Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  14 Jumada I 1444 Na: 1444 H / 022
M.  Alhamisi, 08 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Achaneni na Vijana na Wanawake wetu!

Wanawake wa Palestina Wanapinga Mipango ya Mashirika ya Wanawake katika Shule zetu na Wanataka Yaondolewe Mashuleni

(Imetafsiriwa)

Kitabu, ‘The Handbook against Child Marriage’, kilichotayarishwa na Kituo cha Mafunzo ya Wanawake nchini Palestina chini ya mpango uliopewa jina la Haya unaofadhiliwa na shirika la Ujerumani la Brot für die Welt - ReliefWeb [Bread for the World – Protestant Development Service] na kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu ya Mamlaka ya Palestina inawalenga wanafunzi wa kiume na wa kike kuanzia darasa la saba hadi la kumi na moja. Ni mwongozo wa maelekezo unaofanya kazi kutumia nafasi ya walimu na washauri wa elimu shuleni, ili kufifisha fahamu za Uislamu na kukuza fahamu na maadili ya Magharibi, na wanajaribu kuwatumia walimu na washauri, ili kupigia debe utamaduni wa jinsia na kupambana na thaqafa na desturi za Kiislamu. Inaruhusu na kutoa njia kwa mtindo wa maisha wa LGBTQ+, na kuionyesha ndoa kwa walio chini ya umri wa miaka kumi na nane kama ukiukaji wa haki za watoto huku ikitetea ukombozi wa kingono na majaribio yake chini ya umri wa miaka kumi na nane.

Mashirika na vituo hivi vya wanawake vinaungwa mkono kwa kiasi kikubwa na mipango na mashirika ya serikali za Magharibi ambazo zinajifakhiri kuunga mkono na kufadhili maelezo bora zaidi ya kusukuma programu hizi kama vile Aman, Tamkeen, Haya na mengine mengi shuleni kuwapeleka washauri waelekezi wa shule kwenye warsha zao kuwafundisha mitindo mipya ya kufunza. Lengo ni kueneza programu zao za kutomcha Mungu kwa kutumia uchezaji dori, mitindo ya kupeana mawazo, mbinu za kujifunza kucheza ili kupanda mbegu za uhuru wa kisekula, uhuru wa kijinsia, usawa wa kijinsia, hakuna ndoa chini ya miaka 18 ilhali kujivinjari na kufanya majaribio ya ngono yote yakiwa ndani ya nyanja haramu, jinsia na aina zake ili kuruhusu waliobadili jinsia na LGBTQ+ wote katika hatua muhimu ya ujana.

Kitambulisho cha Kiislamu kiko wapi? Iko wapi Aqidah ya Kiislamu? Yako wapi maadili ya Kiislamu kwa mujibu wa yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu (swt) kwa waja wake? Haya yote yanalazimishwa na Makafiri kupitia vyama vya wanawake baadhi yao katika mfumo wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO's) ambayo huamuru na kutaka katika sheria zao ufikiaji kamili wa mashule ambapo Mamlaka ya Palestina (PA) hutii kikamilifu.

Kwa hiyo watu na wazazi wa Palestina waliosimama kama ngao madhubuti ya kuwalinda watoto wao walikuwa na dori muhimu.

Kutokana na hali hiyo, wazazi, viongozi wa jamii, mawakili, wanaume na wanawake, waliokusanyika na kutoa kero zao katika ngazi zote kuanzia ziara za kibinafsi kwa wazazi wengine, waelimishaji na washauri waelekezi kwenye ziara rasmi za wizara ya elimu katika wilaya za eneo hilo hadi ziara za shule kwa walimu wakuu wa shule hadi kwa  washauri waelekezi (ambao ndio njia kuu ya kufundisha mipango hii) kupitia maeneo mbalimbali kuanzia miji ya Quds, Ramallah, Bethlehem hadi Nablus na vijiji na miji anuwai, wote walishirikiana kupinga programu hizi na kutaka ziondolewe katika shule zetu. Miito na matukio haya ya dharura yaliibua utambuzi miongoni mwa watu ambao walionyesha mshtuko na hasira zao kwa Mamlaka ya Palestina kushirikiana na mipango kama hiyo.

Alhamdulillah, ziara hizo zilikataliwa vikali na waelimishaji na walimu wakuu wa shule kwa programu hizi chafu zilizopangwa kuwaharibu watoto wetu. Huku wengine wakikanusha kuwa programu hizo zilikuwa zikifundishwa katika shule zao ingawa uhalisia ulithibitisha tofauti. Na wengine walipitia nyenzo kabla na kurekebisha yale yaliyofundishwa ili yasigongane na maadili ya Kiislamu.

Kama ishara wakati wazazi na umma wanapokusanyika pamoja ili kupaza sauti moja dhidi ya mipango ya kikafiri ya kukoloni, Wizara ya Elimu ya PA ilitoa ilani ya dharura inayoagiza kusitishwa mara moja kwa programu za Haya na amali nyengine zinazohusika nayo katika mashule hadi watakapojulishwa baadaye.

 Wazazi na Watu wa Palestina - vita havikukoma kwani haya ni mafanikio ya muda mfupi tu katika mfululizo wa vita vingi vijavyo... vyama hivi vya wanawake vitakutana katika ngazi za juu na maafisa wa serikali pamoja na wasaidizi wao ili kurekebisha programu zao ili kuwafanya wakubalike zaidi kwa watu wa Palestina. Baya zaidi mashirika haya kama vile Taasisi ya Tamer yanaitaka PA kushirikiana kamilifu na kuishinikiza Wizara ya Elimu ya PA iruhusiwe kuingia kikamilifu mashuleni vyovyote itakavyokuwa kwa matamshi ya ujasiri ambayo si njama za siri tena. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[وَتَرَى كَثِيراً مِّنْهُمْ يُسَارِعُونَ فِي الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَأَكْلِهِمُ السُّحْتَ لَبِئْسَ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ]

“Na utawaona wengi katika wao wanakimbilia kwenye dhambi, na uadui, na ulaji wao vya haramu. Ni maovu mno hayo wayatendayo!” [Al-Maidah: 62].

Kuna malalamiko ya mwakilishi wa vyama vya wanawake kwa Gavana wa Bethlehem ya "maendeleo" ya polepole ya PA katika kutekeleza itifaki za CEDAW pamoja na kushindwa kufikia matokeo yaliyotarajiwa ya programu hizi katika mujtamaa na shule za Palestina. Wito huo uko hadharani kuwatia usekula na hata kuwachafua mabongo watoto wetu kutumbukia kwenye upagani na kuvumilia na kukubali LBGTQ+ bila kumuogopa Mwenyezi Mungu (swt).

Mapambano baina ya Haki na Batili yatabakia mpaka Siku ya Kiyama. Mapambano kama yanavyoelezewa ipasavyo ni mapambano ya kukataza maovu na kulingania mema kwa sauti kubwa. Hapa ni lazima tuendelee kufahamu njama hizi dhidi ya Ummah wetu katika Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina na tuzifichue na kuzipinga, tukilingania kutabikishwa kwa Uislamu na imani na maadili yake ya kimsingi. Na tuwatetee watoto wetu, la sivyo kizazi kijacho kitafikiria Dini yao kuwa ni suala tu la kibinafsi au jambo la kuepukwa au hata kujiepusha na kuamrisha mema na kukataza maovu, na kuzikumbatia fahamu zenye sumu za kukubali aina zote za maovu, na kuwapoteza milele vijana wetu wa Kiislamu katika dimbwi la usekula na upotovu.

Sisi katika Kitengo cha Wanawake cha Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir tunakukumbusheni kauli ya Mwenyezi Mungu (swt) akisema:

[وَلاَ يَزَالُونَ يُقَاتِلُونَكُمْ حَتَّىَ يَرُدُّوكُمْ عَن دِينِكُمْ إِنِ اسْتَطَاعُواْ وَمَن يَرْتَدِدْ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَيَمُتْ وَهُوَ كَافِرٌ فَأُوْلَئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ وَأُوْلَـئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ]

“Wala hawatoacha kupigana nanyi mpaka wakutoeni katika Dini yenu kama wakiweza. Na yeyote katika nyinyi akiacha Dini yake akafa naye ni kafiri, basi hao ndio ambao a'mali zao zimeharibika duniani na Akhera. Na hao ndio watu wa Motoni; humo watadumu.” [Al-Baqara: 217].

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu