ripoti zinazozungumzia hofu ya Mayahudi wa Uingereza kuhusiana na maandamano ya Wapalestina! Huu ndio “ushahidi” wake, wakati mazungumzo yake mengine yote yalikuwa hotuba ya kisiasa yenye kashfa za uwongo kuhusu Hizb kuwa na chuki dhidi ya Mayahudi, na simulizi mpya ya matukio kama alivyopewa na umbile la Kiyahudi. Kwao, historia ilianza asubuhi ya tarehe 7 Oktoba 2023, kana kwamba mzozo na uvamizi wa ardhi ya Palestina haukuwepo kabla ya siku hiyo! Pia walirudia madai ya vyombo vya habari vya Kiyahudi kuhusu mauaji ya watoto na ubakaji wa wanawake, wakati ripoti na ushuhuda wa video wa kukiri kwa askari wa uvamizi na walowezi unathibitisha kwamba walipewa amri ya kupiga mabomu makaazi na kila mtu ndani yake. Polisi wa eneo hilo pia hawakuweza kupata waathiriwa wa madai ya ubakaji. Inatosha kukumbuka kashfa ambayo Rais Joe Biden wa Marekani aliingia ndani yake wakati alipowasilisha uwongo wa umbile la Kiyahudi kuhusu kukatwa vichwa kwa watoto, na kisha ikatokea kwamba walimdanganya yeye na ulimwengu.

Ujasiri wa Waziri wa Usalama wa Rishi Sunak katika kupotosha rai jumla unaonyeshwa pale alipopuuza kauli na matendo ya wanasiasa wa umbile la Kiyahudi ambayo yaliripotiwa na vyombo vya habari vya kimataifa na kuchapishwa kwenye magazeti, na ambayo kwa hakika yanahitaji kupigwa marufuku na kuadhibiwa, ikiwa ni pamoja na:

•Kauli ya Benjamin Netanyahu, ambaye alisema: "Tutaigeuza Gaza kuwa kisiwa kisicho na watu."

•Netanyahu pia alinukuu simulizi ya Kiyahudi inayosema: “Sasa nendeni mkaangamize kila walivyo navyo, wala msimuache mwanamume, mwanamke, mtoto, wala watoto wachanga, wala ng’ombe, wala kondoo, wala ngamia, wala punda.

•Kauli ya Waziri wa Turathi Amihai Eliyahu kuangusha bomu la nyuklia mjini Gaza.

•Kauli ya Waziri wa Fedha Bezalel Smotrich, ambaye alitoa wito wa kufukuzwa nchi watu wa Gaza.

•Taarifa ya Waziri wa Usalama wa Kitaifa katika umbile la Kiyahudi, Itamar Ben-Gvir, kwamba kitu pekee kitakachoingia Gaza ni mamia ya tani za vilipuzi ambavyo vitaangushwa na jeshi la anga.

•Kauli ya Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant, ambaye alisema: "Tunapigana na wanyama huko Gaza."

•Taarifa ya msemaji wa jeshi la umbile la Kiyahudi, Daniel Hagari, kwamba lengo ni uharibifu, sio kutengeza.

•Taarifa ya rais wa umbile hilo, Isaac Herzog, kwamba kuzungumza juu ya kutowajibika kwa raia sio sahihi.

•Kauli ya mwanachama wa Knesset Merav Ben Ari kwamba "watoto wa Gaza ndio waliojiletea haya wenyewe."

•Kauli ya balozi wa zamani wa umbile la Kiyahudi katika Umoja wa Mataifa, Dan Gillerman, kwamba watu wa Palestina ni wanyama wa kutisha, wasio na ubinadamu.

•Kauli ya mtafiti na mwanahabari maarufu Mordechai Kadar kwamba kufananishwa kwa Wapalestina na wanyama ni tusi kwa wanyama.

Mbali na matamshi ya waandishi wa habari wa Kizayuni, wataalamu wa vyombo vya habari, na watafiti walioandaliwa na idhaa zenye uhusiano na umbile la Kiyahudi, wanaochochea uharibifu kamili wa Gaza.

Labda nia ya Waziri wa Usalama ya kuwa Waziri Mkuu badala ya Sunak (kama alivyosema mara kwa mara) ilimfanya afumbie macho kauli hizi za wanasiasa wa umbile la Kiyahudi, na badala yake kuwa na shauku ya kutoa marufuku ya Hizb ut Tahrir kama kafara kwa utetezi wa wa Wazayuni, ambao unaonekana kulegea kwenye korido za Ikulu ya Westminster, ili pengine atapata upendeleo wao wakati ujao.

Kwa upande wa wasemaji wengine waliohudhuria kikao hicho, mazungumzo yao hayakuwa zaidi ya kurushiana maneno ya kisiasa wenyewe kwa wenyewe, kwani hawakupinga madai yoyote ya Waziri wa Usalama, bali waliongeza kwenye uongo wake uongo mkubwa zaidi, kama wengine wao kusema kwamba Hizb ut Tahrir inapata msaada kutoka Iran! Na wanaosema kuwa kuua na kuwaangamiza Mayahudi ndio kipaumbele cha hizb! Mbali na kukanusha kwao kuwa hizb inapeperusha sauti ya mateso ya watu wa Palestina kwa Waislamu wa Uingereza! Pia wazungumzaji hawakusita kueleza kutoridhishwa kwao na kuona maandamano ya kuwaunga mkono watu wa Palestina, na hawakusita kuyataja kuwa ni "mabaya" na kuwaelezea wale wanaoyahudhuria kuwa "sehemu mbaya zaidi za jamii." Walikariri propaganda za Wazayuni kwamba ni dhihirisho la chuki dhidi ya Mayahudi, huku uhalisia ni maandamano dhidi ya umbile la Kiyahudi linaoikalia kwa mabavu Palestina, jambo ambalo Hizb ut Tahrir nchini Uingereza ilieleza waziwazi katika taarifa zake zilizotangulia. Lakini upendeleo wa wazungumzaji juu ya umbile la Kiyahudi uko wazi mithili ya mchana ambapo baadhi yao walitangaza kwamba wameshiriki katika maandamano "dhidi ya chuki dhidi ya Mayahudi," ambayo kwa kweli yalikuwa maandamano ya kuegemea na kuunga mkono umbile la Kiyahudi, ambapo bendera za umbile la Kiyahudi zilinyanyuliwa kuanzia mwanzo hadi mwisho, na kauli mbiu, maoni na rai za waliohudhuria kwa kiasi kikubwa zilihusu vita vinavyoendelea Palestina, kama ilivyokuwa wazi katika mahojiano ambayo yaliripotiwa kutoka ndani ya maandamano.

Hii ni sera ya unafiki. Wakati jeshi la umbile la Kiyahudi liliposhambulia kwa mabomu Hospitali ya Baptist mjini Gaza na kuua zaidi ya wahasiriwa 500 waliokuwa kwenye ua wa hospitali hiyo, Rishi Sunak alitilia shaka chanzo cha kombora lililoipiga hospitali hiyo, na hiyo ni kwa sababu umbile la Kiyahudi lilitaka kukwepa jukumu la kulipua mabomu hospitali hiyo. Lakini wakati jeshi la umbile la Kiyahudi lilipozishambulia kwa mabomu hospitali zote za Gaza, shule, sehemu za kuoka mikate, misikiti na makanisa, na kuwalipua wahamiaji walipokuwa wakihamia kati ya miji yake, wakikata maji na umeme kutoka kwao, na hawakusita kuyachukua na kuhalalisha vitendo hivi vyote, Rishi Sunak hakuona tena kwamba ukatili huu ulistahiki umakinifu wake!

Inaonekana kwamba wanasiasa wa serikali ya sasa ya Uingereza ni Wazayuni kabisa. Hata "kamishna wa serikali wa kupambana na misimamo mikali," ambaye Waziri wa Usalama alimshukuru kwa ushauri aliotoa kuhusu kupiga marufuku Hizb, ana upendeleo wa wazi dhidi ya Waislamu. Alichaguliwa kwa uangalifu katika nafasi hii, kwani ana historia ya kufanya kazi katika taasisi zinazochukia sana Waislamu, kama zile zinazohusishwa kwa karibu na Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump. Waislamu hawajasahau marufuku ya kusafiri ambayo Trump aliweka kwa Waislamu wanaokuja Marekani. Mbali na vituo vingine vya utafiti, kamishna wa serikali aliingilia kati kabla ya kuchukua wadhifa wake. Taasisi hizi ambazo zimezama kutoka kichwa hadi miguu katika uchochezi dhidi ya fikra za Uislamu, dhidi ya wahamiaji wa Kiislamu, na dhidi ya wanaharakati wa Kiislamu. Badala yake, chuki ya kamishna huyu wa serikali imefikia hatua kwamba anachukulia neno "Uislamu" sawa na neno "msimamo mkali," kama alivyosema katika moja ya makala yake ya Heritage Foundation. Je vipi jukumu la wadhifa kama huo litapewa mtu mwenye siasa na upendeleo dhidi ya Uislamu na Waislamu namna hii?!

Hii ndio serikali ya Rishi Sunak na wanasiasa wake walioamua kupiga marufuku Hizb ut Tahrir; Wamebeba chuki iliyojificha, na ni ala za ajenda ya Wazayuni, inayowataka Waislamu wa Uingereza kusimama pembeni na kutazama mauaji na njaa ya ndugu zao huko Gaza na wasikasirikie hilo wala kuyataka majeshi ya Kiislamu yahamasike kuwanusuru. Serikali ya Rishi Sunak inawataka Waislamu sio tu kutokuwa na hisia za Uislamu, bali inawataka wasiwe na hisia kabisa ili kusibakie chochote katika ubinadamu wao!

Ni wazi kuwa serikali ya Rishi Sunak inavaa vazi la Chama cha Conservative, wakati uhalisia ni kundi la mrengo wa kulia uliokithiri sawa na wahafidhina ambao walichukua madaraka nchini Marekani mnamo 2001 na kutangaza kampeni maarufu ya "Vita dhidi ya Ugaidi", ambapo mamilioni ya Waislamu waliuawa. Tukumbuke kwamba moja ya vipengee muhimu vya kampeni hiyo ilikuwa ni sera ya kuwatia hofu Waislamu wa nchi za Magharibi kutokana na kupinga Marekani na washirika wake kuua ndugu zao katika nchi za Kiislamu. Huu ndio mtazamo wa serikali ya Rishi Sunak kwa Waislamu nchini Uingereza hivi leo. Inataka waangalie mauaji ya watoto na wanawake wa kaka/dada zao huko Palestina na wakae kimya wasifanye lolote! Inataka kuwafanya Waislamu wa Uingereza kuwa miili inayotembea bila roho, kwa kutumia mantiki ile ile aliyoieleza George Bush Mwana alipouambia ulimwengu, “Wewe ima uko pamoja na sisi au uko pamoja na magaidi,” kwa hiyo kila Muislamu amekuwa gaidi kwao mpaka aseme wanachokisema!

Serikali ya Rishi Sunak imeshindwa kukabiliana na hoja kwa hoja na kutoa ushahidi wa kashfa yake, na kwa hivyo itashindwa mbele ya rai jumla. Imeileta jamii katika hatua ya ukandamizaji wa kifikra, na imezindua taasisi za serikali bila kujua kuamiliana na jamii kwa msingi huu. Vitendo kama hivyo ambavyo vinapingana waziwazi na ufisadi, humomonyoa ari ya jamii na kuua nguvu yao. Kila mtu anaona mauaji yanayofanyika dhidi ya watu wa Palestina, na kila mtu anaona kwamba kile serikali ilichokifanya ni kujaribu kuinyamazisha Hizb isifichue uhalifu huo, na kuwatia hofu Waislamu kutokana na ufikiriaji wa pamoja. Ni kana kwamba serikali ya Sunak inasema kitu kama: "Nyinyi Waislamu mmekatazwa kufikiria juu ya masuluhisho yote"! Kila mtu anajua kwamba vitendo vya Hizb katika miongo minne iliyopita vilikuwa vitendo vya kifikra na kisiasa ambavyo havikuwa na uhusiano wowote na ugaidi, na kwa hivyo marufuku hii itaashiria kuingia kwa awamu ya kushambulia rai jumla kila inapopingana na maoni ya mamlaka.

Ulinganizi wa Hizb ut Tahrir uko wazi na rahisi; Mwamko wa Umma wa Kiislamu, umoja wake, na kurudi kwa Khilafah yake kama ilivyokuwa zama za Maswahaba, kwa kauli na vitendo, na hili limekuwa nguzo madhubuti katika moyo wa kila Muislamu anayeupenda Uislamu na kujali maslahi yake. Kwa hivyo, ulinganizi wa Hizb ut Tahrir utabakia, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, thabiti, angavu na safi, ukielekea kwenye lengo lake, yote hayo kwa ajili ya kumridhisha Mwenyezi Mungu.

Kwa hivyo kuweni na subira, watu wetu wa Uingereza. Kuweni na Mwenyezi Mungu, Utukufu ni wake, Yeye anakutoshelezeni, na Yeye ni Msaidizi wenu, na kumbukeni kwamba vitendo vyenu vinapaswa kuwa vya ikhlasi kwa ajili Yake, Utukufu ni Wake. Mwenyezi Mungu amewaahidi Waislamu tamkini tena, kama vile tulivyobashiriwa na Mtume wake (saw) na Mwenyezi Mungu hatavunja ahadi yake, basi kuweni wa bishara njema. Ametutajia katika Qur’an Tukufu kuhusu mabadiliko ya hali ya nchi na mataifa. Ametukumbusha kuwa suala zima liko chini ya himaya yake, kabla na baada ya kuinuka na kuanguka kwa nchi.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

الم * غُلِبَتِ الرُّومُ * فِي أَدْنَى الأَرْضِ وَهُم مِّن بَعْدِ غَلَبِهِمْ سَيَغْلِبُونَ * فِي بِضْعِ سِنِينَ لِلَّهِ الأَمْرُ مِن قَبْلُ وَمِن بَعْدُ وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ يَنصُرُ مَن يَشَاء وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ * وَعْدَ اللهِ لا يُخْلِفُ اللهُ وَعْدَهُ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لا يَعْلَمُونَ * يَعْلَمُونَ ظَاهِراً مِّنَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ عَنِ الآخِرَةِ هُمْ غَافِلُونَ﴿

“Alif-Lãm-Mĩm * Warumi wameshindwa, Katika nchi iliyo karibu. Nao baada ya kushindwa kwao watashinda * Katika miaka michache. Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake. Na siku hiyo Waumini watafurahi. * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu * Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake. Lakini watu wengi hawajui * Wanajua hali ya dhaahiri ya maisha ya dunia, na wameghafilika na Akhera.” [Ar-Rum 1-7].

Mhandisi Salah Eddine Adada

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu