Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  1 Dhu al-Hijjah 1445 Na: 1445 H / 28
M.  Ijumaa, 07 Juni 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kutokana na Mikutano na Maandamano kote Nchini, Wanafunzi na Watu Jumla Wanataka Ukombozi wa Palestina

(Imetafsiriwa)

Watu jumla na hasa wanafunzi wa ngazi zote, wakiwemo wanafunzi wa vyuo vikuu, vyuo na shule mashuhuri nchini humu, wamekasirishwa na kuendelea kwa mauaji ya Waislamu wa Palestina na umbile lililolaaniwa la Kiyahudi, na kutokana na mikutano mbalimbali, maandamano yenye mfano minyororo ya kibinadamu, wanataka ukombozi wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma katika mji mkuu wa Dhaka kama vile: Chuo Kikuu cha Uhandisi na Teknolojia cha Bangladesh (BUET), Chuo Kikuu cha Dhaka, Chuo Kikuu cha Wataalamu cha Bangladesh (BUP), Chuo Kikuu cha Jagannath; Vyuo vikuu vya kibinafsi kama vile Chuo Kikuu cha Kaskazini Kusini, Chuo Kikuu cha BRAC, Chuo Kikuu cha Mashariki ya Magharibi, Chuo Kikuu cha Independent, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Amerika cha Bangladesh, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Daffodil, Chuo Kikuu cha Uttara, Chuo Kikuu cha Kaskazini, Chuo Kikuu cha Sanaa ya Huru, Chuo cha Matibabu cha Anwer Khan; pia katika miji ya tarafa, Chuo Kikuu cha Chittagong, Chuo Kikuu cha Comilla, Chuo Kikuu cha Khulna, Chuo Kikuu cha Rajshahi, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Shahjalal (SUST) pamoja na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya umma na vya kibinafsi na shule mbalimbali zinazojulikana za mji mkuu Dhaka kama vile Chuo cha Dhaka, Chuo cha Notre Dame, Chuo cha Umma cha Bir Shrestha Munsi Abdur Rauf, Chuo cha Umma cha Bir Shrestha Noor Mohammad Shule ya Upili na Chuo cha St. Gregory, Chuo cha Milestone, Shule ya Upili na Chuo cha Uttara, Shule ya Mastermind, Shule ya Monipur, zilifanya mikutano ya hadhara, maandamano ya minyororo ya binadamu, kwa ajili ya ukombozi wa Wapalestina katika maeneo ya umma ikiwemo vyuoni mwao wenyewe.

Kwa kuongezea, vijana pamoja na watu wa matabaka mbalimbali walipanga mikutano ya hadhara, maandamano ya minyororo ya kibinadamu huko Wari, Dhanmondi, Mohammadpur, Khilgaon, Basabo, Rampura, Hatirjheel, Mogbazar, Mowchak, Banshri, nk. ili kuonyesha mshikamano wao kwa Waislamu wa Palestina na kutaka kuikomboa Palestina. Wakiimba kwa kauli mbiu maarufu kama vile “Takbir: Allahu Akbar”, “Kutoka Mto hadi Bahari, Palestina itakuwa huru”, “Iacheni huru! Iachane huru! Palestina!”, walionesha bendera za Shahada zinazoonyesha ushindi wa Uislamu, na mabango mbalimbali kama vile: “ISRAEL’ NI KIVULI CHA WATAWALA WA KIARABU”, “KOMESHENI MAUAJI YA HALAIKI” “SIMAMENI PAMOJA NA PALESTINA” “IACHENI HURU PALESTINA”, “HAPANA KWA UN”, “SULUHISHO LA DOLA MBILI NI UDANGANYIFU” “UMMA MMOJA, MWILI MMOJA” “YUKO WAPI SALAHUDDIN WETU?” “MAJESHI KWA AL-AQSA”, nk. Aidha, “Msafara wa Baiskeli” na “Msafara wa Magari” wa vijana ilipita katika barabara tofauti za mji wa Dhaka, huku watu wa pande zote mbili za barabara wakipunga mikono yao na kuonyesha uungaji mkono wao kwa ukombozi wa Palestina.

Enyi Watu! Ingawa, vibaraka wa Makruseda wa Magharibi, watawala wa sasa, pamoja na vyombo vya habari tiifu, wanajaribu kudhibiti kila pumzi ya Umma wa Kiislamu, lakini wana wa Umma huu - na hasa vijana hawa wanaosoma katika vyuo na vyuo vikuu hawajawasahau Waislamu wa Palestina, na hili ndio dhihirisho la maumbile Asili ya umoja, imani na mihemko ya Umma huu, ambao kipote cha watawala hawa licha ya juhudi zao hawajaweza kuyaondoa katika nyoyo za Umma huu.

Enyi Maafisa Wanyofu katika Jeshi, Enyi Warithi wa Salahuddin! Hakika nyoyo zenu zinavuja damu kwa ajili ya Waislamu wa Palestina. Damu yenu inachemka kwa sababu munashuhudia utawala huu katili ukikutumeni kulinda maslahi ya nchi za Magharibi kwa jina la ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, huku kwa upande mwingine ukikufungeni minyororo kuilinda ardhi iliyobarikiwa ya al-Aqsa na Waislamu nchini Palestina. Kwa hiyo, tokeni nje ya kambi musimame pamoja na watu. Waondoeni watawala wa sasa na muipe nusrah Hizb ut Tahrir, chama cha kweli ili kusimamisha Khilafah. Khilafah tukufu itaunganisha majeshi ya Umma wa Kiislamu na kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, Insha'Allah. Mwenyezi Mungu (swt) anakuahidini msaada katika kufikia mafanikio katika kazi hii, na kisha watu wote wa nchi hii watakupongezeni wakipiga takbira: “Allahu Akbar, Allahu Akbar, wa Lillahil Hamd”.

[إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الأَشْهَادُ]

“Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi” [Surah Ghafir: 51].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu