Afisi ya Habari
Kenya
H. 20 Jumada I 1437 | Na: 1437/07 |
M. Jumatatu, 29 Februari 2016 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ufisadi Nchini Kenya
Kwa mara nyingine tena, Kenya iko katika kurunzi ya ulimwengu kuhusiana na ufisadi. Kwa mujibu wa utafiti kuhusiana na matukio ya uhalifu wa kiuchumi uliotolewa jijini Nairobi mnamo Ijumaa 26 Februari 2016 na kampuni ya uhasibu ya Price Waterhouse Coopers (PwC), Kenya imeorodheshwa nchi ya tatu fisadi zaidi ulimwenguni. Hii ni kwa mujibu wa utafiti huu, Kenya angalau ilifanya vyema kuliko Afrika Kusini na Ufaransa. Matokeo haya yanajiri siku chache tu baada ya Rais Uhuru Kenyatta kusema Wakanya ni mahiri katika wizi, kamari na kueneza ukabila. Maoni haya ya Rais yalitanguliwa na Hakimu Mkuu Willy Mutunga wakati wa mahojiano ya gazeti wiki kadhaa kabla ambapo aliliambia gazeti la Kiholanzi NRC Handelsblad kuwa Kenya imekuwa uchumi wa kijambazi ambao ufisadi umepenya katika viwango vyote vya mujtama.
Kuhusiana na hili chama cha Kiislamu cha Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki kingependa kufafanua yafuatayo:
Kwa kuwa Kenya imejifunga na mfumo wa Kimagharibi wa Kirasilimali, si ajabu basi kuwa katika hatari ya uovu wa ufisadi. Nidhamu iliyoathirika na ulafi mkubwa wa kulimbikiza mali kwa njia na gharama zozote zile. Hii hulifanya tabaka zima la wanasiasa ndani ya serikali ya kirasilimali kuchafuliwa na wizi na ufisadi.
Tafiti zinazofanywa kila baada ya muda fulani mbazo baadaye huja na matokeo ya uorodheshaji mataifa yaliyo na viwango vikubwa vya ufisadi, rushwa, umasikini nk, zote hazisaidii na hazina kitu cha kudhibiti maafa haya. Matokeo haya yanasaidia tu katika kutupa sisi maalumati na takwimu chache pekee huku ulimwengu mzima ukikabiliwa na majanga isiyokuwa na idadi. Fauka ya hayo, tafiti hizi kwa kawaida hulenga kuunganisha aibu na uovu wa Urasilimali ambao daima tumekuwa tukisema ndicho chanzo pekee cha majanga yote yanayo ukumba ulimwengu.
Viongozi na wanasiasa wote wa kirasilimali hawatarajiwi kumaliza ufisadi kwani uhalisia wa uongozi katika mfumo wa kirasilimali ni fursa ya kulimbikiza na kufuja mali ya umma. Ili kufinika uovu huu mbaya huanzisha tume za mara kwa mara za kupigana na ufisadi huku tume zizi hizi zikitumiwa kama hifadhi za wafisadi.
Ama kupiga kwao kelele kwa kukemea na kufichua ufisadi ni uhadaifu tu wa kuwaziba macho raia na kucheza na hisia za umma kwa manufaa yao kwa kuonekana kana kwamba wanajali kisiasa na kuwafichua mahasimu wao wa kisiasa kama wabaya ilhali wote ni gora moja inapokuja uporaji wa mali za umma.
Mwisho kama tunavyoendelea kurudia kwamba chanzo cha ufisadi ni nidhamu chafu ya kirasilimali, kuna haja ya kuing'oa nidhami hii kikamilifu na kuibadilisha kwa Uislamu – mfumo adilifu na wa kweli unaotekelezwa kwa muundo wa Khilafah ya Uongofu kwa njia ya Utume. Kwa karne kumi na nne ambazo Uislamu ulitawala nusu ya dunia kesi za ufisadi zilikuwa ni nadra kama kulikuwepo na yoyote.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kenya |
Address & Website Tel: +254 707458907 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke |