Ijumaa, 29 Rabi' al-thani 1446 | 2024/11/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Je, Watoto wa Kambi ya Wakimbizi ya Al-Rukban Wataachwa Wafe kwa Baridi na Njaa, Huku Wakikosa Mtu Yeyote wa Kuwaokoa?!

Watoto kumi na tano wasio na makao, wengi wao wakiwa wachanga, wamekufa nchini Syria kutokana na baridi kali na ukosefu wa matibabu, kwa mujibu wa ripoti ya UNICEF mnamo Jumanne 15/1/2019. Watoto, 13 kati yao walio chini ya umri wa mwaka mmoja, walifariki katika kambi ya Al-Rukban kusini mashariki mwa Syria, karibu na mpaka wa Jordan. Al-Rukban na kambi nyenginezo zinakumbwa na uhaba mkubwa sana wa misaada ya kibinadamu, pindi wakimbizi wanapowasili baada ya safari nzito baada ya kukimbia ngome ya mwisho ya ISIS mashariki mwa nchi hiyo. Geert Cappelaere, mkurugenzi wa UNICEF wa eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, alisema “Baridi kali zaidi na hali mbaya za maisha katika Al-Rukban zimesababisha maisha ya watoto kuongezeka kuwa hatarini,” aliongeza, “Kwa mwezi mmoja tu, kwa uchache watoto wanane wamekufa – wengi wao wakiwa chini ya umri wa miezi minne, na mdogo wao zaidi akiwa umri wa saa moja.”   

Soma zaidi...

Majanga Halisi Maovu Hata Bila ya Kuwepo Dhoruba za Barafu

Wakimbizi katika kambi za kinyama kadha wa kadha wameyaomba usaidizi mashirika ya misaada na wametoa wito kwa msaada wa dharura kutoka kwa mamlaka husika. Wamesema kuwa ni kiwango kidogo pekee cha msaada ndio kimewafikia wakaazi katika kambi, ambacho hakitoshi kwa asilimia 10 ya idadi jumla ya wakimbizi katika kambi, katika wakati ambapo kuna uhaba mkubwa wa mafuta na njia za kujikanza moto katika hali mbaya za anga kama hizo ambazo zimelikumba eneo zima la Ash-Sham.

Soma zaidi...

Wanawake Hawawezi Kuheshimiwa Chini ya Nidhamu ya Kijambazi ya Kidemokrasia

Vyombo vya habari nchini Kenya vimeangazia habari kuhusu madhila wanayo fanyiwa wanawake (kina mama) katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH) waliokwenda kutafuta huduma za uzazi katika taasisi hiyo kwamba wanadhulumiwa, kubakwa na kufanyiwa vitendo vyengine visivyo semeka na wahudumu wa hospitali hiyo.

Soma zaidi...

Zogo la Matokeo ya Mtihani wa Kitaifa wa Shule za Upili (KCSE) wa Mwaka 2017 linafichua Kufeli kwa Sera ya Elimu ya Kikoloni ya Kirasilimali

Baada ya kutangazwa matokeo ya mtihani wa KCSE mnamo Disemba 2017, vyombo vya habari nchini Kenya vimeangazia sura tatanishi ya shule, wazazi, wanafunzi na vyama vya wafanyikazi wa sekta ya elimu ambayo mwanzoni katika miaka ya 2015 na kwenda chini ili kuwa ni sura ya bashasha. 

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu