Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  6 Shawwal 1445 Na: H 1445 / 20
M.  Jumatatu, 15 Aprili 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ndege Mbili za Marekani Zilikuja Moja Kwa Moja Kutoka Tel Aviv na Kutua Nchini Mwetu; Hatua Muhimu ya Kuhalalisha Mahusiano na Umbile Haramu la Kiyahudi - kupitia hili, Serikali ya Hasina Imelivua Jani la Mulberry ambalo lilisitiri Uchi wa Usaliti Wake kwa Uislamu na Waislamu

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 28 Ramadhan 1445 H, Aprili 7, 2024 na siku takatifu ya Idd ul-Fitr, Aprili 11, 2024 nchini Bangladesh, wakati wananchi walikuwa wakisherehekea sikukuu yao, ndege mbili aina ya Boeing zilisajiliwa na zinazoendeshwa na shirika la National Air Cargo Inc. Marekani, ambazo zina uwezo wa kubeba shehena mbili za mizigo, zilitua kwa siri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hazrat Shahjalal jijini Dhaka kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Gurion wa Tel Avil nchini Israel. Ingawa ndege zote mbili zilikuja moja kwa moja kutoka Tel Aviv hadi Dhaka, zilifanya kituo chao cha pili kwenye uwanja wa ndege wa Sharjah nchini Imarati baada ya kuondoka kutoka Bangladesh. Ilibainika hapa kwamba Imarati (ambako ndege hiyo ilisimama) na Bahrain walitia saini Makubaliano ya Abraham jijini Washington DC mnamo Septemba 15, 2020, iliyofungishwa na Marekani, kuhalalisha mahusiano na 'Israel'. Kwa kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia na umbile la Kiyahudi kwa mara ya kwanza chini ya makubaliano haya, kumaliza sera ya miongo mingi ya kususiwa 'Israel' na nchi za Waislamu, waliweka mfano wa usaliti kwa Ummah wa Kiislamu. Kwa kutapatapa ili kusalia madarakani, serikali ya Hasina pia inajiunga na safu ya watawala hawa wasaliti wa Kiarabu na Waislamu kwa kuwahadaa watu. Wakati ukatili wa vikosi vya Mayahudi waliolaaniwa juu ya Waislamu wa Palestina unasumbua dhamiri ya ulimwengu wa wanadamu, wakati Waislamu ulimwenguni wanapaza sauti katika matakwa yao ya kupelekwa vikosi vya jeshi la Waislamu kukomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na Msikiti wa Al-Aqsa, wakati ombi la Waislamu kwa Mwenyezi Mungu (swt) katika mwezi huu wa Ramadhan ni ukombozi wa Palestina, basi hatua hii ya serikali ya Hasina kuhalalisha mahusiano na dola hii haramu ya 'Israel' imepitiliza.

Hasina ni mtawala mnafiki ambaye amewapotosha watu wa nchi hii kwa kumwaga machozi ya mamba kwa Waislamu wa Palestina. Amelaani vitendo vya 'Israel nchini Palestina katika Kongamano la hivi karibuni la Usalama la Munich na ameikashifu hadharani 'Israeli' mara kadhaa, akisema - 'Israel inafanya mauaji ya halaiki nchini Palestina'. Bado serikali yake inaendelea kudumisha mahusiano na umbile nyakuzi la Kiyahudi. Wakati watu wanalitaka jeshi la nchi hii lipelekwe kulinda Waislamu wa Palestina, serikali yake imetuma wanajeshi 75 wa Jeshi Wanamaji la Bangladesh hadi Lebanon chini ya misheni ya kulinda amani ili kulinda umbile la Kiyahudi kutokana na mashambulizi ya Mujahidina.

Hapo awali, serikali yake iliondoa maneno "isipokuwa Israel" kwenye  pasi za Bangladesh katika harakati za kuhalalisha mahusiano na dola haramu ya Kiyahudi. Wakati maisha ya Waislamu wa Palestina 33,000, pamoja na watoto na wanawake 25,000, yamepotea hadi sasa katika mauaji ya halaiki ya 'Israel', serikali ya Hasina, kwa kuruhusu ndege za 'Israel' kutua kwenye ardhi ya nchi hii, imechuruza damu zaidi ndani ya nyoyo za Waislamu na mshale wake wa udanganyifu na kufichua aibu ya mwisho ya usaliti wake kwa Uislamu na Waislamu. [قَاتَلَهُمُ اللَّهُ أَنَّى يُؤْفَكُونَ] “Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki?” [Surah Al-Munafiqun: 4].

Kwa kweli, serikali ya Hasina bila aibu inataka kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi kulingana na "Sera ya Dola Mbili" ya Marekani. Serikali ya Hasina iliweka hatua muhimu ya uhalalishaji mahusiano kwa kuruhusu kutua kwa ndege ya 'Israel' yenye makao yake Marekani kwenye ardhi ya nchi hii bila kujali hisia za watu na kuchagua njia ya usaliti kwa Uislamu na Ummah wa Kiislamu. Ni jukumu la Waislamu la Kiimani kuwakataa watawala hawa wasaliti kwa sababu wameuza Akhera kwa ulimwengu huu na kunali ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَوَلَّوْا قَوْمًا غَضِبَ اللَّهُ عَلَيْهِمْ قَدْ يَئِسُوا مِنَ الْآخِرَةِ كَمَا يَئِسَ الْكُفَّارُ مِنْ أَصْحَابِ الْقُبُورِ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye rafiki zenu watu ambao Mwenyezi Mungu amewakasirikia. Hao wamekwisha kata tamaa ya Akhera, kama makafiri walivyo wakatia tamaa watu wa makaburini.” [Al-Mumtahina: 13].

Enyi Watu! Tunapaswa kujua, mnamo 18 Mei 1901, mwakilishi wa Jumuiya ya Wazayuni inayoungwa mkono na Uingereza, alipendekeza ununuzi wa ardhi ya Palestina kwa Khalifa Abdul Hamid. Katika kujibu, Khalifa Abdul Hamid alisema, “Siwezi kuiacha hata shubiri moja ya ardhi nchini Palestina, kwa sababu sio mali yangu, lakini ni mali ya Ummah ya Kiislamu. Watu wangu wamepigania ardhi hii na kuinywesha kwa damu yao. Mayahudi nawabakie na mamilioni yao, na endapo siku moja Khilafah itavunjwa, basi wanaweza kuichukua Palestina, lakini sio wakati niko hai ... ”. Ummah wa Kiislamu umeshuhudia jinsi baada ya kuvunjwa Khilafah mnamo 1924 M, Mayahudi waliichukua Ardhi Takatifu ya Palestina kwa msaada wa Wakoloni Makafiri wa Magharibi, kwa kimya cha watawala vibaraka wa kisekula waliopandikizwa juu ya Ummah wa Kiislamu, bado wanaendelea kuwanyanyasa Waislamu wa Palestina wanaokwamilia Ardhi hii Takatifu na kila mara kuunajisi msikiti wa Al-Aqsa, Qibla cha kwanza cha Waislamu. Kwa hivyo, njia pekee ya kukomboa Palestina ni kuungana na Hizb ut Tahrir katika mapambano ya kisiasa ya kusimamisha tena Khilafah na kuhamasisha wale watoto wetu ambao wanahudumia katika jeshi kutoa Nusrah kwa Hizb ut Tahrir katika kusimamisha tena Khilafah, ambayo itakomboa Palestina kupitia operesheni za kijeshi, Insha'allah.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Surah Ar-Rum: 4-5].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu