Jumapili, 10 Dhu al-Hijjah 1445 | 2024/06/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  7 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: 1445 H / 24
M.  Jumatano, 15 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Furaha miongoni mwa Kipote cha Watawala wa Awami-BNP kuhusu Ziara ya Donald Lu nchini Bangladesh ni Dhihirisho la Kufilisika kwao kisiasa

(Imetafsiriwa)

Ziara ya Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Marekani katika Asia ya Kusini na Kati Donald Lu nchini Bangladesh, ni sababu ya furaha kwa watawala wa Awami-BNP wa nchi hiyo, lakini haitakiwi na kukataliwa na wananchi. Waziri wa Mambo ya Nje Dkt. Hasan Mahmud alisema kuhusu ziara ya Donald Lu, “Uhusiano wa Bangladesh na Marekani uko bora kuliko wakati wowote huko nyuma. Donald Lu anakuja Dhaka ili kuupeleka uhusiano huu kiwango cha juu. Pia tutajaribu kuimarisha uhusiano huu”. Kwa upande mwingine, chama kinachodorora cha BNP kwa mara nyingine tena kinasikika katika ulingo wa kisiasa kikitarajia kupata neema yake. Baadhi ya wale wanaoitwa wasomi wa wakala na wachambuzi wa kisiasa ambao hawajui mfumo na siasa za ulimwengu wanashughulika na kuchambua maelezo ya utawala siasa za kijografia za Amerika na China ili kuvutia umakini wa umma kwa kusisitiza kiwango chao cha werevu. Lakini mtu ana ufahamu mdogo anajua kwamba Marekani ni dola ya ukoloni mamboleo katika dunia ya sasa, na 'demokrasia na haki za binadamu' ni barakoa yake. Hivyo basi, lengo kuu la ziara ya mwanadiplomasia mkuu wa Marekani Donald Lu nchini Bangladesh ni kuleta msukumo katika utekelezaji wa miradi yao ya kikoloni kwa jina la ‘Ruwaza Huria na Wazi ya Indo-Pacifiki’. Miradi hii ni pamoja na, uanzishwaji wa bandari ya bahari kuu ya Matarbari, ACSA (Mkataba wa Upataji Huduma Pande zote) - GSOMIA (Makubaliano ya Usalama Jumla wa Habari ya Kijeshi), uundaji wa muungano wa kijeshi, ugawaji vitaru vya gesi ya mafuta (hydrocarbon) katika bandari mpya ya bahari kuu hadi Kampuni mpya ya Mashariki mwa India 'ExxonMobil'. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[إِنْ يَثْقَفُوكُمْ يَكُونُوا لَكُمْ أَعْدَاءً وَيَبْسُطُوا إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ وَأَلْسِنَتَهُمْ بِالسُّوءِ وَوَدُّوا لَوْ تَكْفُرُونَ]

Wakikuwezeni wanakuwa maadui zenu, na wanakukunjulieni mikono yao na ndimi zao kwa uovu. Na wanapenda muwe makafiri. [Al-Mumtahina: 2]. Kipote tawala cha kisekula cha Awami-BNP kinasaidia kuanzisha ukoloni mamboleo wa Marekani juu ya nchi hii ili kusalia madarakani au kutwaa madaraka, jambo ambalo ni wazi kama mchana kwa watu wenye ufahamu wa nchi hii. Kwa sababu hiyo, tabaka tawala la Awami-BNP limefilisika kisiasa na limetenganishwa na watu.

Enyi Wanasiasa Wenye Ikhlasi na Wasomi! Munatambua jinsi Wakoloni Makafiri wa Magharibi wamewatumbukiza wanadamu katika vita na maafa kwa jina la amani! Mwenyezi Mungu (swt) anaonya juu yao,

[وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ قَالُوا إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ * أَلَآ إِنَّهُمْ هُمُ ٱلْمُفْسِدُونَ وَلَٰكِن لَّا يَشْعُرُونَ]

Na wanapo ambiwa:Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji. Hakika wao ndio waharibifu, lakini hawatambui. [Al-Baqarah:11-12].

Tunapenda kukumbusheni mfano wa At-Tufayl Ibn Amr Ad-Dawsi (mshairi mkubwa na mtu mwenye akili sana wa zama hizo) ambaye alipuuza hila za Maquraish, watawala wajinga wa Makka, na akafuata haki na imani thabiti ya Uislamu ulioteremshwa kwa Mtume (saw). Mnapaswa kutoka katika kufuata kwa upofu hila na maadili ya Kisekula, na kuungana na chama cha wakweli Hizb ut Tahrir katika mapambano ya kifikra na kisiasa kupinga ukoloni mamboleo. Kama mnavyofahamu, Hizb ut Tahrir imekuwa ikifanya mapambano ya kifikra na kisiasa kote duniani ili kuukomboa Umma wa Kiislamu kutoka kwa ukoloni wa nchi za Magharibi kwa kusimamisha tena Khilafah na imekuwa ikiwaita maafisa wenye ikhlasi katika jeshi kutoa nusrah kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah. Ni Khilafah inayokuja pekee ndiyo itakayobadilisha mfumo wa kilimwengu wa Kikoloni-Kibepari wa sasa usio na maadili na ubinadamu na kuunda mfumo wa haki na utu wa kilimwengu. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

[وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلاَّ رَحْمَةً لِلْعَالَمِينَ]

“Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.” [Al-Anbiya: 107].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu