Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki

H.  21 Muharram 1444 Na: 1444 / 04
M.  Ijumaa, 19 Agosti 2022

  Rambirambi
Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Uturuki Inatangaza Kifo cha Mmoja wa Dada Zetu Wema, Jayda Arjaan
(Imetafsiriwa)

Dada Jayda Arjaan, aliyejitolea maisha yake kuregesha mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu kama muumini mwema, aliikabidhi roho yake kwa Mwingi wa Rehema jana katika hospitali alikokuwa akipokea matibabu.

(إِنَّا لِلَّهِ وإِنَّا إِلَيْهِ راجِعُونَ)

 Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea. [Baqara: 156]

Jayda Arjaan, mwenye umri wa miaka 50, alikutana na Hizb ut Tahrir mwaka wa 2005 na amefuata da'wah hii pamoja na mumewe sako kwa bako tangu wakati huo. Jayda Arjaan, Mwenyezi Mungu amrehemu, daima amekuwa akimsaidia mumewe mgonjwa na maskini, ambaye alihukumiwa kifungo gerezani kwa ajili ya kazi yake ya ulinganizi wa Kiislamu, daima akiwa akimsaidia licha ya maradhi yake mwenyewe, akivumilia wakati wa matatizo. Tunashuhudia kwamba alikuwa ni mwanamke aliyejitolea muhanga kwa ajili ya kazi ya Dawah na kwa ajili ya familia yake. Tunamuomba Mwenyezi Mungu kwamba magumu aliyopitia Jayda Arjaan baada ya kugundulika kuwa na saratani ya damu yamfute madhambi yake.

Tunamuomba Mola wetu Mlezi ambariki dada yetu mpendwa kwa wingi wa rehema zake, na aijaalie familia yake subira njema na faraja, na pia tunatoa rambirambi zetu kwa jamaa zake, wapenzi na dada zake katika ulinganizi huu.

(إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُمْ بِغَيْرِ حِسَابٍ)

Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu. [Az-Zumar:10]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Uturuki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu