Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  25 Sha'aban 1444 Na: 1444 H / 20
M.  Ijumaa, 17 Machi 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Milipuko ya Mibaya na Mioto Inayoendelea ni Kufeli kwa Mfumo wa Kisekula kwani daima humlinda Raisi wa Nchi kutokana na Kuwajibika kwa Matukio haya na Watu

(Imetafsiriwa)

Bangladesh inashuhudia mfululizo wa matukio mabaya ya moto moja baada ya jengine katika miaka kadhaa iliyopita ambayo yamesababisha vifo vya watu wengi na kujeruhiwa. Pigo la sasa lilisababisha milipuko mitatu mfululizo ndani ya siku nne pekee. La hivi punde zaidi lilitokea mnamo tarehe 7 Machi katika jengo la kibiashara na makaazi karibu na katikati mwa jiji huko Gulistan na kuchukua maisha ya angalau watu 23 na kujeruhi wengine wengi na bado idadi inaendelea. Watu bado wangali hawajatoka kutokana na kiwewe cha "Mlipuko wa Sitakunda", "Janga la Nimtoli" na "Moto wa Gulshan". Ni dhahiri kwamba miundombinu isiyo na mpangilio na iliyo duni ndiyo sababu kuu za matukio yanayosababisha vifo vingi, majeraha na uharibifu wa mali na utajiri. Na kutokuwepo kwa mipangilio muhimu ya kupambana na hatari za moto daima huongeza uzito wa matukio. Hakuna tukio lililoona maendeleo katika suala la uchunguzi na majaribio, achilia mbali fidia inayostahili kwa waathiriwa.

Kila tukio linapotokea wasomi wa jamii yetu daima huwa wanachunguza kwa undani zaidi sababu, athari na utaalam wa tukio hilo badala ya kuzingatia uwajibikaji wa Raisi wa Serikali ambaye hatimaye ndiye mwenye dhamana ya mambo ya watu, kwa sababu yeye ndiye mwenye mamlaka ambaye anawapa mawaziri na mawaziri hatimaye kuwapangia viongozi wa serikali kusimamia mambo ya wananchi. Ni jambo la kusikitisha sana kwamba wanasiasa na wasomi siku zote wanamwondolea Hasina, Mkuu wa Serikali katika majukumu yake kwa ajali. Badala ya kumkamata kwa nguvu ili kumpeleka mahakamani, wanamtakasa kama ‘Mheshimiwa Waziri Mkuu’. Pia yeye kwa ujanja huepuka kuwajibika kupitia kukimbiza vivuli vya 'hujuma ya kigaidi'. Kando na kutojali kwa serikali juu ya mambo ya watu, wahusika wa matukio hayo pia wanapewa kinga endapo wana uhusiano na serikali.

Kwa kweli, katika mfumo wa kisekula watawala wana ubwana na sheria pamoja na mamlaka zote ziko mikononi mwa watu wale wale. Kwa hivyo, watawala daima wanajiweka juu ya uwajibikaji kupitia kutunga sheria. Zaidi ya hayo, kwa vile uwajibikaji haujafungwa na umefafanuliwa vyema katika mfumo wa kisekula, wasomi wanaweza pia kuendesha mijadala yao ili kuiokoa serikali dhidi ya kuhesabiwa kupitia kuficha kushindwa na kufeli kwake. Mwenyezi Mungu (swt) asema

[لَمْ يَكَدْ يَرَاهَا وَمَنْ لَمْ يَجْعَلِ اللَّهُ لَهُ نُورًا فَمَا لَهُ مِنْ نُورٍ]

“Na ambaye Mwenyezi Mungu hakumjaalia kuwa na nuru hawi na nuru.” [An-Nur: 40]

Enyi Watu! Tofauti na mfumo wa kisekula, hakuna nafasi ya kinga ya watawala katika Khilafah. Ikitokea msiba wowote, Khalifa kimsingi ndiye mwenye kuwajibika kwa hilo. Ummah utamhisabu kuwa ni hatua zipi alizochukua kwa ajili ya kuzuia na kwa haraka jinsi gani alihakikisha fidia inayostahili kwa wahasiriwa. Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Umar: Mtume (saw) amesema, «كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ الْإِمَامُ رَاعٍ وَمَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ»Nyote ni wachungaji na nyote mtaulizwa kuhusu mulivyovichunga. Kiongozi wa watu ni mchungaji na na ni mwenye kuulizwa kuhusu raia wake” [Bukhari, Muslim]. Kwa hivyo, Khalifah ndiye atakayefanya uchambuzi wote wa sababu-na-athari na kushughulikia utafiti wa kiufundi kuhusiana na tukio lolote la mkasa. Hataiacha jamii ishughulike na mijadala ya kiusomi na kufurahia kinga kuhusiana na majukumu yake. Kwa sababu katika Uislamu, hakuna nafasi ya kuwawajibisha wengine badala ya Khalifah. Dori ya nyadhifa za utawala katika Uislamu kwa hakika inaitisha viwango vya juu kabisa vya nguvu. Imepokewa kutoka kwa Muslim kutoka kwa Abu Dharr ambaye amesema: “Nilisema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), je hutaniteua mimi kuwa gavana/mtawala? فَضَرَبَ بِيَدِهِ عَلَى مَنْكِبِي ثُمَّ قَالَ: «يَا أَبَا ذَرٍّ إِنَّكَ ضَعِيفٌ وَإِنَّهَا أَمَانَةُ وَإِنَّهَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ خِزْيٌ وَنَدَامَةٌ إِلَّا مَنْ أَخَذَهَا بِحَقِّهَا وَأَدَّى الَّذِي عَلَيْهِ فِيهَا»” Alinipiga mabega yangu kwa mkono wake kisha akasema: “Ewe Abu Dhar, wewe ni dhaifu na utawala ni amana. Na utawala Siku ya Kiyama itakuwa ni fedheha

na majuto isipokuwa kwa yule aliyeuchukua kwa haki yake na kutekeleza wajibu wake ndani yake.” Kwa hivyo, kutokuwa na uwezo kwa mtawala kutekeleza wajibu wake kutamfanya aondolewe katika nafasi yake moja kwa moja na “Mahakama ya Madhalim” (Mahakama ya Matendo ya Udhalimu). Mwisho, tunatoa wito kwa wanasiasa na wasomi wanyoofu hasa na watu wote kwa jumla kuung'oa mfumo wa kisekula kutoka kwa jamii na kurudisha "Khilafah Rashida" kwa njia ya Utume chini ya uongozi wa Hizb ut Tahrir. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا۟ مَا بِأَنفُسِهِمْ]

“Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo nafsini mwao.” [Surah Ar-R’ad:11].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu