Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
H. 16 Dhu al-Qi'dah 1445 | Na: 1445 H / 25 |
M. Ijumaa, 24 Mei 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ili Kuthibitisha Utiifu wake kwa Mkruseda Marekani, Serikali ya Hasina imekuwa ikiwakamata na kuwatesa Watetezi wa Khilafah Rashida na Inapigana Vita dhidi ya Dini ya Uislamu
(Imetafsiriwa)
Katika muendelezo wa mateso ya kimfumo dhidi ya wale wanaobeba Da'wah ya Uislamu na Khilafah, mnamo tarehe 14 Mei, 2024, majambazi wa vikosi vya serikali walimkamata Hedayet Hosen (umri wa miaka 57) - mtetezi wa ulinganizi wa kusimamishwa tena Khilafah Rashida, na wakati wa kuhojiwa rumande walimtesa kiasi kwamba alilazimika kulazwa hospitalini. Ilibainishwa kuwa Hedayet Hosen alikuwa katibu mkuu wa 'Projonmo 71'. Alipotambua kwamba ule unaoitwa utaifa na usekula ni kinyume cha itikadi ya Uislamu na ni zana za ukoloni, ambazo kwazo wakoloni wanaugawanya Umma wa Kiislamu, wakijihusisha na uadui na vita baina yao, na kupora rasilimali za Umma wa Kiislamu, tangu wakati huo amekuwa mtetezi mchangamfu wa Khilafah tukufu - nembo ya utawala wa Shariah na umoja wa Umma wa Kiislamu. Msimamo wake huu wa ikhlasi umefunua barakoa ya wale wanaoitwa mabingwa wa vita vya ukombozi vya serikali ya Hasina na usekula usiotambua Mungu. Kutoka kwa Abu Hurairah (ra) amesema, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: “Mwenyezi Mungu (swt) anasema, «مَنْ عَادَى لِي وَلِيًّا فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ» “Ikiwa mtu atamfanya mja wangu kuwa ni mja wangu uadui kwa sababu ya kujinasibisha kwake na Mimi, basi nimetangaza vita juu yake.” (Bukhari, Hadithi: 6502). Serikali ya Hasina, adui wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, imekuwa ikiwakamata na kuwatesa watetezi wa Khilafah tukufu ili waendelee kubaki madarakani kwa kupata imani ya Mkruseda Marekani, na inapigana vita dhidi ya Dini tukufu. Serikali ya Hasina imeweka historia ya kuharibu uchumi wa nchi na maisha ya watu, lakini imeweza kupata imani ya Mkruseda wa Kimagharibi katika vita vyake dhidi ya Uislamu na Waislamu. Matokeo yake, Hasina Mkruseda wa demokrasia, amejitaja kama badali pekee na akaiambia Marekani, "Swali langu ni, ikiwa watanipindua, basi nani atakuja wakati mwingine? Je, walirekebisha? Hilo ndilo swali langu” [Daily Jugantor, Mei 03, 2024].
Enyi Watu! Kifungu cha 39 cha Katiba ya Jamhuri ya Watu wa Bangladesh kinasema, (1) Uhuru wa fikra na dhamiri umehakikishwa. (2) kwa kuzingatia vikwazo vinavyofaa vilivyowekwa na sheria kwa maslahi ya usalama wa taifa, mahusiano ya kirafiki na mataifa ya kigeni, utulivu wa umma, adabu na maadili, au kwa kudharau mahakama, kashfa au uchochezi wa uhalifu - (a) haki ya kila raia ya uhuru wa kuzungumza na kujieleza, na (b) Uhuru wa vyombo vya habari ulihakikishwa. Sasa unauliza, ni kwa katiba gani serikali ya Hasina inawakamata na kuwatesa wanaobeba matakwa ya Uislamu?! Kwa hakika, mfumo huu wa kisekula na katiba iliyotungwa na mwanadamu ni uongo na udanganyifu wa wazi, na si chochote ila ni chombo cha kuwakandamiza wananchi! Hivyo Mwenyezi Mungu (swt) anasema:
[وَمَنْ لَمْ يَحْكُمْ بِمَا أَنْزَلَ اللَّهُ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ]
“Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhaalimu.” [Surah Al-Ma'idah: 45].
Enyi Watu! Sisi, kwa niaba ya Hizb ut Tahrir, tunatoa wito kwenu muamke na kuutupilia mbali mfumo uliopo wa kisekula, mufuate nyayo za watetezi wa dhati wa Khilafah Rashida. Unganeni katika mapambano ya kifikra na kisiasa pamoja na Hizb ut Tahrir ili kusimamisha tena Khilafah ili kuuondoa utawala huu dhalimu wa sasa. Mwenyezi Mungu (swt) ametuonya juu ya kuwa mtazamaji aliye kimya katika jambo hili. Anasema (swt):
[وَاتَّقُوا فِتْنَةً لاَ تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْكُمْ خَاصَّةً وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ]
“Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu walio dhulumu peke yao kati yenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” [Surah Al-Anfal: 25].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Bangladesh |
Address & Website Tel: +88 01798 367 640 www.ht-bangladesh.info |
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd |