Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  17 Rabi' II 1437 Na: 1437/06 H
M.  Jumatano, 27 Januari 2016

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Je, Mumeshuhudia Waziwazi Uhadaifu wa Demokrasia Nchini Zanzibar?

Siku chache zilizopita, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ilitangaza kuwa mnamo 20 Machi 2016 itakuwa ndio siku ya Marudio ya Uchaguzi ambao ulikuwa umefanyika mnamo 28 Oktoba 2015. Katika uchaguzi huo Chama cha Muungano wa Wananchi (CUF) kilitoa takwimu za Mgombezi wao wa Uraisi kuwa alishinda wadhifa huo.

Cha kushangaza, Mwenyekiti wa ZEC alitangaza kubatilisha uchaguzi huo. Licha ya tangazo kutoka kwa waangalizi wa uchaguzi wa nchini na kimataifa, kusema kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki. Huu ni uchaguzi wa nne tangu kuanzishwa kwa vyama vingi mnamo 1995. Chaguzi zote zimeshuhudia ghasia na vurugu hususan katika wadhifa wa Urais, ambao chama cha CUF takribani mara zote hizo kimetangaza ushindi, lakini baadaye, mgombezi wa urais kutoka katika Chama tawala Cha Mapinduzi (CCM) hutangazwa mshindi.   

Kufuatia kadhia hii, Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki inaendelea kuwakumbusha Waislamu nchini Zanzibar na watu wote kwa jumla yale ambayo tumekuwa tukiyaeleza mara kwa mara na bila ya kukata maneno:

1. mfumo wa vyama vingi ulioanzishwa na Wamagharibi kwa maslahi yao wenyewe, na sio kwa maslahi ya nchi zetu umetiliwa shaka na wengi kufikia hadi watu kuchanganyikiwa huku matarajio makubwa yakiporomoka, muda mwingi kupotea, kutoa jasho jingi – hata kupoteza maisha kwa matarajio ya mabadiliko. Badala yake umeletwa kama njama ya kubadili sura ya serikali kwa kutambua kwamba watu wamechoshwa na kuna hisia ya kutoridhika kutokana na ukatili wa mfumo wa chama kimoja. Vilevile mpangilio huu ulichochewa na mabadiliko ya matukio ya kisiasa ya kiulimwengu ambayo kimataifa yalisababishwa na kuporomoka kwa Umoja wa Nchi Huru za Kisovieti (USSR) na Marekani kuibuka kama dola kuu pekee katika uwanja wa kiulimwengu.   

2. Uchaguzi kwa msingi wa demokrasia yaani kuwapa wanadamu haki ya kutunga sheria pasi na Mwenyezi Mungu, uchaguzi huu mbali na kuwa ni haramu katika Uislamu, pia hauna athari wala maamuzi ya ima kumweka kiongozi au kumwondoa. Badala yake uchaguzi huu hutumika kuwafunga macho, kuwapumbaza raia, kusababisha migawanyiko na kutengana miongoni mwao na kuwaweka watu mbali na kufikiria suluhisho halisi la matatizo yao. Huku dola kuu zikitumia ukoloni mamboleo kuendeleza ulimbikizaji na ufujaji wa rasilimali na huku raia wakifiri kwa upofu kuwa wanafanya maamuzi muhimu ya kisiasa kwa nchi yao.  

3. Vyama vya kidemokrasia eneo la Afrika Mashariki ni vibaraka wa dola kuu. Baadhi ya vyama vimepewa dori ya utawala ili kulinda maslahi ya dola kuu na vyengine ni kwa ajili ya kuwahadaa raia kuona kuwa kuna muendelezo wa mchakato wa kidemokrasia.

CCM inajuwa fika kuwa hakuna demokrasia kupitia wao kudhibiti chaguo la watu! Licha ya wao kujionyesha kama wasimamizi wa vyama vingi. Huku vile vyama vinavyoitwa vya upinzani ikiwemo CUF vinajua vizuri sana kuwa ili kwao kukwea madaraka ni lazima kuwepo na utambuzi kutoka kwa dola kuu hata kama vyama hivyo vya upinzani vitapata kura za kutosha. Kutokana na hayo vyama vya utawala pamoja na vya upinzani vinawadanganya raia na kuwadhalilisha kuwa viumbe duni kabisa wa kutumiwa katika kupata maslahi yao pekee.

4. Dola za Kimagharibi zinatambua kuwa hakuna demokrasia kwa uhalisia wake. Vilevile dola hizo haziko kusimamia haki kwani ziko mamlakani ili kulinda maslahi yao pekee. Hivyo daima humweka kibaraka wao mtiifu uongozini ili kulinda maslahi yao ima awe amepata kura nyingi, kura chache au hakupata kitu kabisa.

5. Demokrasia na udikteta ni pande mbili za sarafu moja. Katika hali zote hizi katiba na sheria hutungwa na kutekelezwa na wanadamu ambao wameleweshwa na maslahi na hawajali halali na haramu wala kumcha Mwenyezi Mungu (swt). Hivyo basi upuza katiba zao wenyewe na kukiuka sheria zao wenyewe ni kitendo cha kawaida pindi maslahi yao yanapohusika kama ilivyoshuhudiwa katika uchaguzi uliofutiliwa mbali nchini Zanzibar. Licha ya ukweli kuwa katiba na sheria chimbuko lake ni akili za wanadamu zilizo na kikomo. 

6. Tunawakumbusha Waislamu wa Zanzibar na kuwasihi kwa unyenyekevu kuwa dola za Kimagharibi zina tayarisha mazingira ya umwagaji damu zenu kama zilivyofanya kwa ukatili mnamo 1964 na 2001; kisha baadaye wanaoathirika zaidi ni raia wa kawaida. Mwishowe, CUF na CCM zitakaa chini kwa utulivu kugawanya ngawira kana kwamba hakuna chcohote kilichotokea katika maisha yenu matukufu. Kwani vyama vyote hivi vinamilikiwa na bwana mmoja Amerika.

Kwa mukhtasari, Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki kamwe haitoacha kuwalingania tena na tena Waislamu: Amkeni kutoka katika usingizi mzito wa kuing'ang'ania nidhamu fisidifu ya demokrasia iliyo wazonga nyinyi na ulimwengu mzima kwa majanga yasiyo mithilika, idhilali na vurugu. Tunawaulizeni; je, wakati haujawadia kwenu kuungana na Hizb ut Tahrir katika kuulingania mfumo wa Kiislamu. Mfumo pekee ulio na haki na uadilifu ili kutekeleza yale yanayomridhisha Muumba wetu kwa muundo wa dola ya Khilafah kwa njia ya Utume? Au je, munahitaji dalili zaidi za kuthibitisha uharamu wa nidhamu ya kidemokrasia? Zishaurini nyoyo zenu na mutafakari, je munakumbuka mwanzoni mulikuwa chini ya Ufalme, na baadaye chini ya vyama vingi baada ya uhuru wa bendera mnamo 1963, kisha mukawa na chama kimoja baada ya mapinduzi ya 1964, na kisha mukarudi tena kwa vyama vingi. Je, bado mungali hamuja tambua kwamba safari yenu imefika mwisho? Je, munataka kumfanya Mwenyezi Mungu (swt), Muumba wenu, awe ndio chaguo lenu la mwisho baada ya msururu wa kufeli? Hivyo basi amkeni na mutambue. Itumieni fursa hii kabla haijatoweka! 

Masoud Msellem
Naibu Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu