Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  20 Sha'aban 1444 Na: 1444 H / 19
M.  Jumapili, 12 Machi 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Enyi Waislamu! Ni Faradhi kwa Waumini Kuachana na Watawala Wanaounda Mahusiano na Umbile Haramu la Kiyahudi

(Imetafsiriwa)

Serikali ya khiyana ya Hasina inataka kuhalalisha mahusiano na umbile nyakuzi la Kiyahudi wakati linafanya uvamizi wa kikatili katika Kambi ya Wakimbizi ya Jenin katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Mnamo tarehe 05 Machi 2023, Dhaka Tribune ilichapisha maoni ya Joseph Rozen, mkurugenzi wa zamani wa masuala ya Asia na Euro-Asia katika Baraza la Usalama la Kitaifa la umbile la Kiyahudi, iliyochapishwa hapo awali katika The Jerusalem Post (“Mkataba wa Abraham unaleta fursa kwa ushirikiano wa Israel na Bangladesh”). Lengo la ripoti hiyo ya vyombo vya habari liko wazi. Kwa kutumia vyombo vya habari, serikali ya Hasina inataka kuwarubuni Waislamu nchini Bangladesh kukubali mkataba wa kuhalalisha mahusiano unaoongozwa na Marekani, Mkataba wa Abraham, na umbile haramu la Kiyahudi. Ripoti hiyo inasema kwamba Bangladesh sasa inaweza kucheza dori muhimu kama mchezaji wa kiuchumi na kimkakati wa kikanda kwa usaidizi kutoka kwa umbile hili haramu 'Israel'! Baada ya Imarati, Bahrain, Sudan na Morocco, sasa wanaitazama Bangladesh kwa vile wanajua kwamba mtawala mtumwa kama Sheikh Hasina yuko tayari kuvuka mipaka yote ili kuendelea na utawala wake. Ingawa mpango huu wa kuhalalisha mahusiano unasimamiwa na Amerika mkoloni wa sasa, umbile la Kiyahudi kiasili lilikuwa ni mradi wa bwana mkoloni wa Hasina - Uingereza. Kwa hivyo, tayari alianzisha uhusiano wa siri na umbile haramu la Kiyahudi kwa kununua vifaa vya uchunguzi wa watu wengi kutoka kwa mvamizi wa ardhi iliyobarikiwa ya Palestina. (“Bangladesh ilinunua vifaa vingi vya upelelezi kutoka kwa kampuni ya Israeli”, Aljazeera, 2 Feb 2021). Hapo awali, serikali yake tayari ilitupilia mbali kifungu cha maneno ‘isipokuwa Israel’ kutoka katika pasipoti ya Bangladesh kwa kisingizio cha kudumisha kiwango cha kimataifa. Hivi sasa wanatayarisha mazingira kupitia ripoti hizo za vyombo vya habari, wakizijaribu hisia za Waislamu wa Bangladesh kabla ya kutangaza hadharani mpango huo wa ushirikiano haramu na umbile la Kiyahudi.

Enyi Waislamu! Serikali ya Hasina tayari imeusaliti Ummah kwa kudumisha uhusiano wa siri na umbile hili haramu la Kiyahudi. Sasa ni lazima mupinge hatua zake zote zaidi za kujenga uhusiano wowote na umbile hili nyakuzi. Ni lazima muondoe mikono yenu ya utiifu kutoka kwa watawala hao wasaliti ambao wanachukua upande wa maadui wa Mwenyezi Mungu (swt). Musisahau kwamba kuikomboa Palestina kutoka kwa Mayahudi waliolaaniwa ni amana juu ya Ummah. Ni wajibu juu yetu kuitakasa ardhi hii iliyobarikiwa kutokana na najisi ya Mayahudi waporaji, achilia mbali kuhalalisha mahusiano nao. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لاَ تَخُونُوا اللَّهَ وَالرَّسُولَ وَتَخُونُوا أَمَانَاتِكُمْ وَأَنْتُمْ تَعْلَمُونَ]

“Enyi mlio amini! Msimfanyie khiana Mwenyezi Mungu na Mtume, wala msikhini amana zenu, nanyi mnajua.” [Al-Anfal: 27].

Na ikiwa tutaendelea kuwavumilia watawala hawa makhaini ambao wameshirikiana na makafiri wa kikoloni kudumisha mradi wao wa Kiyahudi, hakika tutakuwa tunawasaidia kusaliti amana ya Mwenyezi Mungu Azza Wa Jal na Mtume Wake (saw). Ni lazima muinuke kuwaondoa hawa watawala vibaraka wanaosimama katika njia ya suluhisho pekee la ukombozi wa Palestina na migogoro katika ardhi zote za Kiislamu - Khilafah Rashida iliyoahidiwa kwa njia ya Utume. Waiteni maafisa waaminifu wa Jeshi letu kutoa nusrah (usaidizi wa kimada) kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha tena Khilafah, kuziunganisha tena ardhi zote za Kiislamu, na kuzindua vikosi vyake vya kijeshi vyenye nguvu ili kuikomboa Palestina na maeneo mengine ya ardhi za Waislamu zinazokaliwa kwa mabavu. Vyenginevyo kutotenda na kunyamaza kwetu kutakuwa sababu ya maumivu makali Siku ya Kiyama. Mtume (saw) ametuonya juu ya madhara ya kuwatii watawala waovu kama hawa na wenye kuidhinisha yale ambayo Mwenyezi Mungu anayachukia:

«أَعَاذَكَ اللَّهُ مِنْ إِمَارَةِ السُّفَهَاءِ» قَالَ: وَمَا إِمَارَةُ السُّفَهَاءِ؟ قَالَ: «أُمَرَاءُ يَكُونُونَ بَعْدِي لَا يَقْتَدُونَ بِهَدْيِي وَلَا يَسْتَنُّونَ بِسُنَّتِي فَمَنْ صَدَّقَهُمْ بِكَذِبِهِمْ وَأَعَانَهُمْ عَلَى ظُلْمِهِمْ فَأُولَئِكَ لَيْسُوا مِنِّي وَلَسْتُ مِنْهُمْ وَلَا يَرِدُوا عَلَيَّ حَوْضِي وَمَنْ لَمْ يُصَدِّقْهُمْ بِكَذِبِهِمْ وَلَمْ يُعِنْهُمْ عَلَى ظُلْمِهِمْ فَأُولَئِكَ مِنِّي وَأَنَا مِنْهُمْ وَسَيَرِدُوا عَلَيَّ حَوْضِي»

Mwenyezi Mungu akulindeni dhidi ya viongozi wajinga (wajinga na waovu)”. Akaulizwa “Viongozi ruwaybidah ni kina nani?” Yeye (saw) akasema: “Ni viongozi watakaokuja baada yangu, hawataongoza kwa uongofu wangu, wala hawatachukua Sunnah yangu. Yeyote anayeamini uwongo wao na akawasaidia katika upotovu wao si katika mimi, na mimi si katika wao, na hawatanijia kwenye Hawdh (birika) yangu. Na asiyewaamini uwongo wao na wala hakuwanusuru katika upotovu wao, basi hao ni katika mimi, na mimi ni katika wao, na atanijia kwenye Hawdh (birika) langu.” [Sahih na Ibn Hajar]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu