Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  13 Jumada I 1444 Na: 1444 H / 021
M.  Jumatano, 07 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watoto wa Afghanistan: Wamenaswa katikati ya Kuuwawa na Njaa

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 30 Novemba, takriban watu 17 waliuawa na wengine 26 kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu katika madrasa huko Aybak, mji mkuu wa mkoa wa Samangan kaskazini mwa Afghanistan. Wengi wa waliouawa wanaaminika kuwa watoto wenye umri wa miaka 9-15. Katika kipindi cha miezi 15 iliyopita, kumekuwa na mashambulizi kadhaa dhidi ya madrasa, ikiwemo mikoa ya Mazar-e-Sharif, Balkh na Kunduz. Septemba hii, mlipuaji bomu mmoja aliwalenga wanafunzi wa kike katika kituo kimoja cha elimu jijini Kabul, na kuwaua karibu wasichana 50 na wanawake wachanga na kuwajeruhi makumi ya wengine. Watoto wa Afghanistan pia wanakabiliwa na baa la njaa kutokana na mgogoro mkubwa wa kiuchumi unaosababishwa sehemu kubwa na vikwazo vilivyowekwa dhidi ya nchi hiyo na dola za kikoloni za Magharibi kufuatia Taliban kuichukua nchi hiyo mnamo Agosti iliyopita. Nchi hiyo inayotegemea misaada ilikatiliwa mbali kutoka taasisi za fedha za kimataifa, misaada ilisitishwa na dolari bilioni 10 za mali zake zilizuiliwa na utawala wa Marekani usio na utu, na kusababisha matatizo makubwa ya kifedha kwa wakaazi. Kulingana na shirika la ‘Save the Children’, karibu watoto milioni 10 nchini Afghanistan wana njaa kila siku na karibu 50% ya watu (watoto na watu wazima milioni 19.7) wanahitaji msaada wa dharura ili kuishi. Hospitali za umma zinafurika watoto wanaougua utapiamlo mkali.

Watoto na vijana wa Afghanistan hawajui lolote isipokuwa mizozo na ukosefu wa usalama kutokana na ardhi yao kuharibiwa na miongo kadhaa ya uingiliaji kati wa kikoloni na vita ambavyo vimeiangamiza nchi hiyo na kuwaacha kila mara wakihofia maisha yao. Ima wanakabiliwa na mauaji ya kinyama ambapo wanauawa katika mchakato wa kujifunza Dini yao, au hali ya njaa kali na matumbo matupu ambapo hawajui mlo wao mwengine utakuja lini. Hali nchini Afghanistan ni mfano wa matokeo ya utegemezi wa kiuchumi kwa dola za kigeni. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[مَثَلُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِنْ دُونِ اللَّهِ أَوْلِيَاءَ كَمَثَلِ الْعَنكَبُوتِ اتَّخَذَتْ بَيْتًا وَإِنَّ أَوْهَنَ الْبُيُوتِ لَبَيْتُ الْعَنْكَبُوتِ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ]

“Mfano wa walio wafanya walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, ni mfano wa buibui alivyo jitandia nyumba. Na hakika nyumba dhaifu mno kuliko zote ni jumba la buibui, laiti kuwa wanajua.” [Al-Ankabut: 41]. Vile vile inadhihirisha kutengwa, udhaifu na kuwa hatarini kunakotokana na kufuata itikadi ya dola ya kitaifa ambayo inazuia rasilimali na utajiri wa ardhi za Kiislamu kutumika kuwasaidia Waislamu wanaohitaji kutokana na tawala kutedna kwa mujibu tu wa maslahi ya kisiasa na ya kiuchumi ya kitaifa pekee. Kwa hivyo, tunaona Qatar ikitumia zaidi ya dolari bilioni 200 kwenye Kombe la Dunia la kipuuzi, wakati watoto wa Afghanistan na kwengineko katika ulimwengu wa Kiislamu wanakufa kwa njaa. Kutengwa kutokana na kukumbatia falsafa ya dola ya kitaifa pia kuwezesha serikali za kikoloni kuendesha siasa za ardhi hizi, kupitia hata kutumia baa la njaa, au kupanda uharibifu na machafuko.

Je! ni miaka mingapi zaidi kina mama na kina baba wa Afghanistan, Palestina, Yemen, Kashmir na kwengineko watazika watoto wao waliouwawa kinyama katika vurugu, migogoro na uvamizi. Je, ni kwa muda gani zaidi wanapaswa kutazama watoto wao wakiharibika mbele ya macho yao au kufa kutokana na sababu zinazoweza kuzuilika? Dini yetu inatufundisha kwamba nguvu, maendeleo na usalama huja kupitia umoja. Na umoja kama huo hautapatikana bila ya kubomoa mipaka ya kitaifa iliyowekwa na Magharibi ambayo inagawanya ardhi zetu za Kiislamu, na kuungana chini ya kiongozi mmoja, dola moja na mfumo mmoja wa uongozi wa kweli wa Kiislamu - Khilafah kwa njia ya Utume - ambayo itatabikisha Uislamu kikamilifu juu ya ardhi. Ni dola hii pekee ndiyo itakayoondoa giza mara moja kutoka kwa maisha ya watoto wa Ummah huu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur: 55].

Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake

katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu