Afisi ya Habari
Kenya
H. 3 Rabi' II 1437 | Na: 1437/05 |
M. Jumatano, 13 Januari 2016 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Usekula Unapanda Uovu Wake kwa Dini Kuu
Mkuu wa Sheria wa Kenya, Bw. Githu Muigai, ametengeza mswada wa sheria za kuyadhibiti mashirika na makundi ya kidini pamoja na wahubiri wake. Sheria hizi zinadaiwa kuwa ni njama ya serikali ya kukomesha vitendo viovu vya kitapeli vinavyo tekelezwa na baadhi ya makanisa na pia kupambana dhidi ya misimamo mikali ya kidini. Hili kwa jumla limezuia hisia kali kwa viongozi wote wa kidini huku wengi wao wakizikemea sheria hizi zilizopendekezwa. Sisi katika Hizb ut Tahrir / Afrika Mashariki tungependa kueleza yafuatayo:
Tunakemea vikali sheria hizi ambazo kwa uhalisia ni dhihirisho la uchafu na ufisadi wa fikra ya kisekula ambayo imewapa wanadamu uhuru wa kutunga sheria na kukiuka utukufu wa kidini. Tunaeleza kinaga ubaga kuwa sheria hizi zilizopendekezwa ni kinyume na ile inayodaiwa kuwa ni haki ya kikatiba ya uhuru wa kuabudu na kwamba dola haipaswi kuingilia dini!
Ama matatizo ya kanisa ya vitendo vya uhadaifu na utapeli, bila shaka hiyo ni sehemu tu ya matatizo mengi ambayo mujtama wa kirasilimali unakabiliwa nayo. Haya ni matunda ya mfumo muovu wa kirasilimali ambayo yanachangia katika ulimbikizaji mali kwa njia zozote zile. Suluhisho halisi la kupambana na tatizo hilo na mengineyo ni kuutupilia mbali mfumo wa kirasilimali ambao umewaangamiza watu ikiwemo wale wanaojulikana kama viongozi wa kidini. Hivyo basi ni dhahiri shahiri kuwa hili ni jaribio jengine tena la kuficha aibu ya mfumo wa kirasilimali ambao umeufisidi mujtama mzima na hususan tabaka lake la wanasiasa ambalo kila uchao huiba mali ya umma na kuwaacha raia wakiteseka.
La kushangaza sheria hizi mpya ni sehemu ya silaha hatari za serikali za kudhibiti ulinganizi wa Kiislamu ambao unalenga kuukomboa ulimwengu kutokana na majanga ya warasilimali. Kabla ya sheria hizi, kuna sheria za kikatili zilizopitishwa dhidi ya Waislamu kwa jina la vita dhidi ya ugaidi. Na sio hilo tu, Sheria za Kiislamu zinapigwa vita vikali chini ya pazia ya kupambana na uvukaji mipaka, misimamo mikali na ugaidi.
Tunatamatisha kwa kusema kuwa Usekula ambao ndio muhuri wa demokrasia katika kutunga sheria za kiajabu na za kikatili ni itikadi fisidifu na haipaswi kuchukuliwa na watu wote wa dini kuu. Kinachovunja moyo ni kuwa huku kanisa likipinga vikali sheria hizi mara kwa mara tunaliona likisimama pamoja na dola za kisekula katika kupigana dhidi ya Uislamu! Kutokana na hilo Uislamu haukubaliani na fikra za kisekula kwa sababu zinagongana na umbile la mwanadamu. Mwenyezi Mungu (swt) amewaumba wanadamu na kuwapa nidhamu kamili ili washikamane nayo hapa duniani na sio kutunga sheria zinazo sababisha aina zote za matatizo.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kenya |
Address & Website Tel: +254 707458907 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke |