Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  23 Jumada II 1444 Na: 1444 H / 16
M.  Jumatatu, 16 Januari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Enyi Waislamu! Mahusiano ya Siri na Umbile la Kiyahudi Yanaonyesha kwamba Watawala wa Kisekula na Wanasiasa ndio Adui wa Waislamu na Uislamu

(Imetafsiriwa)

‘The New Age’ na magazeti mengine mashuhuri nchini Bangladesh yalichapisha ripoti mnamo Januari 11, 2023 kwamba serikali ya Bangladesh ilinunua kwa siri programu za ujasusi na zana za uchunguzi wa hali ya juu mwaka jana kutoka kwa kampuni inayoendeshwa na kamanda wa zamani wa kitengo cha teknolojia cha ujasusi cha umbile haramu la Kiyahudi 'Israel'. Serikali ya kinafiki ya Hasina imechagua kuwa mshirika na wale waliolaaniwa na Mola wa ulimwengu (swt). Ni nani miongoni mwa Waislamu anayeweza kushirikiana na maadui wakubwa wa Ummah kwa kuwafanyia ujasusi na kuwatesa isipokuwa wale ambao wao wenyewe wana chuki kubwa kwa Waislamu?! Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَدَاوَةً لِلَّذِينَ آمَنُوا الْيَهُودَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا]

“Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina.” [Surah Al-Maida 5:82]. Mnamo Januari mwaka jana, wasaliti hawa walikuwa wametuma vikosi vyetu vya wanamaji kwenye Mazoezi ya Kimataifa ya Baharini (IMX) ambapo ‘Israel’ pia ilijiunga kwa mara ya kwanza. Mkuu wa makruseda, Amerika, aliandaa mazoezi hayo kama sehemu ya kukuza uhusiano kati ya nchi za Kiislamu na umbile haramu la Kiyahudi. Ni dhahiri kwamba serikali ya kihaini ya Hasina inataka kuhalalisha polepole uhusiano na dola vamizi ya Kiyahudi ili kutumikia siasa za kijiografia za Amerika na kulinda kiti chake cha enzi. Hakika serikali hii ni miongoni mwa ‘Dhalimun’ (madhalimu) ambao wanapata ghadhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kwenda kinyume na amri yake (swt) na kufanya miungano na Mayahudi na Wakristo:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لاَ تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاءَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ مِنْكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللَّهَ لاَ يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.” [Surah Al-Maida: 51].

Isitoshe, sio tu watawala wa sasa pekee wanaoshiriki katika usaliti huo, viongozi wengine wa vyama vya upinzani vya kisekula wanaonekana pia kuwasiliana na viongozi wa ‘Israel’ inayokalia kwa mabavu. Hapo awali mikutano yenye utata ya Katibu Mkuu Mwenza wa BNP Aslam Chowdhury na hivi karibuni ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Muungano wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dhaka (DUCSU) na kiongozi wa Bangladesh Gono Odhikar Parishad Nurul Haque Nur na mwanasiasa mkuu aitwaye Mendi N Safadi wa umbile haramu la Kiyahudi imechochea hisia za watu. Hivyo, wasaliti, watawala wa kisekula na viongozi wa vyama vya upinzani wanawahadaa Waislamu kwa kuonyesha mshikamano bandia na Waislamu wa Palestina, huku wakifanya urafiki wa siri na mvamizi wa Msikiti uliobarikiwa wa Aqswa.

Enyi Waislamu! Kiini cha siasa za kisekula na mfumo wa utawala ni faida na manufaa. Katika ulimwengu wa kisekula, hakuna nafasi kwa imani za kawaida za Kiislamu kama Al-Wala'a wal Bara'a (Kupenda na Kuchukia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu). Utiifu kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake (saw) na waumini, na kujitenga na maadui makafiri wa Waislamu kunabadilishwa na utiifu kamili kwa Wakoloni Makafiri katika mfumo huu wa ulimwengu unaotawala wa Magharibi. Wanasiasa wa kisekula na watawala wa nchi zetu waliozaliwa kutokana na uzao wa mfumo huu wa dunia wamekusudiwa kuhifadhi maslahi ya dola za Kikoloni. Siasa zao hazitokani na uchungaji unaojali wa Ummah na kuunganisha rasilimali na nguvu zake ili kuukomboa kutoka katika minyororo ya Wakoloni Makafiri. Hivyo usaliti, ukandamizaji na dhulma ndio kiini kikuu cha siasa zao. Kwa hiyo, ni lazima muwakatae watawala hawa wa kisekula wasaliti na mfumo wao dhalimu wa utawala, na mujitahidi kuiregesha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume iliyoahidiwa. Khilafah inayokaribia itawahesabu watawala hawa wasaliti katika ulimwengu huu kabla ya Mwenyezi Mungu Al-Qawiy, Al-Adhim kuwahesabu Siku ya Kiyama. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ametwambia kuhusu hatma ya wasaliti kama hao: «لِكُلِّ غَادِرٍ لِوَاءٌ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يُرْفَعُ لَهُ بِقَدْرِ غَدْرِهِ أَلَا وَلَا غَادِرَ أَعْظَمُ غَدْرًا مِنْ أَمِيرِ عَامَّةٍ» “Kila mhaini atakuwa na bendera Siku ya Kiyama ya kuwatambulisha kulingana na wingi wa khiyana yao; hakuna msaliti mkubwa zaidi kuliko kiongozi wa watu (Muslim, Bukhari).

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu