Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  22 Rabi' I 1444 Na: 1444 H / 09
M.  Jumanne, 18 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Enyi Waislamu, Sarakasi ya Uchaguzi sasa ni ya Kipuuzi mithili ya Demokrasia Yenyewe! Uchaguzi utakuwa wa Haki na wa Maana chini ya Mfumo wa Khilafah

(Imetafsiriwa)

Sarakasi ya kisiasa kwa jina la demokrasia kwa mara nyengine tena imeregea Bangladesh kabla ya uchaguzi ujao wa kitaifa mnamo 2023. Joto la kisiasa linazidi kuongezeka mitaani huku chama kikuu cha upinzani, Bangladesh Nationalist Party (BNP), kikiruhusiwa ghafla na Serikali ya Hasina kuhamasisha umati kwa ajili ya kampeni dhidi ya serikali. Wakati watu wanataka kuondoa udhalimu wa Serikali ya Hasina, watu wengi katika mujtamaa wetu huona uchaguzi huru na wa haki kuwa ndio njia ya kubadilisha utawala dhalimu wa Hasina. Pia wana matumaini huku wakiona mikusanyiko mikubwa ya BNP kote nchini inayotaka uchaguzi ujao uwe huru na wa haki. Lakini katikati ya 'ishara hii nzuri' katika vita dhidi ya kile kinachoitwa ufashisti, kusimamishwa kwa ghafla kwa uchaguzi mdogo wa kiti cha ubunge cha Gainbandha-5 na Tume ya Uchaguzi (EC) mnamo Jumatano (12 Oktoba 2022) kwa wizi mkubwa wa kura na vitisho kwa wapiga kura imewafanya kuwa na mashaka kuhusu uchaguzi wa haki chini ya serikali hii.

Vyama vya kisiasa vya upinzani vya kisekula vinatafuta uingiliaji wa pande zote wa nchi za kigeni ili kuishinikiza serikali kufanya uchaguzi huru na wa haki. Hata sasa tunaona jinsi Amerika ya kikoloni inavyotuma ishara kali kwa watendaji wa serikali kabla ya uchaguzi ujao wa kitaifa kwa kuwaadhibu maafisa wa RAB na polisi. Marekani inawataka waziwazi kuchukua hatua kulingana na matakwa yake hata kama itahitaji kwenda kinyume na utawala wa Hasina. Kwa hakika, inajulikana wazi kwamba Marekani inataka kuharakisha maslahi yake ya kisiasa ya kieneo ima kwa kushinikiza utawala wa Hasnia au kwa kumbadilisha, huku Uingereza ikitaka kumuunga mkono kibaraka wake mtiifu zaidi Sheikh Hasina kwa ajili ya kinyang'anyiro chake cha hisa. Kwa hivyo tunaona mvutano wa wazi kati ya polisi na vikaragosi vya Hasina vya EC ambao waliwaita polisi "vibogoyo" na "wasio na makucha" (“DC, SP arguments with EC a misunderstanding: CEC”, The Business Standard, 11 Oktoba, 2022).

Ili kubaki kuwa na maana katika siasa za kawaida za kidemokrasia, hakuna hata kimoja kati ya vyama hivi vya kisiasa na makundi ya kijamii yanayoibua swali muhimu zaidi. Je, chaguzi za kidemokrasia chini ya mfumo wa kilimwengu wa Wakoloni wa Kibepari (yaani ukoloni mamboleo) unaweza kuakisi utashi wa watu na uwakilishi na kuisaidia Bangladesh kujitoa kutokana na mshiko wa Wakoloni - kutoka kwa wale wanaovamia rasilimali zetu za kimkakati na kujaribu kudhibiti jeshi letu kulitumia kama nishati kwa maslahi yao ya kisiasa ya kieneo? Katika miaka hamsini iliyopita, tumepitia chaguzi nyingi sana nchini Bangladesh lakini je, hizo zilisababisha ukombozi kutoka kwa sera za IMF-Benki ya Dunia za kupora mali zetu, kuharibu uchumi na kuwaweka watu katika taabu ya kudumu? Kwa kweli hakuna serikali yoyote kati ya zilizochaguliwa nchini Bangladesh iliweza kuifanya sera yake ya kigeni kuwa huru na maslahi ya kisiasa ya kieneo ya Uingereza au Amerika tangu 1971.

Enyi Watu, huu ndio uhalisia wa uchaguzi wa kidemokrasia chini ya mfumo wa kilimwengu wa Kimagharibi. Kudai 'uchaguzi huru na wa haki chini ya serikali ya muda' au 'hakuna uchaguzi chini ya serikali ya Hasina' hakuna maana bila kuregelea mfumo wa Kirasilimali iliyoshikiliwa chini yake. Uchaguzi wenyewe hauwezi kuchukuliwa kama jambo kubwa kwa sababu sio mbinu madhubuti ya kubadilisha mfumo, unaweza tu kubadilisha sura za watawala ndani ya mfumo huu huu. Hamuwezi kuanguka katika udanganyifu wa 'uchaguzi huru na wa haki' ulioundwa na Magharibi tena na tena. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «لَا يُلْدَغُ الْمُؤْمِنُ مِنْ جُحْرٍ وَاحِدٍ مَرَّتَيْنِ» “Muumini hang’atwi kutoka kwenye tundu moja mara mbili” (Bukhari). Lakini mumeng’atwa na kudanganywa mara nyingi na wanasiasa wetu wa kisekula na wasomi wenye vichwa vya matope wanaotaka kuufanya usekula kuwa kipimo cha maisha yenu. Mabadiliko ya kweli na ukombozi yatakuwa kupitia kuung'oa mfumo huu ili kukomesha utawala wa Magharibi na watawala vibaraka inaowazalisha.

Enyi Waislamu, uchaguzi utakuwa wa haki na wenye maana chini ya mfumo wa kisiasa wa Kiislamu - Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo italeta mabadiliko ya kweli kwa watu. Chini ya Khilafah ubwana ni wa Mwenyezi Mungu (yaani sheria inavuliwa kutoka kwa vyanzo vya Mwenyezi Mungu). Kwa hiyo, hakutakuwa na upeo kwa sheria kupendelea sehemu yoyote iliyokabidhiwa, achilia mbali Makafiri-Wakoloni. Mamlaka yako kwa ajili ya watu ambao wanaweza kuakisi kikweli utashi na uwakilishi wao kwa njia ya uchaguzi na mchakato wa uchaguzi. Tofauti na demokrasia, watu wanashikilia mamlaka ya utawala katika Khilafah na wanawapa mkataba watawala (makhalifa na magavana) kutawala kwa mujibu wa Shariah ya Mwenyezi Mungu. Shariah inataka kwa uwazi mamlaka ya watu kwa ajili ya uteuzi wa mtawala kupitia mchakato wa uchaguzi. Koti ya Mahkamat al-Madhalim (Mahakama ya Matendo Yasiyo ya Haki ya watawala) inaweza kumwondoa mtawala yeyote kwa kukiuka mkataba wao wa kikatiba. Mahakama hii iko huru na chombo cha utendaji na inaweza kusikiliza malalamishi yoyote yanayotolewa na raia bila kujali rangi na dini zao. Raia chini ya Khilafah watafurahia uangalizi na udhibiti wa kweli kwa njia ya Baraza la Jimbo (Majlis ul-Wilayah) katika kila jimbo (Wilayah) ambayo huchaguliwa moja kwa moja. Jumuiko hili kisha huchagua kutoka miongoni mwao bunge la kitaifa linaojulikana kama Baraza la Ummah (Majlis al-Ummah / Baraza la Shura). Watahisabu na kutoa mchango kwa mtawala katika ngazi ya kitaifa na kuteua Magavana (Wali) katika ngazi ya mashinani. Hivi ndivyo uchaguzi na mchakato wa uchaguzi chini ya mfumo wa Khilafah utakavyoleta haki, utulivu na maelewano kwa mujtamaa. Hivyo, uangalizi na udhibiti wa kweli upo ndani ya mfumo wa Khilafah. Kwa hivyo, amkeni kutoka kwenye mtego wa udanganyifu wa ‘uchaguzi huru na wa haki’ chini ya demokrasia na muitishe uchaguzi chini ya mfumo wa Khilafah Rashida.

Mwenyezi Mungu Azza wa Jal asema:

[إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ أَمَرَ أَلَّا تَعْبُدُوا۟ إِلَّا إِيَّاهُ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]

“Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimuabudu yeyote isipo kuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo Dini Iliyo Nyooka. Lakini watu wengi hawajui.” [Surah Yusuf: 40].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu