Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  27 Shawwal 1444 Na: 1444 H / 24
M.  Jumatano, 17 Mei 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kwa Kutangaza Kutokuwa na Matamanio kwa Jeshi Letu, Utawala Saliti wa Hasina Unataka kutumiwa kama 'Kikaragosi' cha Marekani

(Imetafsiriwa)

Bangladesh imeandaa 'Kongamano la 6 la Bahari ya Hindi 2023' (IOC) la siku mbili mnamo Mei 12. Toleo la sita la kongamano hilo liliandaliwa na Wakfu wa India kwa ushirikiano na wizara ya mambo ya nje ya Bangladesh. IOC ina umuhimu wa kimkakati kwa India kwa kuwa imeunganishwa kwa karibu na sera ya baharini ya India katika eneo la Bahari Hindi - Usalama na Ukuaji kwa Wote katika Kanda (SAGAR). Lakini tunapaswa kukumbuka kwamba IOC hii pamoja na sera ya baharini ya India zinafungamana na sera "kuu" ya Mkakati wa Marekani wa Indo Pasifiki (IPS). Na kongamano hili lilifanyika wakati ambapo serikali ya Hasina hivi karibuni imetangaza rasmi 'Mtazamo wake wa Indo-Pasifiki'. Naibu Waziri Msaidizi wa Marekani Afrin Akter pia aliwasili nchini Bangladesh hasa kuhudhuria IOC ambayo ilihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Wendy Sherman (Chanzo: Dhaka Tribune, 13 Mei 2023). Zaidi ya hayo, Mkuu wa Jeshi la Bangladesh Jenerali SM Shafiuddin Ahmed aliondoka kuelekea Marekani kwa ziara rasmi mnamo Jumapili kwa mwaliko wa Jeshi la Marekani kuhudhuria kongamano la kijeshi linalojulikana kama Land Forces Pacific Conference (LANPAC), jukwaa linaloungwa mkono na Jeshi la Marekani kuimarisha sera ya Marekani ya Indo-Pasifiki. Kibaraka khaini wa Uingereza Hasina anawahadaa watu kwa kutoa kauli ya kijasiri dhidi ya Marekani, huku nyuma ya mlango akijadiliana na Marekani ili kusalia madarakani.

Enyi Watu, Bangladesh inazidi kuzidiwa nguvu na utawala wa Marekani, na utawala wa kisaliti wa Hasina unajaribu kulinda kiti chake cha enzi kwa kusalimisha mamlaka yetu kwa mkoloni Marekani. Tunapoburutwa kwa khiyana katika ujanja wa kisiasa wa kijiografia wa Marekani, waziri wa mambo ya nje wa Bangladesh Md Shahriar Alam alisema mbele ya IOC kwamba Bangladesh haina malengo ya kijeshi na inatamani kuibuka kama dola ya kikanda. Ni aibu iliyoje kwamba kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje inakwenda kinyume na sera ya kijeshi ya jeshi letu la Kiislamu shupavu! Serikali yake haitaki tuwe na nia ya kijeshi, bali inataka kulibakisha jeshi letu litiifu mbele ya maadui Washirikina na Makafiri wa Kikoloni. Wanataka kutumia jeshi letu shupavu kama ala katika vita vya Marekani ili kukabiliana na China katika eneo hili. Usalama, amani na ubwana wetu hauwezi kulindwa na watawala hawa vibaraka wa kisekula wa magharibi.

Enyi Waislamu, watu wa bara hili dogo la India bila kujali dini na rangi wamekuwa chini ya utawala uliobarikiwa wa Khilafah kwa karne nyingi. Khalifa wa Umawiyya Alwaleed bin Abd al-Malik alilifungua eneo hili kupitia jeshi lisiloshindika kutoka Iraq chini ya uongozi wa jenerali shupavu wa kijeshi Muhammad bin Qasim mwaka 711. Hivyo basi, Waislamu wa bara hili dogo wamefungwa bila kutenganishwa na Uislamu, damu na pamoja na historia ya izza na ushindi. Lakini kwa kuvunjwa kwa Khilafah mwaka 1924 na khiyana ya watawala vibaraka wa kisekula, Wakoloni wa Makafiri wa Kimagharibi wameuvunja umoja wa Ummah katika bara hili dogo kupitia siasa za utaifa zenye mgawanyiko wa kimadhehebu. Watawala hawa wa kisekula wa kitaifa wapo ili kudumisha hali hii halisi iliyopo na kutumikia maslahi ya Makafiri wa Magharibi na Washirikina kwa gharama ya watu. Hatuwezi kuikata mikia ya wakoloni katika eneo hili isipokuwa tuwaondoe watawala hawa watumwa na utawala wao wa kisekula. Hizb ut Tahrir inafanya kazi bila kuchoka katika Bara Dogo la India ili kurudisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume iliyoahidiwa ili kuwatoa watu katika giza la dhulma na kuwaingiza kwenye nuru ya Uislamu na uadilifu wake. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «السُّلْطَانُ ظِلُّ اللَّهِ فِي الْأَرْضِ» “Sultan ni kivuli cha Mwenyezi Mungu katika ardhi.” [imeorodheshwa kama hadith Sahih katika Al-Jaam’a as-Saghir]. Khilafah iliyokaribia itang'oa mipaka bandia ya nchi za Kiislamu za eneo hili na kuziweka chini ya bendera ya Tawhid kwa mara nyingine tena. Itaziunganisha tena Pakistan na Bangladesh, na kuikomboa India kwa mujibu wa bishara njema ya Mtume (saw) ili kukomesha utawala wa Makafiri na Washirikina katika eneo hili. Sera ya kijeshi ya Khilafah itaegemezwa imara katika sera yake ya kigeni ya kuitawala dunia nzima. Hakuna nafasi ya kuanzisha kile kinachoitwa usawazishaji wa mamlaka katika sera yake ya nje. Dola ya Khilafah itaimarisha taasisi zake za kijeshi kwa namna ambayo itatia hofu katika nyoyo za wakoloni makafiri. Mwenyezi Mungu (swt) asema ndani ya Quran,

[وَأَعِدُّوا لَهُمْ مَا اسْتَطَعْتُمْ مِنْ قُوَّةٍ وَمِنْ رِبَاطِ الْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِ عَدُوَّ اللَّهِ وَعَدُوَّكُمْ]

“Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu...” [Al-Anfal :60]. Kwa hivyo, kimaumbile itaondoa kila aina ya uingiliaji wa nchi za kikoloni na taasisi zao katika eneo hili. Hivyo basi sera ya mambo ya nje ya Khilafah kuhusiana na mahusiano ya kimataifa itakuwa ni sera iliyojengwa juu ya msingi wa vita. Itafikisha Dawah ya Kiislamu kwa ulimwengu ili kuziunganisha jamii zilizo chini ya mamlaka na utawala wa Dola ya Kiislamu kupitia Jihad, achilia mbali kuunda miungano na maadui wavamizi wa Kikafiri na kuwa na uwepo wao muovu hapa. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَكَفَى بِاللَّهِ شَهِيدًا]

“Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki, ili aitukuze juu ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi.” [Al-Fath:28].

Enyi Maafisa Wanyoofu katika Jeshi la Bangladesh, je hamuelewi kwamba watawala hawa wasaliti wanawatumia ninyi kama kafara katika vita vya mabwana zao Makafiri? Je, damu yenu haichemki kuona kwamba mumekuwa watu wa kutumika katika vita vya Makafiri? Watawala hawa wa duni bila aibu wanasema kwamba hawana matarajio ya kijeshi. Machoni mwao, nyinyi, kizazi cha jemadari shujaa Khalid bin Walid (ra) na Answari watukufu, ni zana za duni za kulinda maslahi ya Makafiri! Tunakuulizeni je, damu yenu ya Kiislamu imekusudiwa kumwagika kwa ajili ya Makafiri au kwa ajili ya Mwenyezi Mungu? Mnawezaje kutarajia wokovu wenu kesho Akhera kwa kuachana na Jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kutumiwa kwa maslahi ya Marekani kukabiliana na China? Vita vyenu lazima viwe ni Jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu; chochote kisichokuwa hicho hakitakuleteeni isipokuwa udhalilifu katika duniani na Akhera. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ameonya, «مَا تَرَكَ قَوْمٌ الْجِهَادَ إِلَّا ذُلُّوا» “Hawakuacha watu Jihad isipokuwa watadhalilika” [Ahmad]. Basi mtegemeeni Mwenyezi Mungu Al-Qawi, Mwenye nguvu, na fanyeni hima kuwaondoa watawala wa wasaliti wa kisekula na utawala wao. Toeni nusrah yenu (msaada wa kijeshi) kwa chama shupavu cha Hizb ut Tahrir ili kuiregesha Khilafah Rashida. Khalifa atakuongozeni katika Jihad kwa ajili ya ukombozi wa bara dogo hili zima ili kulifanya eneo hili kuwa ngome ya Uislamu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu