Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  20 Jumada II 1444 Na: 1444 H / 15
M.  Ijumaa, 13 Januari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali Inaiba Akiba ya Watu Iliyo Chumwa kwa Tabu kupitia Kuchapisha Pesa Mpya bila Uegemezi wa Mali Halisi; ni Kipimo cha Madini Mawili (Dhahabu na Fedha) cha Dola ya Khilafah pekee ndicho kinacho weza kumaliza Utawala wa Kifedha wa Urasilimali

(Imetafsiriwa)

Benki ya Bangladesh iliunda pesa mpya kwa zaidi ya Taka bilioni 500 katika kipindi cha Julai-Disemba kwa jina la usaidizi wa bajeti, ambazo ni za juu zaidi katika historia ya hivi majuzi (The Business Standard, Januari 03, 2023), ili kufidia pesa zilizoporwa kutoka kwa mabenki na kipote cha Mabepari. Mikopo ya awali ya benki za biashara tayari imefikia Taka 1253 bilioni. Kwa kuona ufujaji kama huo wa benki, watu wameanza kutoa akiba zao walizozichuma kwa tabu kutoka kwa mabenki katika miezi kadhaa iliyopita ambayo imezidisha mgogoro wa fedha. Msaliti Hasina alitishia mara moja kuiba pesa hizo kutoka kwa watu: "Chukua pesa na uziweke nyumbani, chini ya mto chini ya godoro, au uziweke kwenye kabati. Kisha pesa hizo zinaweza kuibiwa na mwizi" (BBC News, Disemba 4, 2022). Na serikali yake inatarajiwa kuwa haijachukua hatua yoyote dhidi ya waporaji wa benki, badala yake ilichukua hatua haraka ya kuwaadhibu watu kwa kuchapisha pesa mpya zaidi. Hii imepandisha bei kwa kiasi kikubwa na kupunguza uwezo wa watu wa ununuzi, huku watu wakiwa chini ya shinikizo kubwa kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu, umeme na gesi. Hivi ndivyo fedha ya zisizo na thamani ya dhati, zimekuwa chombo chenye nguvu cha mfumo wa Kibepari unaoruhusu serikali kuchapisha pesa bila kuegemeza na mali yoyote halisi kama dhahabu na fedha. Mnamo 1971, serikali ya Nixon ya Amerika ilikata kabisa uhusiano kati ya dhahabu na dolari ya Amerika. Ili kuunda mamlaka ya dolari, Amerika ilizifunga sarafu za dunia kwa dolari kupitia kukomesha mfumo wa Bretton Woods. Tangu wakati huo sarafu hii isiyo na thamani ya dhati (fiat) iko wazi kwa ghiliba za serikali. Serikali za kibepari huchapisha pesa kutoka hewani bila kikomo cha kiasi cha sarafu zinazochapishwa, na kusababisha dhoruba za mfumko wa bei.

Enyi Watu! Upeni mgongo mfumo wa Ubepari ulioundwa na mwanadamu uliojengwa juu ya akili yenye kikomo na matamanio yasiyo na mwisho, na jitahidi kusimamisha tena mfumo wa utawala wa Kiislamu yaani Khilafah Rashida ambao utakukomboeni kutoka katika utumwa wa kiuchumi na Mabepari walafi. Kwani sera ya fedha ya fiat haina kikomo cha kiasi cha pesa cha kuchapishwa, serikali ya Kibepari inaweza kuchapisha pesa wakati wowote inapoona ni muhimu kufidia deni la matumizi yake makubwa na uporaji mkubwa. Uislamu, kwa upande mwingine, umetoa sheria za uhakika na zisizobadilika za uchapishaji wa pesa, yaani sarafu za dhahabu na fedha. Katika sera yake ya fedha ya madini mawili, fedha huchapishwa dhidi ya hifadhi ya dhahabu na fedha. Pesa haziwezi kuchapishwa kwa kuponyeza tu kitufe kwenye mashine ya uchapishaji, lakini kupitia mchakato mgumu wa kuchimba madini na kusafisha dhahabu na fedha. RasulAllah (saw) aliamuru hifadhi ya gramu 4.25 za dhahabu kwa sarafu ya dinari 1 na gramu 2.975 za fedha kwa dirham 1. Kwa kuwa haiwezekani kuongeza ugavi wa madini ya thamani yanayotokea kiasili kama vile dhahabu na fedha, uchapishaji wa pesa kulingana na viwango vya dhahabu na fedha hauwezi kuwa wa kichekesho na wa kiholela. Matokeo yake, hakuna kitu kama mfumko wa bei wa fedha katika mfumo wa fedha wa msingi wa dhahabu na fedha. Khilafah itatoa tu sarafu inayoegemezwa na dhahabu na fedha, na kuondoa mfumko wa bei unaosababishwa na uchapishaji wa sarafu zisizo na thamani ya dhati (fiat) zaidi ya mali na bidhaa. Kwa hivyo, asili ya sarafu ya dhahabu na fedha ya madini mawili huweka nidhamu katika matumizi na ukusanyaji wa mapato, na hivyo kuzuia serikali kutoa kwa uvivu sarafu zaidi ili kufadhili mapungufu. Hakika, ni aibu kubwa kwetu kuteseka kimyakimya katika dhiki ya kiuchumi inayosababishwa na Ubepari mlafi. Ni aibu kusalia kuwa wanyenyekevu na wazembe mbele ya watawala waovu na wasio na watepetevu wakati Dini yetu tukufu inatoa suluhisho la tatizo la mfumko wa bei na umaskini. Ni lazima tuinuke kama mwili mmoja, tukukute vumbi la kujisalimisha na uoga, na tufanye kazi kujiondoa katika mfumo huu fisadi wa kibepari ili kusimamisha tena Khilafah iliyoahidiwa kwa Njia ya Utume. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

(وَمَنۡ اَعۡرَضَ عَنۡ ذِكۡرِىۡ فَاِنَّ لَـهٗ مَعِيۡشَةً ضَنۡكًا)

Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki.” [Surah Taha 20:124]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu