Mauaji Dhidi ya Watoto wa Yemen yanaendelea, ilhali Wauaji wanacheza dori ya Waweka Amani
- Imepeperushwa katika Kitengo cha Wanawake Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo 26 Aprili, Umoja wa Mataifa ulipeperusha ripoti kwamba idadi ya waliofariki ndani ya Yemen kutokana na mzozo unaoendelea unatarajiwa kupita 230,000 mwishoni mwa 2019. Utafiti kwa kichwa “Tathmini ya Athari ya Vita Juu ya Maendeleo ndani ya Yemen”, pia iliripoti kuwa Wayemen 131,000 watakuwa wamefariki kutokana na athari mbaya za vita baina 2015 na 2019 mfano kutokana na njaa, maradhi na kukosekana kwa kliniki za afya. Kwa mujibu wa UN mwishoni mwa mwaka, mapigano yatakuwa yamechukuwa maisha ya watu 102,000.